labda tujiulize, ile faida wanayopata, anapata mtanzania au mtu wa nchi za nje, na akiiipata si atakuwa amepata kipato kikubwa zaidi kuboresha hospitali yake? kuna nchi zingine hadi serikali huwa una bailout baadhi ya taasisi zinazohudumia wananchi, ukweli uliopo ni kwamba hao waliojitolea kufungua hospitali binafsi wamesacrifice sana hadi kufikia hatua hiyo, ilitakiwa iwe kazi ya serikali tuliyoiweka na hatutakiwi kulichukulia hili kama vita kati ya serikali na hospitali binafsi, wasababu hata hivyo bima wanazopokea sio za NHIF tu, na zingine pia, kwanini wao tu NHIF ndio waonekane na mgogoro, bima zingine za binafsi huko hawana shida? kuna uwezekano mkubwa shida ni serikali na sio hospitali binafsi.
hivi mashirika binafsi ya bima yanaweza kukubali kuendelea kuibiwa (kama kuibiwa kupo) kuliko serikali? kwanini bima za mashiriak binafsi hazina shida, hawalalamiki kuibiwa, ni hizi tu za serikali? serikali ina hospitali za kutosha? kwanini msikae mezani mkakubaliana kuliko kupigana wakati ninyi mlioko serikalini wenye kutoa maamuzi mnatibiwa south africa? mna uwezo, wale wasio na uwezo mnawatoa kafara?