Bujibuji Simba Nyamaume
JF-Expert Member
- Feb 4, 2009
- 74,893
- 155,911
Mimi na wadau wengine wa mazingira ikiwemo taasisi ya TREE OF LIFE FOUNDATION tuna mpango madhubuti wa kwenda kuwapokea mashujaa wetu waliokaa ughaibuni kwa miongo miwili.Mpango wa Serikali ni kuwarudisha nchini na wataishi kwenye vituo mahususi vilivyotengwa (Chuo Kikuu cha Dar es Salaam-UDSM na Kihansi kuanzia Aprili mwaka huu," alisema Chande na kuongeza kuwa hadi kufikia Julai 2023 vyura wote watakuwa wamerejeshwa nchini na kuwaweka katika maeneo yao ya asili na yale yaliyotengenezwa
Hii nchi ina longolongo nyingi sana huenda hao chura walikufa miaka mingi sana ila wajanja wazito wamewafanya ni mtaji wa ulaji.
Tuliambiwa kuwa vyura hao wakiwa nje ya Kihansi hawawezi kuzaa, hata huko USA 🇺🇸 watakaa muda mfupi kisha warudishwe nchini kwani wako 500 tu dunia nzima.
Vyura wameishi miaka 23 USA, je lifespan ya chura ni miaka mingapi? Maana waliondoka vyura 5⁰0 na wanarudi haohao 500. Hii ina maana kwa miaka 23 hajafa chura hata mmoja?
Ukistaajabu ya Musa utayaona ya Mwaigwisya