Serikali iungwe Mkono Kutengeneza Ajira Milioni 8 Sekta ya Kilimo

Jamal Akbar

JF-Expert Member
Oct 9, 2014
413
471
JUZI, Naibu Waziri wa Kilimo, Anthony Mavunde, amesema serikali Ina mpango wa kutengeneza ajira milioni nane kwa vijana ifikapo mwaka 2025, kutatua changamoto ya ajira.

Kauli hiyo aliitoa bungeni jijini Dodoma, wakati akijibu swali la Mbunge wa Buhigwe, Felix Kavejuru aliyetaka kujua mkakati wa serikali wa kuhusisha vijana katika sekta ya kilimo kuondoa changamoto za ajira kwa kundi hilo.

Mavunde alisema serikali kupitia llani ya Uchaguzi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), ina mpango wa kutengeneza ajira milioni nane kuondoa changamoto ya ajira. Hii ni hatua nzuri, kwani itatatua changamoto kwa baadhi ya vijana ambao wamekuwa wakikimbilia mijini wakihisi ndiko maisha bora yanapatikana kwa urahisi na kukataa kujishughulisha na kilimo.

Tunaipongeza serikali kwa vile imefanya tathmini na kuja na mpango wa kutengeneza ajira hizo ambazo zitakuza uchumi wa nchi kwa ujumla kwani kazi hiyo ikikamilika, vijana wengi watakuwa wanafanya kazi ya kilimo na kukuza uchumi wao binafsi lakini na wa nchi pia, kwani kilimo wanachojiandaa nacho ni kilimo biashara.

Kwa kilimo hiki, sasa wakulima watapata fursa ya kuuza mazao ya ndani na nje ya nchi na kujipatia fedha za kujikimu, lakini taifa nalo litafaidika kutokana na sekta hiyo kuchangia katika pato la taifa. Ni matumaini yetu serikali imejipanga vema kuhakikisha mitaji, miundombinu ya umwagiliaji na masoko ya uhakika itapatikana kwa wakati.

Tunaamini serikali imeanza kuweka mikakati mbalimbali ya kuhakikisha inatatua changamoto hizo na kuvutia vijana kushiriki katika kilimo. Tunaipongeza serikali kwa kuweka mkakati ikiwemo ya mradi wa Jenga Kesho iliyo Bora, ambapo imetenga maeneo ya kilimo na kuwamilikisha vijana.

Ni vema elimu zaidi, ikaendelea kutolewa na vijana wengine waliopo mitaani wakaelewa nafasi nyingine zikitolewa, wajitokeze na kwenda kupata ujuzi wa kilimo cha kisasa.

Tunasema hivyo kwani tunajua wazi kwamba Serikali inayoongozwa na Rais Dk. Samia Suluhu Hasasan ni sikivu na ipo makini ndiyo maana, inaweka miundombinu ya umwagiliaji, inawawezesha kupata mitaji na masoko wanufaike na shughuli za kilimo ili vijana wengi waingie katika sekta kwa maendeleo ya nchi.

Ukweli ni kwamba mradi huo utaweza kutoa hamasa nzuri kwa vijana waweze kujiunga na kuacha mawazo ya kusubiri kazi za kuajiriwa. Rai yetu kwa watendaji wa serikali kuendelea kufanyia kazi hiyo kwa weledi mkubwa na si kufanya hujuma. Ni ukweli shughuli za kilimo zikifanyika kisasa, Tanzania itaweza kupata chakula cha kutosha na kuuza nje ya nchi.

Hapo, tutakuwa tayari tunakuza uchumi wetu na vijana kukuza uchumi wao binafsi na hoja za tatizo la ajira zitakuwa zimefutika. Kwa upande wa vijana, tunawashauri kusubiri taratibu zikikamilika wajitokeze kuomba nafasi hizo​
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom