Serikali inavyowakomoa walimu

Serikali inavyowakomoa walimu

Tatizo ni maofisa utumishi, tsc na afisa elimu wake. Hii mijitu haipendi kuona mtu kawazidi kielimu. Wanachofanya ni kumfrastrate hadi aache kazi. Huyo ni mfano mmoja tu. Halimashauri zetu zimejaa mashetani yaani tena shetani ana unafuu anaweza kukuacha upumue. Hawa wamekuwa miiba tena mbigili kwenye haki za watumishi. Serikali iweke mfumo rasmi wa watumishi kupeleka malalamiko yao I'll kuondoa huu ukiritimba wa kuwategemea hawa viwavi,!!!
Kwa Sasa tamisemi Wana call center ya kupokea malalamiko toka kwa watumishi...
 
Malisa acha uongo haiwezekani mwalimu ana miaka zaidi ya miaka kumi na tano akalipwa mshahara ule ule alioajiliwa nao...
Upo sahihi . Mimi ni mdau wa elimu na mzoefu wa masuala ya elimu kuanzia ufundishaji darasani, utawala wa elimu na masuala ya upandaji wa madaraja kwa walimu.

Ningeweza kuandika mengi tu kwa faida ya wanajamvi lakini nahofia nitawachosha. Kwa kifupi sana km aliyoandika Bwana Malisa ni ya kweli, mwalimu huyo atakuwa anakabiliwa na haya yafuatayo:-

1. Tatizo la maadili.

2. Mahusiano mabovu na wasimamizi wake wa kazi hasa Idara
ya Elimu katika eneo husika.

3. Intervals za ruhusa zake za kwenda masomoni, nazo zaweza kuwa kigezo , ufafanuzi unatakiwa hapa.

4. Kama anajihusisha na lobbying kwa wanasiasa hasa madiwani katika kufanikisha ndoto zake, hilo ni tatizo katika utendaji wa Idara ya Elimu.

Masuala ya upandaji wa madaraja huhusisha TSC zamani TSD na Idara ya Utumishi katika Halmashauri husika. Kwa maana hiyo, mleta mada amelishwa maneno ambayo kimsingi naweza kusema ni ya mwamba ngozi pamoja na kwamba sekta ya elimu bado ina changamoto nyingi sana hapa nchini.

Naweza kukosolewa au kuulizwa maswali zaidi.
 
Upo sahihi . Mimi ni mdau wa elimu na mzoefu wa masuala ya elimu kuanzia ufundishaji darasani, utawala wa elimu na masuala ya upandaji wa madaraja kwa walimu....
Kwa kiasi Fulani uko sahihi, tatizo pia linguine la walimu ni kutojua haki zao, huenda mwalimu kajiendeleza hata taarifa zake hajaziwasilisha wilayani kwa mfano vyeti na barua kuomba kubadilishiwa muundo....changamoto kubwa za watumishi wengi kutojua haki zao
 
Upo sahihi . Mimi ni mdau wa elimu na mzoefu wa masuala ya elimu kuanzia ufundishaji darasani, utawala wa elimu na masuala ya upandaji wa madaraja kwa walimu...
Kama ana tatizo la maadili kwanini asichukuliwe hatua badala ya kumuacha aendelee kuharibu hapo alipo ? halafu hata kama ni unyama wa kumkomoa, mtu mwenye elimu ya kiwango chake ni sawa kweli kufundisha shule ya msingi ?

Napata picha kwamba ili upandishwe cheo ni lazima ulambe miguu ya wakubwa hata kama unastahili ili ionekane una maadili mema .

Hii nchi hata kuiombea ni sawa na kumtukana Mungu tu
 
Huku wanasema mwalimu ukijiendeleza ukipata Masters or PhD yako utasikia eti mwajiri hana shida na hiyo elimu yako wao wanadai kuwa maximum ni degree

Haiishi hapo wanasema vyeti hivyo ni additional qualifications a.k.a wanakuita 'Over Qualified (OQ)'

Nadhani kuna haja ya kuangalia mtu mwenye elimu yake alipwe

Mfano Masters au PhD mnasoma pamoja wengine wanaenda vyuo vikuu halafu wanalipwa tofauti, wanaoenda vyuo vya ualimu wanalipwa juu kidogo wanaenda primary au sekondari unarudi na tgts D au E. Lakini shule nimesoma moja na qualifications sawa na pengine mmewazidi kabisa

Yaan unafikiria mpaka unashangaa any way ngoja tukaze tu
 
Huko Ujerumani kuna maslahi .na walimu wanathaminiwa sio kama hapa.
Ndio maana akifundisha chekechea huko na kulipwa vizuri hana muda wa kuhangaika kutafuta maslahi.

Ulaya kwa ujumla, katika kazi za umma (public service), ualimu na polisi ni kazi zenye kuthaminiwa sana. Hata vigezo na mchakato wa kuajiriwa huko ni makini hasa.
 
Kama ana tatizo la maadili kwanini asichukuliwe hatua badala ya kumuacha aendelee kuharibu hapo alipo ? halafu hata kama ni unyama wa kumkomoa , mtu mwenye elimu ya kiwango chake ni sawa kweli kufundisha shule ya msingi ?...
Km utakuwa umenielewa vizuri, maadili ni kipengele kidogo kati ya factors nilizoainisha. Si suala la kulamba miguu ya bosi wake ili apate haki yake, la hasha.

Matatizo ya walimu yapo tangu nchi ipate uhuru na yanaendelea kuongezeka kila uchao. Kimsingi kada hii naweza kusema ndiyo kada dhaifu sana kimaslahi . Cha ajabu ndiyo kada inayoongoza kwa watumishi wake kujiendeleza na baada ya hapo wengi wao hubadili uelekeo na kujiunga na kada nyingine.

Mbali na matatizo ya sekta hii, walimu pia wana matatizo yao binafsi na bila kubadilika kifikra, kamwe kada hii haitajikwamua.

1. Uoga wa kuwasilisha hoja zao. Hubaki kulalamika tu.
2. Wepesi kudanganyika kwa ahadi hewa.
3. Hawana umoja.
4. Hawajui kudai haki zao za msingi hasa utunzaji na uwasilishaji nyaraka muhimu za utumishi wao kwa wakati.
5.Kutokujua haki na wajibu wao ipasavyo.

Kwa hali hii, matatizo ya walimu hayataisha leo wala kesho. Kada hii ina changamoto lukuki kuanzia maslahi, vitendea kazi, mazingira ya kazi na makazi pamoja na uongozi wa sekta hii kwa ngazi mbalimbali.
 
Upo sahihi . Mimi ni mdau wa elimu na mzoefu wa masuala ya elimu kuanzia ufundishaji darasani, utawala wa elimu na masuala ya upandaji wa madaraja kwa walimu...
Malisa amekurupuka secta ya elimu ina changamoto ila changamoto nyingine ni historia yani hazipo tena.

Waswahili wanasema mnyonge mnyongeni ila haki yake mpeni serikali pamoja na mapungufu yake kuna baadhu ya mambo.

umeyapunguza mfano suala la madai kuna kundi dogo sana la madai kwa sasa ukilinganisha na miaka ya zamani
 
Kama ana tatizo la maadili kwanini asichukuliwe hatua badala ya kumuacha aendelee kuharibu hapo alipo ? halafu hata kama ni unyama wa kumkomoa , mtu mwenye elimu ya kiwango chake ni sawa kweli kufundisha shule ya msingi?..
Dhana ya maadili ni pana sana nakupa mfano mdogo tu pengine unakosa nidhamu ya siri yani wewe mlopokaji sasa hapa utachukuliwa hatua gani yani hujui kukaa na siri wewe kila jambo unalopoka tu watu wakikupima wanaona katika uongozi utoshi kwani kuna vitu vya usiri
 
Ukimaliza kusoma inabidi utumikie miaka 3 ili upande daraja. Labda jamaa kabla ya miaka 3 akachomoka kwenda shule aliporudi kabla ya mitatu akachomoka tena ongeza miaka ya uhakiki, ongeza miaka ya mapito 2014-2021
Malisa acha uongo haiwezekani mwalimu ana miaka zaidi ya miaka kumi na tano akalipwa mshahara ule ule alioajiliwa nao...
 
Huyo mwalimu kwa muda wa miaka 15 atakuwa alikuwa amepanda daraja mpaka kufikia walimu wenye degree yaani Tgts D au E hivyo basi hawezi kupanda daraja tena kwa kutumia elimu yake, masters na postgraduate hazina scale ya mishahara serikalini.
Kama yupo chini ya daraja D yaani B au C ana haki ya kulalamika lakini kama ni D kupanda juu mwambie ale mtori nyama ziko chini.

Halafu mshauri awe mpole anaweza kupewa hata ualimu mkuu akapata posho ya madaraka akapooza machungu, inavyoooneka ana kiburi na dharau na kujiona amesoma sana wakati masters ni elimu ya kawaida sana tena Kuna vijana wengi wanazo na bado ni machinga tu mtaani.
 
Binafsi nimeumia sana kwasababu ya kutopanda daraja kutokana na elimu yake lakini kuhusu nafasi yake katika kazi sijaona ubaya.

Labda nikupe mfano “ Nina mdogo wangu yupo ujerumani alipata chance kipindi cha Corona kutibu wagonjwa katika nchi ya ujerumani, yeye kajiongeze na kuendelea kujiendeleza kimasomo. Nikiwa nawasiliana nae ananiambia walimu wa awali katika nchi ya hiyo ni watu wenye elimu kubwa tu na tofauti na hapa Tanzania “

Binafsi natamani walimu wa awali wawe na elimu ya juu ili kuwapa knowledge kubwa vijana wetu.
Wana elimu kubwa kwenye gani,kwakukusaidia tu ni kwamba sio km ya huyu,mfumo wao na kwetu ni tofaut,specialization ni primary hadi Phd sis kwetu haiko hivi!Kwa kuongeza ujeruman ni moja ya nchi inayolipa walim vzr kuliko mtumishi yeyoye
 
Wana elimu kubwa kwenye gani,kwakukusaidia tu ni kwamba sio km ya huyu,mfumo wao na kwetu ni tofaut,specialization ni primary hadi Phd sis kwetu haiko hivi!Kwa kuongeza ujeruman ni moja ya nchi inayolipa walim vzr kuliko mtumishi yeyoye

Mitigator!! Mimi nipo kwenye maslahi ya mwalimu sio position alikuwepo! Mwalimu alipaswa kupata haki take.

Ndio maana ukifatilia comment zangu nilitaka serikali waweke kiasi cha mshahara usioleta daraja kubwa kwa watumshi. Mpka watu wanatafu nafasi ili wapate kiasi hicho ndio maana watu wanarogana
 
Malisa acha uongo haiwezekani mwalimu ana miaka zaidi ya miaka kumi na tano akalipwa mshahara ule ule alioajiliwa nao

Watu ambao wanalipwa mishahara ilel ile kwa walimu ni kundi la ajira mwaka 2014 chini ya hapo hakuna hiyo moja

Pili serialini hakuna mshahara wa masters kuna mshahara wa degree hizo masters ni weredi upatapa maslahi yake endapo utapata position yenye posho ya ukuu wa hicho kitengo mfano masters yake nk inauwezo wakumpa nafasi ya uafisa elimu,

USHAURI
Kama ana phd na bado yupo darasani mwambie andike barua kwa katibu mkuu wizara ya elimu akijielezea wasifu wake na aombe nafasi anayoona anastahili kwa kusema anatuma maombi yake ikiwa nafasi itatokea basi yeye yupo

DOUBT
Uyo mwalimu achunguzwe atakuwa ana sifa ya elimu ila sifa ya kimaadili kama mtumishi wa umma anayestahili kupewa promition hana yani watu wa veting wakimpitia wanaona kasoro

ndio maana anasoma akimini kusoma kutamsaidia hawazi madili ya utumishi wa umma je anafaa

Kwa sababu kita halmashauri kila mwaka huwa zinachukua tarifa za watumishi kuhusu elimu nk tarifa hizo hzikai halmashauri tu zinaenda mpaka utumishi kwaiyo kwa elimu yake na mda aliokaa kazini lazima wangemuona wangeuliza uyu mtu tunamuitaji so mwambieni ajichunguze atakuwa na tatizo tusishie kulaaumu tu
Wewe utakuwa ni Afisa Elimu bila shaka!! Au ni Mtumishi wa Tamisemi!! Siyo kwa ufafanuzi huu uliokwenda shule.
 
Back
Top Bottom