Wakudadavuwa
JF-Expert Member
- Feb 17, 2016
- 17,506
- 15,997
Ndugu zangu,
Kumekuwa na juhudi kubwa kwa vyama vya upinzani kupitia mitandao ya kijamii kupotosha yanayoendelea kuanzia kipindi cha uandikishaji, uteuzi wagombea na hatimaye uchukuaji na urejeshaji wa fomu.
Kipindi cha kujiandikisha walikuja na kampeni susia susia huku wakitoa picha za kuonesha kuwa zoezi la kujiandikisha wapiga kura litakwama, wakafeli wao. Baadaye wamejikuta wakitunga uongo kupitia mitandao ya kijamii kuwa wagombea wa upinzani wanadhulumiwa huku katika kipindi cha kujiandikisha uongozi wa Chadema hususani mkoa wa Kilimanjaro ulikiri kukosa fedha za kuweka mawakala tafsiri pana ni kuwa hata kupata wagombea wa uhakika ni shida.
Baada ya uongo unaosambazwa kupitia mitandao ya kijamii ikiongozwa na Zitto,Lema na ''vikaragosi'' kuonekana kushindwa serikali iwe macho kwani baada ya wao kukosa uhalali kwa wananchi hawatakuwa na ''option'' nyingine zaidi ya kuetengeza mauji, kujeruhi, kufanya vitendo vya kuharibu mali na wizi kwa kuvizia ili tu kuonesha ulimwengu Watanzania ''hawajaridhika''.
Ukizunguka mitaani,vitongojini na vijijini wananchi wanaendelea na shughuli zao kujiletea maendeleo lakini baadhi ya viongozi wa vyama vya upinzani wamejikita kwenye mitandao ya kijamii huku wakitoa vijineno kama vile, ''nchi itawaka moto'', ''wananchi wamechoka'' ili wakija kufanya uhuni wao iwe rahisi kuhalalisha.
Nimalize kwa kusema navishauri vyombo vya ulinzi na usalama viimarishe intelijensia ili kuhakikisha waovu wote wanamulikwa na kuumbuliwa mipango yao.
Nawasilisha kwa mjadala wenye afya.