Nanyaro Ephata

JF-Expert Member
Jan 22, 2011
1,221
1,788
Sakata la Mkurugenzi Jiji la Arusha, Halmashauri inapaswa kuvunjwa

Jana Mbunge wa Michongo wa Arusha mjini alisikika akilalamika mbele ya Waziri Mkuu kuhusu tuhuma kadhaa ambazo zinamkabili Mkurugenzi wa Jiji!

Mosi huyu Mbunge akumbuke kuwa hana uadilifu wa kukemea ufisadi wa aina yoyote maana yeye ni zao la ufisadi. Matendo ya Mkurugenzi ni matokeo ya uchafuzi wa 2020 ambako CCM ilimtumia Mkurugenzi huyu kupora haki za watu wa Arusha, matokeo yake imezaliwa baraza la madiwani la michongo na kibogoyo.

Ni wazi baada ya kumtumia sasa hawana kazi naye, hili liwe funzo kwa wengine wanaotumiwa kupora haki za watu

Kwa mujibu wa sheria za serikali za mitaa, Mbunge ni mjumbe wa baraza la madiwani na ni mjumbe wa kamati ya fedha na utawala ya Halmashauri. Moja ya majukumu ya kamati hii ambayo kisheria inakutana kila mwezi ni kusimamamia mapato na matumizi ya fedha na mali za Halmashauri.

Sasa iliwezekanaje kamati inayokutana kila mwezi na Mbunge akiwepo ishindwe kubaini ubadhirifu mkubwa kama huu?tafsiri yake ni rahisi tu Jiji la Arusha halina mbunge wa madiwani wenye uwezo na weledi. Kamati hii inakutana kwa gharama walipakodi lakini imeshindwa hata kujua kuwa shule yake yenyewe imepangishwa.

Halmashauri ambayo imeshindwa kuendesha shule ni Halmashauri iliyofeli na suluhisho la kudumu ni kuivunja na kuunda tume ya jiji kuelekea uchaguzi mkuu 2025.

Fikiria ujasiri wa mkurugezi kuagiza fedha ziwekwe kwenye akaunti binafsi ya mtumishi au ujasiri wa kukodisha shule,ujasiri huu unatupa picha tu kuwa kuna hitilafu kubwa kwa upande wa madiwani na mbunge wao! Madiwani michongo!
Mbunge michongo! Mkurugezi michongo!

Wakati wanapanga wamachinga niliandika kuhusu ufisadi huu,bajeti ya kupanga wamachinga ilikuwa zaid ya bilioni moja. Ni hatari kutumia mamilioni ya fedha kwa jambo shikizi ambalo sio la kudumu, maeneo ya Machame na Nyire ni open spaces passive, kwa mujibu wa sheria ya mipango miji open space passive haziruhusiwi kufanyiwa maendeleo yoyote, haya ndio baraza la madiwani la michongo liliona ni sehemu ya kuwekeza bilioni moja, sehemu ambazo kibiashara hazina tija na kisheria ni haramu. Hii ni hitilafu kubwa

Tangu hayo masoko shikizi yamejengwa ni zaidi ya miezi eti madiwani na mbunge hawaoni hata mabati kuwa ni geji 32 alafu wanataka waitwe Waheshimiwa, hii hitilafu kubwa.

Kimsingi tangu 2020 shughuli za maendeleo kwenye jiji la Arusha zimesimama kwa kuwa makusanyo ni hafifu na matobo ni mengi

Ni katika siku za karibuni gari la Mkurugenzi limekamatwa huko mkoa wa Kilimanjaro likiwa na mirungi, madiwani wapo kimya, mbunge yupo kimya, hata kama kuna hatua za kipolisi zinaendelea walipaswa kuchukua hatua za kimadili.

Wito wangu kwa mamlaka za Serikali zichukue hatua stahiki mapema na wavunje Halmashauri ili kunusuru mali ya umma.

Nanyaro EJ
 
Kufichua ufisadi hakuhitaji uadilifu ila tunapima uadilifu kwa kuchukia ufisadi. Alichofanya Gambo ni uongozi bora na kupigwa mfano.

Hoja zenu zinapoegemea uadilifu wa zamani wa mtu ni kuonesha kichekesho. Ikiwa watu wanaongoka na kutubu na kuacha njia zao mbaya ,kwani Gambo hawezi kufanya hivyo?

Gambo kajidhihirisha ni mtu mpya na amebadilika na ikiwa kuna lolote lililowahi kufanywa naye kipindi hicho apelekwe kwenye vyombo vya sheria
 
Umejibu kwa ushabiki,ebu soma kwanza kwa utulivu,Gambo ana kikao kinachosimamia Mkurugenzi na timu yake,kwa nini wanamwacha hadi aibe ndio walalamike?
 
Kwanza ile issue ya kuhamisha stendi ya mabasi kujengwa Kiserian na kupeleka kwake, huko mbali vile na mji limeishia wapi?
Gambo anaonekana na mbabe flani hivi japo fisadi. Anajua kuwavizia wenzake
 
Umejibu kwa ushabiki,ebu soma kwanza kwa utulivu,Gambo ana kikao kinachosimamia Mkurugenzi na timu yake,kwa nini wanamwacha hadi aibe ndio walalamike?
Nafikiri hujui utendaji kazi wa mamlaka za Serikali, subiri nikufumbue macho.

Gambo ni mjumbe wa kikao cha baraza madiwani na Baraza la madiwani naweza kulifananisha na bodi ya wakurugenzi katika taasisi za Serikali na kazi yake kubwa ni kusimamia utekelezaji wa mipango ya Halmashauri.

Chini ya baraza la madiwani Kuna chombo Cha utendaji wa shughuli za Halmashauri za kila siku ambacho kinasimamiwa na mkurugenzi ambaye pia ni katibu wa baraza

Nije kwenye swali lako, ni kweli Gambo ni sehemu ya vikao lakini vikao hivyo havijapewa mamlaka ya kuingilia utendaji bali kusimamia na kuputisha miongozo. Kwenye utendaji ndipo Mambo ya aibu yanafanyika ambapo baraza la madiwani kwa kuwa si sehemu ya utendaji kujua kwake ni mpaka vikao vya baraza.

Natumai umepata mwanga kidogo
 
Nafikiri hujui utendaji kazi wa mamlaka za Serikali, subiri nikufumbue macho.

Gambo ni mjumbe wa kikao cha baraza madiwani na Baraza la madiwani naweza kulifananisha na bodi ya wakurugenzi katika taasisi za Serikali na kazi yake kubwa ni kusimamia utekelezaji wa mipango ya Halmashauri...
Mtake radhi Diwani mstaafu wa Levolosi Mh Ephata Nanyaro. Umeniudhi mno kusema Nanyaro hajui hicho ulichokiandika wakati alikuwa diwani wa halmashauri hiyohiyo.

Gambo ni mpuuzi, mfitini na mwenye roho mbaya sana. Hakuna sehemu Gambo alipowahi kuwepo kukawa na amani. Lakini safari hii watakula nae sahani moja. Kagusa pabaya.
 
1 mpaka 11 yote majizi tu...naunga mkono HOJA YA EPHATA WASAFISHWE WOTE TUANZE UPYAA

Tumeanza KAZI
 
Nafikiri hujui utendaji kazi wa mamlaka za Serikali, subiri nikufumbue macho.

Gambo ni mjumbe wa kikao cha baraza madiwani na Baraza la madiwani naweza kulifananisha na bodi ya wakurugenzi katika taasisi za Serikali na kazi yake kubwa ni kusimamia utekelezaji wa mipango ya Halmashauri....
Hii itumie huko huko Ushirombo ndani ndani sio ARUSHA ....
 
Mtake radhi Diwani mstaafu wa Levolosi Mh Ephata Nanyaro. Umeniudhi mno kusema Nanyaro hajui hicho ulichokiandika wakati alikuwa diwani wa halmashauri hiyohiyo.

Gambo ni mpuuzi, mfitini na mwenye roho mbaya sana. Hakuna sehemu Gambo alipowahi kuwepo kukawa na amani. Lakini safari hii watakula nae sahani moja. Kagusa pabaya.
Kuwa diwani hakumaanishi kwamba ana uwezo wa kupewa kila taarifa ya Halmashauri na pia haimaanishi kwamba anajua kuliko wengine.

Kwenye suala la Gambo kuna upotoshaji mkubwa unaendelea lakini bado kaulimbiu yetu ni GAMBO NI MZALENDO, PIMA NA KIHONGOSI WAWAJIBISHWE KAMA NI KWELI WAMEHUSIKA
 
Nafikiri hujui utendaji kazi wa mamlaka za Serikali, subiri nikufumbue macho.

Gambo ni mjumbe wa kikao cha baraza madiwani na Baraza la madiwani naweza kulifananisha na bodi ya wakurugenzi katika taasisi za Serikali na kazi yake kubwa ni kusimamia utekelezaji wa mipango ya Halmashauri.

Chini ya baraza la madiwani Kuna chombo Cha utendaji wa shughuli za Halmashauri za kila siku ambacho kinasimamiwa na mkurugenzi ambaye pia ni katibu wa baraza

Nije kwenye swali lako, ni kweli Gambo ni sehemu ya vikao lakini vikao hivyo havijapewa mamlaka ya kuingilia utendaji bali kusimamia na kuputisha miongozo. Kwenye utendaji ndipo Mambo ya aibu yanafanyika ambapo baraza la madiwani kwa kuwa si sehemu ya utendaji kujua kwake ni mpaka vikao vya baraza.

Natumai umepata mwanga kidogo

Kazi ya Baraza la madiwani ni usimamizi wa utendaji wa halmashauri [ OVERSIGHT FUNCTION}. Hivyo haijalishi wanakutana mara ngapi hata kama ni mara moja kwa mwezi kazi ya usimamizi wa utendaji uko pale pale!! Kumbuka pia kuwa katika Baraza la madiwani kuna kamati zinazosimamia utendaji wa idara mbali mbali ; hizi kamati zinatakiwa kutoa taarifa zake kwa Baraza kila mara Baraza linapokutana.
Mapungufu ya utendaji wa halmashauri yanatakiwa yathibitiwe mapema kabisa kabla hayaharibu kazi za halmashsuri na hiyo ndio mantiki ya kuwa na vikao vya mara kwa mara. Sasa kama baraza na kamati zake zinakutana ; halafu baadae mambo ya hovyo kama vile matumizi mabaya ya mapato ya halmashsuri yanakuja ibuka, baraza lazima liwajibike kwa kutokutimiza wajibu wake!
 
Kazi ya Baraza la madiwani ni usimamizi wa utendaji wa halmashauri [ OVERSIGHT FUNCTION}. Hivyo haijalishi wanakutana mara neap hata kama ni mara moja kwa mwezi kazi ya usimamizi wa utendaji ko pale pale!! Kumbuka pia kuwa katika Baraza la madiwani kuna kamati zinazosimamia utendaji wa idara mbali mbali ; hizi kamati zinatakiwa kutoa taarifa zake kwa Baraza kila mara Baraza linapokutana.
Yuko Ntobo Kahama msamehe....
 
Sasa Kama watendaji wakaamua kuficha baadhi ya taarifa kwa Baraza unadhani Baraza hata likikaa kila siku litajuaje ikiwa wao sio sehemu ya utendaji?
 
Kuwa diwani hakumaanishi kwamba ana uwezo wa kupewa kila taarifa ya Halmashauri na pia haimaanishi kwamba anajua kuliko wengine.

Kwenye suala la Gambo kuna upotoshaji mkubwa unaendelea lakini bado kaulimbiu yetu ni GAMBO NI MZALENDO, PIMA NA KIHONGOSI WAWAJIBISHWE KAMA NI KWELI WAMEHUSIKA
Duh! Gambo mwenyew huyu! Au mcherepuko wake! Kudadek!
 
Sasa Kama watendaji wakaamua kuficha baadhi ya taarifa kwa Baraza unadhani Baraza hata likikaa kila siku litajuaje ikiwa wao sio sehemu ya utendaji?

Kamati za baraza kama zina weledi zitagundua kuwa kuna taarifa zimefichwa na itawaamuru watendaji wazikabidhi. Taarifa za mapato na matumizi ya fedha ni rahisi sana kugundulika kama zimefichwa!!
 
Kamati za baraza kama zina weledi zitagundua kuwa kuna taarifa zimefichwa na itawaamuru watendaji wazikabidhi. Taarifa za mapato na matumizi ya fedha ni rahisi sana kugunduklika kama zimefichwa!!
Weledi gani unauzungumzia kwa kamati za Pima?
 
Back
Top Bottom