Serikali kufuta leseni za Halmashauri, Leseni zote zitatolewa na BRELA

ChoiceVariable

JF-Expert Member
May 23, 2017
43,114
49,840
Nawapa Tano Serikali Kwa uamuzi huu, Sasa ni Mwendo wa biashara tuu.

Pia msisahau kulinganisha matozo ya taasisi zote Ili tulipe mara Moja badala ya kuzunguka kwenye Kila taasisi.

====

Katika kuendelea kuboresha mazingira ya ufanyaji biashara nchini, Serikali kupitia Wizara ya Viwanda na Biashara inatarajia kuanza kutoa leseni zote kupitia Wakala wa Usajili wa Biashara na Leseni (BRELA).

Awali Leseni Daraja A zilizikuwa zikitolewa na Wakala huo na Leseni Daraja B zilikuwa zikitolewa na Halmashauri nchini hali iliyokuwa ikilalamikiwa na wafanyabiashara kote nchini kuwepo kwa urasimu pindi wanapo safirisha bidhaa au mazao kutoka halmashauri moja kwenda nyingine.

Hayo yameelezwa na Waziri wa Viwanda na Biashara, Dk. Ashatu Kijaji alipokutana wafanyabiashara pamoja na wajasiriamali wa Mkoa wa Dodoma kwa ajili ya kuwasikiliza pamoja na kutatua changamoto zinawazowakabili.

“Kumekuwa na malalamiko kutoka kwa wafanyabishara juu ya hizi leseni zinazokatwa na Halmashauri. Mfano nikiwa na leseni niliyokata Bahi nikiwa napeleka mzigo wangu Chamwino nikipita Dodoma Jiji wananikamata wanataka niwe na leseni ya Jiji na nikifika Chamwino wananikamata wanataka niwe na leseni ya Chamwino. Sasa huu ni usumbufu, hatumsaidii Mhe Rais. Mtu akitoka Kagera kama anapeleka bidhaa Dodoma si atakuwa na leseni 10,” alihoji Waziri Kijaji.

“Tulichokiamua tutakuwa na leseni moja itakayokatwa kupitia BRELA itakayokuwezesha kufanya biashara nchi nzima. Hicho tutakwenda kukifanya ili dhamira ya Mhe Rais wetu ya kurahisisha mazingira ya uwekezaji nchini,” amesema Dk. Kijaji.

Waziri Kijaji amesema kuwa awali Halmashauri zilipewa mamlaka hiyo ya kukata leseni za biashara kutokana na mifumo ya upatikanaji wa leseni zamani ilikuwa ni lazima mfanyabiashara asafiri kwenda Dar es Salaam kwa ajili ya kupata leseni ya biashara lakini kwa sababu ya maendeleo ya Sayansi na Teknolojia wananchi hawana sababu tena ya kusafiri kwenda Dar Es Salaam kwa ajili kupata.

Waziri wa Viwanda na Biashara Mhe Dkt. Ashatu Kijaji (Mb) amesema Serikali iko mbioni kuunganisha leseni ya biashara inayotolewa na Wakala wa Usajili wa Biashara na Leseni (BRELA) na Halmashauri kuwa leseni moja ya biashara itakayowawezesha kufanya biashara Nchi nzima.

Dkt. Kijaji ameyasema hayo Agosti 17, 2023 wakati akijadiliana kuhusu maendeleo ya biashara na Wafanyabiashara wa Mkoa wa Dodoma katika Ukumbi wa Ofisi za Mkuu wa Mkoa ikiwa ni mwendelezo wa mikutano hiyo katika kila mkoa ambapo Dodoma ni Mkoa wa Saba baada ya Arusha, Kilimanjaro, Tanga, Pwani, Morogoro Mbeya na Songwe.

Aidha, Dkt. Kijaji amewashauri wafanyabiashara wa Mkoa wa Dodoma kusajiri biashara zao, kuwa waaminifu katika kurudisha mikopo na kuchangamkia fursa za biashara kwa kuwa Dodoma ni Makao Makuu ya Nchi pamoja na fursa za kibiashara katika masoko ya EAC, SADC, AGOA na AfCFTA yenye soko lenye jumla ya watu bilioni 1.3 bila kutozwa kodi wala ushuru wowote.

Dkt. Kijaji pia amesema Wizara yake inaendelea kutekeleza Mpango wa Kuboresha Mazingira ya Biashara na Uwekezaji nchini (MKUMBI) ambapo hadi sasa imefuta au kupunguza Tozo, Ada na Faini 374 kati ya 380 na katika kipindi cha 2023/24 Tozo, Ada na Faini 67 zimefutwa au kupunguzwa.

Naye Naibu Waziri wa Viwanda na Biashara Mhe. Exaud Kigahe akijibu Baadhi ya changamoto za wafanyabiashara hao amesema Serikali inatambua umuhimu wa sekta binafsi na itaendelea kuishirikisha katika utekelezaji wa miradi mbalimbali nchini pamoja na jitihada za uboreshaji wa mazingira ya biashara nchini.

Kwa upande wa Kaimu Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Viwanda, Biashara, Kilimo na Mifugo Mhe. Fransis Mtinga aliwahakikishia wafanyabiashara hao kuwa Kamati hiyo iko tayari kushughulikia changamoto zote za kisheria na sheria ndogo zinazowakabili katika ufanyaji biashara.

Naye Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Bi. Rosemary Senyamule amemhakikishia Waziri Kijaji kuwa Mkoa wake kwa kishirikiana na wadau mbalimbali utashughulikia changamoto zote ziliowasilishwa na wafanyabiaahara hao ikiwemo utoaji wa mafunzo kwa wajasiliamali na kuanzisha kituo cha huduma za pamoja za kuhudumia wafanyabiashara.View attachment 2720693View attachment 2720694View attachment 2720695View attachment 2720697View attachment 2720696View attachment 2720698
20230818_124522.jpg
 
Jambo zuri. Ila hizo pesa zitarudishwa halmashauri husika. Maana pesa zote nazo kwenda serikali kuu na kisha wakubwa huko ndiyo wakaamua yule mupe yule muruke si jambo zuri hata kidogo.

So nikiwa na leseni ya BRELA nafungua duka langu popote? Rushwa pekee nitakayotoa ni kuwalipa halmashauri husika waniambie kama hiyo sehemu inafaa kuweka baa? Nzuri hii.
 
Inaanza lini Hii?
Maana biashara z kusafirisha ni kipengele.

Tena Kodi ilikilipiwa Kwa mfumo wa digital itakuwa Pouwa Sana
 
Nawapa Tano Serikali Kwa uamuzi huu, Sasa ni Mwendo wa biashara tuu.

Pia msisahau kulinganisha matozo ya taasisi zote Ili tulipe mara Moja badala ya kuzunguka kwenye Kila taasisi.

====

Katika kuendelea kuboresha mazingira ya ufanyaji biashara nchini, Serikali kupitia Wizara ya Viwanda na Biashara inatarajia kuanza kutoa leseni zote kupitia Wakala wa Usajili wa Biashara na Leseni (BRELA).

Awali Leseni Daraja A zilizikuwa zikitolewa na Wakala huo na Leseni Daraja B zilikuwa zikitolewa na Halmashauri nchini hali iliyokuwa ikilalamikiwa na wafanyabiashara kote nchini kuwepo kwa urasimu pindi wanapo safirisha bidhaa au mazao kutoka halmashauri moja kwenda nyingine.

Hayo yameelezwa na Waziri wa Viwanda na Biashara, Dk. Ashatu Kijaji alipokutana wafanyabiashara pamoja na wajasiriamali wa Mkoa wa Dodoma kwa ajili ya kuwasikiliza pamoja na kutatua changamoto zinawazowakabili.

“Kumekuwa na malalamiko kutoka kwa wafanyabishara juu ya hizi leseni zinazokatwa na Halmashauri. Mfano nikiwa na leseni niliyokata Bahi nikiwa napeleka mzigo wangu Chamwino nikipita Dodoma Jiji wananikamata wanataka niwe na leseni ya Jiji na nikifika Chamwino wananikamata wanataka niwe na leseni ya Chamwino. Sasa huu ni usumbufu, hatumsaidii Mhe Rais. Mtu akitoka Kagera kama anapeleka bidhaa Dodoma si atakuwa na leseni 10,” alihoji Waziri Kijaji.

“Tulichokiamua tutakuwa na leseni moja itakayokatwa kupitia BRELA itakayokuwezesha kufanya biashara nchi nzima. Hicho tutakwenda kukifanya ili dhamira ya Mhe Rais wetu ya kurahisisha mazingira ya uwekezaji nchini,” amesema Dk. Kijaji.

Waziri Kijaji amesema kuwa awali Halmashauri zilipewa mamlaka hiyo ya kukata leseni za biashara kutokana na mifumo ya upatikanaji wa leseni zamani ilikuwa ni lazima mfanyabiashara asafiri kwenda Dar es Salaam kwa ajili ya kupata leseni ya biashara lakini kwa sababu ya maendeleo ya Sayansi na Teknolojia wananchi hawana sababu tena ya kusafiri kwenda Dar Es Salaam kwa ajili kupata.

wale ambao wameshalipia mwaka mzima wanawaweka fungu gani?
 
Back
Top Bottom