Serikali tunaomba mfute ada za Leseni ya Biashara

BROKE BOYS

JF-Expert Member
Jan 12, 2019
13,218
39,048
IMG_0823.png


Kabla hatujafika mbali embu tuzitambue kodi zinazolipwa na wafanyabiashara hapa Tanzania. Mfanyabiashara mmoja anaweza kuwa analipa hizi kodi zote:
1. Withholding Tax
2. Stamp duty
3. Income Tax/ Makadirio
4. VAT
5. PAYEE
6. SDL
7. Ada na shuru mbalimbali za Forodha
8. Ada za Leseni Manispaa
9. Service levy 0.3%
10. Taka
11. Fire
12. OSHA
13. NEMC nknk

Hivi hizi ada za Leseni na service levy kwanini Serikali isizifute? Ni kivipi mtu alipie service levy 0.3% kila mwaka wakati analipa kodi? Na kwanini leseni ya biashara itolewe na Manispaa na sio TRA, kwa mfanyabiashara anayelipa kodi, why asipewe na leseni bure?

Unalipa kodi kila mwaka bado tena leseni ukalipie manispaa, sio fair kwakweli. Serikali mnatupa mizigo mikubwa wafanyabiashara. Kodi zinakua nyingi lakini mazingira ya biashara bado mabovu ukienda kule bandarini kuna uozo kibao Rushwa nje nje. Ndomana watu kwa sasa wanaona bora watumie bandari za Zanzibar na Kenya kidogo ni cheap.

Serikali futeni baadhi ya makodi hayana maana bali mnazidi kuongeza wigo wa watu kukwepa kodi. Mwisho wa siku utajikuta unaifanyia biashara serikali wewe huoni unachokipata.

Tunalipa hizo kodi zote lakini hakuna return yoyote tunayopata kutoka serikalini. Serikali mnashindwa hata kulipia Pesa ya taka wakati tunalipa makodi kibao. Nchi za wenzetu wanalipa Pesa ya mazingira kwa wafanyabiashara.

Mnasema kulipa kodi ni uzalendo lakini sio kwa Mikodi hiyo huko ni kukomoana.
 
Back
Top Bottom