Serikali inavyowakomoa walimu

Serikali inavyowakomoa walimu

Binafsi nimeumia sana kwasababu ya kutopanda daraja kutokana na elimu yake lakini kuhusu nafasi yake katika kazi sijaona ubaya.

Labda nikupe mfano “ Nina mdogo wangu yupo ujerumani alipata chance kipindi cha Corona kutibu wagonjwa katika nchi ya ujerumani, yeye kajiongeze na kuendelea kujiendeleza kimasomo. Nikiwa nawasiliana nae ananiambia walimu wa awali katika nchi ya hiyo ni watu wenye elimu kubwa tu na tofauti na hapa Tanzania “

Binafsi natamani walimu wa awali wawe na elimu ya juu ili kuwapa knowledge kubwa vijana wetu.
Aliendaje Ulaya wkt ndege hazipo? alipaa!! Tza ndo walikuwa hawatakiwi kabisaa ajili ya lugumya aliktaaga chanjo yule!! yaani ujermani waajili asiye kuwa na chanjo?
 
Jingine, kwa mitihani ya kumaliza kidato cha nne 2021, wasimamizi ni walimu wa msingi wenye degree, na walimu wasimamizi kutoka sekondari wanadiploma, wenye masters wameachwa! Sasa utajiuliza elimu yetu inamaana gani, ukiwa wasome hawanamaana
 
Aiseee hadi inasisimua
Mwezi February niliweka hapa taarifa ya Mwalimu mmoja mkoani Arusha ambaye ana astashahada ya ualimu (Teaching Certificate), Bachelor Degree ya Ualimu (B.A with Education), Postgraduate Diploma in Special education (aliyoipata huko Norway) na Masters Degree ya usimamizi wa Elimu (Master of Education - Planing &Administration).

Lakini Mwalimu huyo amekuwa akilipwa mshahara wa certificate na bado anafundisha MAGAZIJUTO darasa la 3B.

Nilimuandikia Naibu Waziri wa TAMISEMI, Mhe.Silinde Ernest David kumuomba mambo mawili. Moja huyo mwalimu abadilishiwe muundo wa mshahara ili alipwe kwa viwango vya Mwalimu mwenye degree, na pili kama ikipatikana nafasi Mwalimu huyo aondolewe shule ya msingi apelekwe sekondari au vyuo vya kati akatumike vizuri. Kumuacha msomi kama huyu kuimba mabata madogo madogo ni matumizi mabaya ya rasilimali.

Napenda kutoa mrejesho kwamba Mhe.Silinde alilifanyia kazi suala hilo, aliwasiliana nami, baadae akawasiliana na Mwalimu huyo pamoja na uongozi wa Halmashauri anayofanyia kazi. Tayari amebadilishiwa muundo wa mshahara, kwa sasa analipwa kwa kiwango cha mwalimu mwenye degree. Pia Silinde ameahidi kufanyia kazi suala la kuhamishiwa vyuo vya kati. Amesema kwa sasa hakuna nafasi lakini zikipatikana Mwalimu huyo atapewa kipaumbele.

Nitumie fursa hii kumpongeza Mhe.Silinde kwa kuchukua hatua kwa haraka. Pia aendelee kugusa maisha ya watumishi wengine wa wizara yake hata wale ambao hawapati fursa ya kusemewa kama huyu. Hongera Silinde. Tutawapongeza mnapofanya vizuri, na kuwakosoa mnapoboronga. We give credit where credit is due.

Mawaziri wengine pia waige hili. Zile zama za kuogopa kufanyia kazi matatizo yanayoibuliwa na upinzani zimepitwa na wakati. Mama amesema tufungue ukurasa mpya kwa maslahi ya watanzania wote.!

GJ Malisa
 
Ualimu ndo Kada itoayo viongozi wakuu miaka yote 90% walikuwa walimu wakilalamika kama walimu ,ila tu ule msemo wa aliyeshiba.......
Mwalimu ilitakiwa awe na pesa nyingi kuliko mbunge.
 
Ualimu ndo Kada itoayo viongozi wakuu miaka yote 90% walikuwa walimu wakilalamika kama walimu ,ila tu ule msemo wa aliyeshiba.......
Mwalimu ilitakiwa awe na pesa nyingi kuliko mbunge.
Kuna uhalisia fulani.mfano uchaguzi uliopita walimu walitumika vibaya sana kuiba kura
 
Kuna watu Wana Diploma na wengine Bachelor ndiyo wamepata uteuzi katika Ofisi za serikali. Kwa Nchi yetu kinachoangaliwa ni unafahamiana na nani? He Una ndugu yako au rafiki yako anayeweza kukusemea? Vinginevyo turidhike kufanya kazi popote Kwa ajili ya Watanzania wenzetu. Ni vema vyombo vinavyohusika vikawa makini kufanya maamuzi yenye tija Kwa ajili ya Taifa letu
 
Baada ya kuelezea 'scenario' ya jana rafiki yangu mmoja amenitafuta. Ni rafiki yangu wa muda mrefu, lakini sikuwahi kujua sana kuhusu upande wa pili wa maisha yake.

Yeye ni firstborn kwenye familia. Baba yake alifariki akiwa kidato cha 3, hivyo alipomaliza kidato cha 4 aliamua kusomea ualimu (grade III) ili asaidie wadogo zake. Pamoja na kufaulu vizuri lakini kwenda form five angeshindwa kulea wadogo zake.

Akasomea ualimu na kuhitimu. Akapangiwa shule ya kufundisha mkoani Arusha. Akaweza kujikimu na kusaidia wadogo zake kusoma. Baadae akaamua kujiendeleza kidato cha 5&6 kama Private Candidate. Akafanya mtihani na kupata division 2 ya points 10. Yani alama moja tu apatae division 1.

Akapata udahili chuo kikuu. Akaomba ruhusa kwa mwajiri wake akapewa. Akasoma shahada ya kwanza ya ualimu. Enzi hizo walimu wa shahada hawakua wengi kama sasa. Lakini aliporudi kwa mwajiri (DED) hakumpandisha daraja wala kumuongezea mshahara. Akaendelea kufundisha shule ya msingi na degree yake, kwa mshahara uleule wa mwalimu wa certificate.

Hakuvunjika moyo. Baada ya muda akajiunga tena chuo kikuu kusoma shahada ya uzamili ya usimamizi wa elimu (Master of Education - Planing &Administration). Akahitimu kwa ufaulu mzuri. Akarudi kwa mwajiri lakini hakumuongezea mshahara wala kumbadilisha daraja.

Wakati huo mambo ya uhakiki yalikua yakiendelea. Uhakiki ukamalizika lakini hakupandishwa daraja wala kuongezewa mshahara. Akaendelea kufundisha shule ya msingi kwa mshahara uleule wa "certificate" bila kujali elimu yake ya "masters degree"

Baadae akapata ufadhili chuo kimoja nje nchi, kusoma Stashahada ya uzamili ya Elimu maalumu (Postgraduate Diploma in Special Education). Akapewa ruhusa ya kwenda kusoma. Akahitimu na kurudi kwa mwajiri wake. Akarudishwa kulekule shule ya msingi, bila kubadilishwa daraja wala kuongezewa mshahara.

Kwahiyo nchi hii ina mwalimu wa shule ya msingi mwenye Certificate ya Ualimu, Bachelor Degree ya Ualimu, PGD ya elimu maalumu na Masters Degree ya usimamizi wa Elimu. Lakini serikali imeamua kumtumia kuimba "mabata madogo madogo" na watoto wa darasa la 3B. Just imagine.!

Halafu akipata kazi nje ya nchi mnasema si mzalendo. Au akipata kazi sekta binafsi akaondoka serikalini mnasema amekimbia sababu ya maslahi, mnaagiza akamatwe na huko alikoenda hiyo taasisi ifungiwe. Hivi serikali ikoje? Yani nyie mmeshindwa kumtumia na hamtaki wengine wamtumie. Roho ya kichawi hii.!

Mtu kama huyu alitakiwa awe mahali ambapo ataweza kutumia elimu, uzoefu na vipawa vyake kwa manufaa ya taifa, sio kufundisha MAGAZIJUTO darasa la 3B. Lakini amehangaika sana kupandishwa daraja bila mafanikio. Mbaya zaidi analipwa mshahara uleule kama mwalimu mwenye certificate.

Kinachoumiza zaidi ni analipwa mshahara wa cerificate halafu HESLB wanamkata 18% ya mshahara huo kufidia mkopo waliompa wakati akisoma Degree, wakati degree yenyewe haijamsaidia. Mlipeni basi mshahara wa degree ili mkimkata mkopo kuwe na logic. Sio mnamlipa mshahara wa certificate halafu manamkata mkoko wa degree. Ilogical.!

Naomba Mhe.Silinde Ernest David ulione hili na kulifanyia kazi ukiwa kama Naibu Waziri mwenye dhamana. Hali hii inavunja sana moyo watumishi. Mchukueni kijana huyu mtafutie mahali panapomfaa kulingana na elimu na uzoefu wake.

Kama mlikua hamtaki kutumia elimu yake kwanini mlikua mnampa ruhusa ya kwenda kusoma? Mmempa na mkopo ambao anateseka kuulipa lakini elimu aliyochukulia mkopo hamtaki kuitumia. Jamaa yuko very frustruted, kwa sababu ana familia inamtegemea na kipato hakitoshelezi. Tumuombee asije kufanya maamuzi magumu kama yule wa Pugu.

Mwalimu mwenye uzoefu wa miaka zaidi ya 15, msomi Cert, BA, MA, PGD mmeshindwa kabisa kumtumia kwa tija? Mpelekeni basi hata vyuo vya kati akafundishe, na mumlipe kwa hadhi ya elimu yake. Kumuacha shule ya msingi ni matumizi mabaya ya rasilimali, na kuendelea kumlipa mshahara wa Certificate ni UONEVU usiovumilika. Si ajabu amewazidi hata "maboss" zake elimu na uzoefu.

Tafadhali lifanyie kazi hili litakupa heshima wewe na serikali yenu. Weka alama kwenye maisha ya huyu Mwalimu. Wasiliana nami kwa maelezo zaidi. Namba yangu ni ileile, naamini ulipohama 'chama' hukuifuta.!

Malisa GJ
Huyo Lusinde degree holder,atamfikilia mtu mwenye PhD ili achekwe? Hapo yeye kaingia huko kisa njaa Sasa mwenye njaa akipata na kushiba hamwangalii mwenye shida! Huon akienda mikoan anavyowaharasi watumishi utadhan yeye anajua Kila kitu tena kwa sifa
 
Back
Top Bottom