Serikali iwekeze nguvu nyingi kwenye sekta ya Sanaa na Michezo

covid 19

JF-Expert Member
May 9, 2014
4,876
10,590
Ni wazi kabisa tena bila upinzani hii sector pendwa sana wananchi wa Tanzania ipo haja ya serikali sasa kuwa serious na hii sekta na kuitazama kwa macho mawili.

Ni sector inayoweza kuingiza trillion za pesa kwa serikali kama tutadhamiria kweli. Uwejezaji mkubwa kwenye michezo kama ya mpira wa miguu italeta tija na ajira nyingi sana pia ni fursa kujitangaza kiutalii.

Uwekezaji kwenye sanaa hasa muziki na filamu pia utaleta tija na kutoa ajira nyingi kwa vijana pia serikali itapata mapato mengi sana.

Natamani kuanzishwe "art and sports authority" ijikite kwenye kuhakikisha hatimiliki na mapato ya watanzania wengi wenye vipaji na talanta mbalimbali havipotei.

Ila pia ijikite kwenye uwekezaji kwa kusaidia kutafuta wawekezaji wa kimataifa wanaohitajika kwa wingi sana kwenye hii sector.

Tofauti na sasa wawekezaji wa ndani (azam kwenye mpira na wcb kwenye music) ndio wanaibeba hii sector kwa kiwango kikubwa sasa serikali iendeleze kwa kuwashika mkono kutafuta wawekezaji wa nje pia.
 
Hauwezi kufaulu sekta ya filamu bila wahusika kuwa na elimu badala ya kusema watanzania tumejaliwa vipaji hatuhitaji shule.

Hivi karibuni seriksli iliwapa mikopo wasanii bila kuwaandaa jambi ambalo halitaleta tija.
 
Hauwezi kufaulu sekta ya filamu bila wahusika kuwa na elimu badala ya kusema watanzania tumejaliwa vipaji hatuhitaji shule.
Anayetakiwa kusaidia ili wapate elimu ni serikali hiyohiyo.

Iwawezeshe ndio maana ya kufanya uwekezaji maana yake unahakikisha sector inakuwa very modern na ivutie wasomi wengi waingie humo ili mambo sasa yafanywe kitaalam.
 
Anayetakiwa kusaidia ili wapate elimu ni serikali hiyohiyo.

Iwawezeshe ndio maana ya kufanya uwekezaji maana yake unahakikisha sector inakuwa very modern na ivutie wasomi wengi waingie humo ili mambo sasa yafanywe kitaalam.
Serikali imetimiza wajibu wake kwa kuweka kitivo cha sanaa chuo kikuu UDSM kwa zaidi ya miaka 40 sasa, hawajitokezi.
 
Serikali imetimiza wajibu wake kwa kuweka kitivo cha sanaa chuo kikuu UDSM kwa zaidi ya miaka 40 sasa, hawajitokezi.
Najua kipo kitivyo hiko na pia basata na the like ila mimi napendekeza kuwe na overall checking ya hii sector kwa kuifanya ya kisasa zaidi na sio kama ilivyo sasa.
 
Tatizo hizo sekta zinategemea umaarufu wa kipumbavu.

Wasanii hutengenezwa
 
Kwa serikali hii ya ccm sidhani aisee.
taifa letu limejaaliwa wasanii mahili na maarufu zaidi afrika mashariki lakini ndio maskini zaidi.
hakuna ulinzi wa kazi zao wala namna bora ya kuzisambaza wanabaki kuwa matajiri wa majina lakini maskini wa kifedha.

wakati akina michael jackson wanaingiza pesa huku wamekufa kazi za kina kanumba hazijulikani hata zilipo zinauzwa kama njugu mitaani.

akina jay dee kafanya mziki zaidi ya miaka 20 ana nini cha kujivunia zaidi ya kuitwa comando huko mitandaoni?

yaani ukiona mwanao anaimbaimba au anaigiza piga viboko aache kabisa huo upumbavu ,sanaa ni biashara kichaa kabisa bongo hii huku wenzetu wakitengeneza mabilioni.

Ovyo sana hii serikali.
 
Back
Top Bottom