Serikali Imewekwa Mfukoni na Kampuni ya Multichoice!

Serikali Imewekwa Mfukoni na Kampuni ya Multichoice!

nyiue watu nyie TBC iko DSTV free of charge tena serekali ndio ili walazimisha kwamba TV ya taifa ni sharti iwe bure haya ni maelezo kwa mujibu wa TCRA wenyewe,swala la private TV station kama itv,channel 10 star tv ni ziwepo DSTV sio swala la TCRA hilo ni swala la kibiashara kati ya wamiliki wa vyombo hvi na DSTV ingekuwa itv ni tv ya taifa nayo unge iona DSTV,so kama mtu una taka itv DSTV nenda kaonge na mzee Mengi wafanye makubaliano na dstv wajuane watakatana shilling ngapi kujumlisha itv katika list zao.pia ikumbukwe DSTV ime pewa leseni ya kibiashara hawawezi tu amua kuweka channel za mfanya biashara mwingine kwa bure kwenye channel zao.swala la dollar nadhni ndilo la kulipigia kelele

Mkuu maelezo yako nimeyapata vizuri. Nadhani uneeleza Ukweli na hali halisi on the ground.

Kwa upande wa malipo makubwa yanayotozwa na multichoice pamoja na kwamba ni hiari kupata service Multichoice wanalo jukumu la kupunguza hii gharama lakini TCRA pia wana jukumu la kulinda haki za watumiaji kama wanavyofanya kwenye mitandao ya Simu.

Vile vile TCRA au serikali kupitia wizara husika wana jukumu la kuhakikisha ushindani wa haki kati ya makampuni yanayotoa huduma za tv kwa kuondoa vipengele vinavyoifanya Multichoice kuwa na monopoly Au exclusive right ya Chanel za kimataifa inazozirusha. Pamoja na ubora wa matangazo yao nadhani hili nalo linawafanya wawe na bei za kiburi.

Kwa upande wa Chanel za kitaifa (ingawa si chanel za taifa) nakubaliana na wewe kwamba ili kuingizwa DSTV itategemea sana negotiation ya makambuni husika na Multichoice. Lakini vile vile naamini itakuwa ni faida kwa Multichoice wakiingiza hizi Chanel Na kufanya bei yao iwe reasonable. Kwa kufanya hivi watanzania wengi wataweza kujiunga na watapata faida zaidi.
 
Mkuu ni kweli wameweka TBC lakini kwa nini na wao wasiweke vituo vingine vya kitaifa ambavyo tumekuwa tukivipata bure. Kampuni zingine za Star Time Na Zuku pamoja na kwamba nao wanafanya biashara kama ya Multichoice chini ya uangalizi mmoja wa TCRA wameweka hivi vituo Au wao wana masharti tofauti.

Bei za DSTV zimekuwa juu tangu ianzishwe miaka 15 iliyopita. Makampuni yote yanapokuwa wamepata wateja wengi hupunguza gharama lakini hawa jamaa wako kiuchumaji na wanacharge kwa dola kinyume na keseni yao ya biashara. Ukienda kulipia wanakupigia mahesabu ya dola!
Tena USD 1 kwa 1650
 
Ndugu wanabodi nashangazwa sana kwa msimamo wa kampuni ya Multichoice ambayo inatoa huduma ya kuonyesha chanel za TV za digitali nchini kwa kupitia DSTV.

Kampuni hii haijaonyesha nia au tuseme imekataa kuweka chanel za kitaifa za hapa nyumbani ambazo ndizo zinatupa habari za hapa nyumbani.

Nashangazwa sana na msimamo huu pamoja na ukimya wa serikali hasa kupitia TCRA na wizara husika ambao ndio wanapaswa kulinda maslahi ya wananchi wake.

Inavyoelekea baadhi ya viongozi wa serikali wana maslahi binafsi kwenye kampuni hii. Iweje kampuni zingine kama Star time na Zuku waweze kuingiza chanel zetu za kitaifa kama ITV na Star Tv kwenye bundle zao lakini DSTV wakatae? Hakuna mantiki yoyote ya kutoziingiza hizi chanel kwani ni chanel ambazo si za kulipia.

Hii ina maana watu tulio na DSTV baada ya tarehe 31 mwezi huu hatutaweza kuona chanel zetu labda kama utanunua king'amuzi kingine ambacho nacho uwe unakilipia. Na kama TV yako haiwezi kuchukua ving'amuzi viwili basi itakubidi ununue TV nyingine! Au uondoe deki nk

Pia ingawa hawa jamaa wanatoa huduma kibiashara lakini bei zao ni kubwa mno tofauti hata ukiwa huko kwao SA na hata huwezi ukalinganisha na watu wanavyotozwa huko ulaya au marekani ambako wao ndio wenye kipato kikubwa. Huduma za TV ni chanzo cha taarifa na elimu (information & education) kwa karne hii kama ilivyo simu za mkononi si anasa tena Bali ni huduma muhimu kwa wananchi.

Pamoja na kwamba hawa Multichoice wana miaka 15 wakitoa hii huduma ya DSTV na sasa hivi wana wateja wengi ambapo ingewezekana kupunguza bei kwa kiwango kikubwa lakini bei zao zimebaki kuwa za kiwizi. Sasa hivi wanatudanganya kwa kupunguza asilimia 10!

Pamoja na kwamba kujiunga na DSTV ni hiari kama ilivyo kujiunga na makampuni ya simu za mkononi hii haihalalishi wizi kwa mteja na kichwa ngumu kukataa kuingiza TV zetu za kitaifa za kitanzania na serikali yetu ikiwaangalia na kuendelea kutoza gharama ya wastani wa 120,000 kwa mwezi ambayo ni sawa na elfu 4 kwa siku!
Dawa ni kuwasusia ,lakini kwa waTZ tulivyo na akili ya samaki itakuwa vigumu,tungewasusia anagalau kwa mwezi mmoja tu ,nina hakika uwezekano wa kushusha bei ni mkubwa.kwa hali ilivyo hapa TZ kinachotakiwa ni kususia haya makampuni ndipo nasi watumiaji tutakuwa na sauti ,tukisema tuwasubiri akina Nkoma&Mungi na TCRA hakuna kitakachofanyika
 
Umenena Mkuu, tuwafanye Kama vodacom tuliwasusia na siku hizi wameshika adabu
 
Dstv kwakweli is the best ukilinganisha na ving'amuzi vingne tatizo ni bei na kwann wameweka viwango tofauti kwann TCRA wasiwawekee ngumu kwa kuwakatalia viwango vyao kwamba mtu ukilpia una uwezo wa kuona channel zote mona startimes,easy tv,zuku wote wanalipia kwa kiwango kimoja alfu kumi au chini yake na mteja anauwezo wa kuona channel zote,TCRA waaliangalie hili kwa makini huu ni uonevu au DSTV walilenga baadhi ya watu katika nchi hii ndo wawe na access ya kupata huduma yao,kwasasa ambapo tunaelekea mfumo wa digital walipaswa kuliangalia hili kila mtanzania ana haki katika hili
 
Ni kweli kabisa Mkuu, nadhani TCRA wana wajibu wa kuingilia kati kwa sababu wanawajibika kulinda na maslahi ya wateja ambao wengi ni watanzania.

Nashangaa kwa nini wao wa operate kwa masharti tofauti na kupewa haki miliki ya Chanel hata za kimataifa Kama CNN ms BBC.
 
Wakuu ni kweli kwamba Dstv ni expensive( ila ni kwa anayetaka na si lazima) ila hivi tatizo ni Dstv au mamlaka za nchi hii? Hapa bongo gharama za cmu ni kubwa sana na bado hayo makampun ya cmu yanachangia kiduchu kwenye pato la taifa, the same goes to sekta ya madini, bandari na takataka nyingine za kutosha.

Tujiulize,hivi ni kwa nini nchi zisizo na bandari(land locked countries kama Zambia,Rwanda,Uganda) na nyingine zinatumia bandari yetu kwa kiasi kikubwa kupitishia bidhaa zake (kama Zambia) zinakua na bei nafuu katika hizo bidhaa kuliko hapa zilikopitia?

Hivi tatizo ni Dstv au mamlaka zetu? Kama huko kwingine mnakosema (kama South Africa) kwamba Dstv ni affordable kuliko hapa then tatizo si Dstv ila ni mamlaka zetu.

Personally, Dstv wako poa sana hata customer servise yao ni bomba probably kuliko makampun mengi yaliyopo bongo na hii PVR decoder ni noma mazee, inaipa uhai TV!

...Mkuu, samahani kwa kuchepuka kidogo kutoka kwenye mada. Hebu tafadhali nifafanulie kidogo kuhusu hii PVR yao unayosema hapa...
 
Gharama za DSTV ziko juu ni kwa sababu viongozi wenu wana gawio apo so ni mwendo wa kukomoana tuu
Ipo siku watz tutajikomboa na DSTV mtakuja kuyakumbuka haya maneno yangu "you are completely not fair when it comes to pricing your packages"
Hao wanaowakingia kifua kutoza ivyo hawataishi milele na atakuja Farao asiyemjua musa mtajuta
SA Malawi kenya rates zao ziko chini kuliko Tz WHY?
Siku yaja mtakapo lia na kusaga meno wateja watakapoanza kuwakimbia
 
Anadai yeye ni waziri kijana na anasikiliza na anajali wananchi wake

Angeweza kama angekuwa nje wa mfumo wa kifisadi wa CCM.

Ni kweli tuna vijana wazuri kama kina January Makamba lakini wanaharibiwa na mfumo.
 
Gharama za DSTV ziko juu ni kwa sababu viongozi wenu wana gawio apo so ni mwendo wa kukomoana tuu
Ipo siku watz tutajikomboa na DSTV mtakuja kuyakumbuka haya maneno yangu "you are completely not fair when it comes to pricing your packages"
Hao wanaowakingia kifua kutoza ivyo hawataishi milele na atakuja Farao asiyemjua musa mtajuta
SA Malawi kenya rates zao ziko chini kuliko Tz WHY?
Siku yaja mtakapo lia na kusaga meno wateja watakapoanza kuwakimbia

Kweli Mkuu hawa jamaa wana kiburi sana hapa Tanzania. Na ni kweli kama unavyothibitisha hapa mamlaka zetu zimewekwa Mfukoni na hawa jamaa.

Tangu DSTV wameingia nchini miaka 15 iliyopita hawajawahi kupunguza bei zao kiasi cha kueleweka. Sasa hivi wanadanganyia na punguzo la 10% tena mpaka uwahi kulipia kabla ya muda.

Hawa dawa yao ni kuwagomea, Vinginevyo nao wataonja joto ya jiwe pale fastjet ya TV itakapoingia.
 
Naomba kujua bei za packages za DSTV za family, Compact na Compact Plus
 
Naomba kujua bei za packages za DSTV za family, Compact na Compact Plus

Dstv Access sh. 16,100*
Family sh. 32,200
Compact sh. 48,300
Compact plus sh. 80,500
Premium sh. 128,800 kwa mwezi
*Viwango kulinganisha na bei ya kubadiri dola za Marekani!
 
Hawa jamaa kuna kipindi nilikuwa nawalipa kwa 6month unapigwa kitu kile kile hamna punguzo biashara za kizamani sana izi ata sijui kama wana watu competent wa market and sales?
Ni kunzisha kampeni ya nchi nzima kuwademarket hawa jamaa bse hawana ata haya then tuone hao akina mpungwe na ben waje watetee
 
Ndio kabisa Mkuu, huu ni Wizi Mkubwa kwa wananchi.

Nashangaa wengine tena wanajiita great thinkers halafu wanatetea huu upuuzi kwa kudai ni biashara huria.

Mbona kuna biashara nyingi huria serikali inaingilia biashara ikigeuka kuwa ya wizi; mfano bei za mabasi.

Inaelekea DSTV Tanzania ni mradi Wa vigogo serikalini.

Inabidi tuungane wote tuwakatae.
 
Dstv Access sh. 16,100*
Family sh. 32,200
Compact sh. 48,300
Compact plus sh. 80,500
Premium sh. 128,800 kwa mwezi
*Viwango kulinganisha na bei ya kubadiri dola za Marekani!

Umefafanua vizuri.

kwa sababu bei zao za ki Wizi hawaziweki hata kwenye website yao!

Na hizo zinaoonekana bei nafuu kidogo access Na family ni Chanel ambazo hazistahili hata kulipiwa
 
DSTV wahusika sana, imagine now nipo kwenye TV yangu naangalia Kombe la klabu bingwa duniani. Isingekuwepo ningeangalia wapi? Hayo ya cost nayawaza baadaye sana, cha muhimu nipate service ya uhakika na kwa wakati ninaoihitaji.
 
Back
Top Bottom