Serikali imeungana na Dunia ya Kwanza kuwakandamiza Masikini. Acha wakandamizwe tu

Autocratic leadership has positive impact or negative this will depend on how brave the leader is
That is problem. All, rapid progress they have been achieved under such leadership.

Queen Victoria was there for almost lifetime. It is in her period Great Britain became foremost, superpower in the world.
 
Ni kati ya watu wachache Tanzania wenye akili timamu. Nchi zote Ulaya zilitumia ukatili mkubwa kupata maendeleo, utumwa, ukoloni hadi sasa ukoloni mamboleo.

Kwa zaidi ya miaka 500 ziliongozwa kiditekta. Madikteta wenye dhamira nzuri, kusaidia nchi zao watu wao. Uarabuni, China, Japan, Korea wote walikuwa ni madikteta ila wameendeleza nchi zao.

Ni lazima ufikie level flani, kielimu, kiuchumi, kujitambua kupewa hii Western Democracy. Mtoto wako haumpi democracy mpaka afikie level flani ya kujitambua.

Nchi inaruhusu kila kitu kisa Wazungu wamesema na nchi ya ajabu sana.
Kuna jambo inabidi ujielimishe kidogo Ili upanue uwezo wako hasa wa kuchambua hicho unachoita "history of development". Jambo lenyewe ni ZAMA. Maendeleo katika jamii hutokana na uwezo wa nchi husika kutumia rasilimali zake kulingana na fikra, teknolojia na muundo wa kidunia wa wakati huo (ZAMA). Kuamini kwamba kwa kuwa ulaya na Marekani iliendelea bila kutumia demokrasia hii ya leo, kwanza sio kweli lakini pili ni ujuha. Yes, jukumu la kujiletea maendeleo ni letu wenyewe wala si la mshirika wa maendeleo au wafadhili lakini ni lazima tulitimize kwa kutumia Zama za leo si vinginevyo. Kuna mambo yalifanywa kwa UJUHA kutokana na ufinyu wa Elimu na taarifa kwa nyakati hizo. Kuna ZAMA zilipita mwanamke hakuwa na nafasi ya kurithi au kumiliki mali, kuna ZAMA zilipita wafanyakazi wa viwanda vya nguo kule Marekani walikuwa mabinti wadogo wa miaka 15-20. Lakini huwezi kuchukua historia hiyo ukaitekeleza leo kwasababu ufahamu na Elimu imepanuka na jamii kuweka demarcation na kubainisha haki za mtoto. ZAMA. ZAMA hizi si zama za kuficha watoto wa kike ndani, si zama za kuweka wari ndani Ili wasubiri kuolewa, si zama za kutumikisha wanawake shambani na mume kunywa mbege au ulanzi.

Infact, tuna mambo mengi tu ya kujifunza (kama sio kuiga) kutoka kwa hao tunaowaona hawana msaada kwenye maendeleo yetu. Kwa mfano, umewahi kujiuliza how comes shule zilizojengwa na mkoloni miaka ya 1920-1960 zilikuwa bora (comprehensively) kuliko shule zinazojengwa miaka 60 baadaye? Hapa anazungumzia shule kama Mzumbe, Tabora, Tanga Tech, Ifunda, Iyunga, Tambaza (HH Aga Khan Boys) nk nk. Hizi shule ni mfano mzuri wa kuacha kuiga wazungu. Je zimetusaidia? Unadhani Elimu yetu ingekuwa vipi leo kama shule zote hizi zilizojengwa miaka ya hivi karibuni zingejengwa kwa mfano wa shule za wakoloni?

Mfano mwingine ni katika viwanda. Hatuhitaji kupita hatua walizopita wazungu katika kujiletea maendeleo maana wao walifanya invention na innovation kwa pamoja. Lakini sisi hatuhitaji kupita huko, tunahitaji innovation tu. Same in democratic process, we may no longer need to go through democratic process kama walivyopita wao wakati wa maendeleo kwasababu ZAMA haziruhusu kwa kuwa innovation process has taken place.

Hivyo kuamini kuwa Dictatorship au Autocratic wana nafasi kubwa ya kufanya kama miaka 200-500 iliyopita ni kujidanganya na huenda isiwe msaada kwetu.
 
Ukitaka mikopo na misaada ya Wazungu lazima ufuate masharti yao. Na kati ya masharti yao ni kufuata mfumo wa demokrasia, kulinda haki za binadamu. Kama wewe hutaki hayo masharti achana na hela zao. Wewe unategemea kodi ya shoga aliyeko Marekani au Ulaya ije hapa itumike kuwakandamiza mashoga wa hapa Tanzania?
 
Usiropoke, kaa chini tulia, jiulize Democracy (Haki ya wengi) ni nini?

Umeme, maji, chakula, makazi, afya, elimu,ajira, biashara, usalama, rasilimali za nchi zitumike vipi ni Democracy.

Unafikiri ni haki tu ya kupiga kelele, kupinga kila kitu, kutukana?
Lengo lako la kupalilia udikteta ili unufaike nao halitafanikiwa zaidi tutakung'oa meno,,,kupiga kelele na kupinga ndio dawa sahihi ya viongozi walafi wa Afrika
 
SERIKALI IMEUNGANA NA DUNIA YA KWANZA KUWAKANDAMIZA MASIKINI. NAMI NASEMA WAMALIZENI KABISA.

Na, Robert Heriel.

Kusoma wakati mwingine sio kuelimika, ninaushahidi wa kutosha usiotia Shaka kuwa wasomi wanashindwa na mambo mengi zaidi ya Wale wasiosoma.
Sio kwenye ndoa, sio kwenye kazi, sio kwenye uongozi.
Unajua ni kwanini?
Kwa sababu wasomi wengi wamesomea upumbavu Kama sio ujinga.
Ni Kwa sababu wasomi wamefundishwa kuwa Uniform, kufanana, kuwa kama Fulani (hasa kuwa kama Wazungu) ni nadra elimu ya wasomi wengi Kwa jamii zetu zikamfundisha mtu kuwa mbunifu zaidi ya kukariri mambo.

Ndio maana wasomi wengi na Wale wanaojiona hivyo na wenye kutumainiwa kwenye taifa hili, wasomi mashuhuri, iwe maarufu kwenye mitandao wengi hujionea fahari kujiona wasomi Kwa kukariri na kujisarehesha na Wazungu.
Wengi huwa na mtazamo kuwa Uzungu ndio usomi na hapo ndipo upumbavu wao unapodhihirika.

Wazungu wanafahamu wazi kuwa elimu waliyotupa ni mtego wao muhimu na wapekee kutufanya tuwe watu wasioweza kufikiri vizuri, tuwe watu wa bendera fuata UPEPO.

Yaani Mzungu akifanya nawe unaiga kunya Kwa Tembo.
Wasomi wengi ni waiga kunya Kwa Tembo. Siwalaumu Kwa sababu ndio wameshaathirika kisaikolojia.

Afrika haiwezi kuendelea Kwa sababu maendeleo yake niya bendera fuata UPEPO, kuiga Kwa Tembo.

Ni nadra Sana umkute msomi asiyeiga kunya Kwa Tembo, nadra Sana.

Mzungu akisema Uzazi wa mpango, bendera fuata UPEPO nao HAO.
Mzungu akisema haki Sawa, bendera fuata UPEPO hao.
Mzungu akisema Demokrasia, waiga kunya Kwa Bata HAO.
Mzungu akisema haki za wapenzi WA jinsia moja, wasomi uchwara nao HAO.
Mzungu akisema waliopewa mimba waendele na Shule, wenzangu na miye HAO wanarukia makida.

Huwezi iga watu ambao mpo tofauti nao Kwa karibu kila kitu.

Huwezi leta Demokrasia kwenye jamii ya watu masikini na wajinga Kama nchi za Afrika huko ni kuikandamiza Afrika na Nchi yako.

Hivi masikini tangu lini akawa na demokrasia?
Tangu lini masikini na mjinga akapewa demokrasia nauliza.

Demokrasia ya Wazungu ilikuja baada ya maendeleo kukua, baada ya watu kupata elimu.

Unaletaje Haki Sawa baina ya mwanamke na Mwanaume kwenye jamii ya watu masikini na wajinga. Ajabu Sana hii.
Haki Sawa inawafaa watu walioendelea kiasi na walioikimbia UMASIKINI.

Kwenye umasikini lazima mfumo mmoja utumike IMA ni mfumo jike au mfumo Dume.

Sasa unaruhusu wanawake wafanye kazi Kama wanaume alafu muda huo huo sheria hubadili unaacha Kama zilivyokuwa; mwanaume ndiye anawajibu WA kumtunza mwanamke! Hivi hiyo ni Akili kweli ndugu zangu.
Hivi hamuoni kuwa Kama mwanamke kwenye jamii masikini akipewa nafasi ya za kuajiriwa automatically tatizo la Ajira litajitokeza,

Hamfikirii kuwa Kuruhusu wanawake wafanye kazi automatically ni kuangusha taasisi ya ndoa. Hamuoni kuwa Vijana watachelewa kuoa kwani Ajira zitakuwa hakuna?

Wasomi lazima tuelewe kuwa, huwezi taka nchi yako masikini ifanane kimifumo na Nchi zilizoendelea.
Nchi zilizoendelea zinazouwezo wa kufanya hivyo Kwa sababu zimeshaendelea, kwenye maendeleo ndio kuna haki Sawa. Hata wanawake wakiajiriwa ni Sawa Kwa sababu serikali inajua wapi itapata pesa iwe Kwa kudhulumu na kunyonya nchi masikini au kuzitawala kabisa.

Sasa kanchi Kako hata uwezo wa kuvamia taifa jingine ili waibe Mali hakana unataka kuiga mambo ya nchi kubwa. Wasomi tuweni Sirius tunaongoza Nchi.

Kama serikali na wasomi ingekuwa inawapenda watoto wakike, ingeweka mipango na mikakati wasijiingize kwenye ngono zembe mapema, wangezuia watoto wasifanye zinaa ili wasipate matokeo ya zinaa ambayo huweza kuwa chanya au Hasi.

Wazungu sio kwamba wanaakili kutuzidi Waafrika isipokuwa viongozi na wasomi wa Afrika wengi wao ni bendera fuata UPEPO.

Msomi na serikali lazima tujiulize kuwa Mzungu na mataifa makubwa yanapotuamrisha Jambo Fulani, labda ni Uzazi wa mpango, au ushoga, ya Kuruhusu waliopewa mimba kuendelea na masomo, tujiulize mataifa hayo kipindi yakiwa na uchumi Kama wetu yaliruhusu mambo hayo?
Au ndio wametuhusu sasa hivi Kwa sababu washaelimisha jamii zao zikaelimika kiasi kwamba wanajua kabisa jamii zao mpaka watoto wanauelewa na elimu ya Uzazi wa mpango,

Wasomi na serikali lazima tujue kulinganisha na kutofautisha.

Lazima tujiulize, wakati Uingereza au USA ikiwa na Hali Kama yetu, ikiwa na miaka 60 tangu ipate Uhuru iliruhusu mambo ambayo inataka tuyafanye?

Sio wenzanu wamefikia level ya Kula mifupa na ninyi mpo level ya kunyonya maziwa na kunywa uji alafu wanawashinikiza mle mifupa wakati hamna Meno. Tuweni Makini Sana.

Jamii yoyote changa inahitaji sheria Kali zisizo na huruma.
Jamii na taifa likiwa masikini na ujinga mwingi linahitaji sheria Kali zisizo na huruma, huku elimu ikiendelea kutolewa.

Jamii ikishaendelea kiuchumi na kielimu ndio unaanza Kupunguza ukali wa SHERIA. Unatoa demokrasia, ndio mambo yanavyoenda hivyo.

Ustaarabu haumfai mtu mjinga na masikini Hilo kila siku ninasema na nitasema.

Serikali ninaiomba iache kuungana na Dunia ya Kwanza kuikandamiza jamii yake.

Wazungu wanatabia ya kujifanya wanakusaidia kumbe Kwa nyuma yake wanaagenda ya Siri kabisa ambayo huko mbeleni huwa mtego Kwetu.

Tangu zamani Wazungu walitumia serikali,
Dini, mashirika binafsi, watu mashuhuri, Elimu, misaada n.k kutawala Afrika.

Serikali ingejikita zaidi kuweka sheria Kali, wala isijali hawa wasomi fuata UPEPO wa Wazungu Kama bendera.

Nipumzike sasa.

Ni Yule Shahidi kutoka Nyota ya Tibeli.

Robert Heriel
Taikon wa Fasihi
Kwa sasa, KARIAKOO, DAR ES SALAAM
Acha uongo kuamua kuelimika na mpango wa Mtu mwenyewe. Hiyo njia ya kukariri ndio wachina wanaitumia kuchukua teknolojia za wengine vipi wanavyo piga hatua kimaendeleo. Ukitaka kuelimika unaanza mwenyewe hata ulaya pia kuna wajinga.
 
Ukitaka mikopo na misaada ya Wazungu lazima ufuate masharti yao. Na kati ya masharti yao ni kufuata mfumo wa demokrasia, kulinda haki za binadamu. Kama wewe hutaki hayo masharti achana na hela zao. Wewe unategemea kodi ya shoga aliyeko Marekani au Ulaya ije hapa itumike kuwakandamiza mashoga wa hapa Tanzania?

Waarabu wanafata masharti hayo. They do participate in world economic system.
 
Kuna jambo inabidi ujielimishe kidogo Ili upanue uwezo wako hasa wa kuchambua hicho unachoita "history of development". Jambo lenyewe ni ZAMA. Maendeleo katika jamii hutokana na uwezo wa nchi husika kutumia rasilimali zake kulingana na fikra, teknolojia na muundo wa kidunia wa wakati huo (ZAMA). Kuamini kwamba kwa kuwa ulaya na Marekani iliendelea bila kutumia demokrasia hii ya leo, kwanza sio kweli lakini pili ni ujuha. Yes, jukumu la kujiletea maendeleo ni letu wenyewe wala si la mshirika wa maendeleo au wafadhili lakini ni lazima tulitimize kwa kutumia Zama za leo si vinginevyo. Kuna mambo yalifanywa kwa UJUHA kutokana na ufinyu wa Elimu na taarifa kwa nyakati hizo. Kuna ZAMA zilipita mwanamke hakuwa na nafasi ya kurithi au kumiliki mali, kuna ZAMA zilipita wafanyakazi wa viwanda vya nguo kule Marekani walikuwa mabinti wadogo wa miaka 15-20. Lakini huwezi kuchukua historia hiyo ukaitekeleza leo kwasababu ufahamu na Elimu imepanuka na jamii kuweka demarcation na kubainisha haki za mtoto. ZAMA. ZAMA hizi si zama za kuficha watoto wa kike ndani, si zama za kuweka wari ndani Ili wasubiri kuolewa, si zama za kutumikisha wanawake shambani na mume kunywa mbege au ulanzi.

Infact, tuna mambo mengi tu ya kujifunza (kama sio kuiga) kutoka kwa hao tunaowaona hawana msaada kwenye maendeleo yetu. Kwa mfano, umewahi kujiuliza how comes shule zilizojengwa na mkoloni miaka ya 1920-1960 zilikuwa bora (comprehensively) kuliko shule zinazojengwa miaka 60 baadaye? Hapa anazungumzia shule kama Mzumbe, Tabora, Tanga Tech, Ifunda, Iyunga, Tambaza (HH Aga Khan Boys) nk nk. Hizi shule ni mfano mzuri wa kuacha kuiga wazungu. Je zimetusaidia? Unadhani Elimu yetu ingekuwa vipi leo kama shule zote hizi zilizojengwa miaka ya hivi karibuni zingejengwa kwa mfano wa shule za wakoloni?

Mfano mwingine ni katika viwanda. Hatuhitaji kupita hatua walizopita wazungu katika kujiletea maendeleo maana wao walifanya invention na innovation kwa pamoja. Lakini sisi hatuhitaji kupita huko, tunahitaji innovation tu. Same in democratic process, we may no longer need to go through democratic process kama walivyopita wao wakati wa maendeleo kwasababu ZAMA haziruhusu kwa kuwa innovation process has taken place.

Hivyo kuamini kuwa Dictatorship au Autocratic wana nafasi kubwa ya kufanya kama miaka 200-500 iliyopita ni kujidanganya na huenda isiwe msaada kwetu.

Mpuuzi wewe, huna hoja. Mtukanaji.
 
Unafikiri wanasayansi, technology ya kupata gas, oil, usafirishaji, uwekezaji, uendeshaji hio sekta imetoka wapi?
Watu binafsi na makampuni binafsi wana uhuru wa kufanya wanachotaka ili mradi hawavunji sheria za nchi zao. Naongelea misaada na mikopo inayotokea kwa serikali za Marekani na Ulaya. Zina masharti kwa kuwa ni kodi za watu.
 
Naunga mkono hoja...bora kuwa na dikteta mwenye akili kuliko demokrasia ......hebu imagine miaka 42 ya uongozi wa Gadafi libya imezaa matunda gani halafu linganisha na miaka 60 ya demokrasia imetufikisha wapi..
 
Madikiteta nafasi yenu Duniani ni finyu sana. Inazidi kuwa finyu zaidi.
Nakuonea huruma kwa kuwaona watu wanaotumia nguvu kulinda wananchi na mali zao kuwa madikteta
Je USA na NATO yao China Urusi ujerumani nazitumii nguvu kwa demokrasia na ukomunisti kutuhadaa
Waafrika na kujaribu kutawala ulimwengu

Basi nakwambia subiri ndo kwanza tunaanza uzi makini sana umesisimua hamu yangu ya black panther
 
Kapewa pesa za kuja kuwachumbia akina mama eti wampende kwa kuwaambia ni mikopo iso na riba. Swali ni, kwanini mkopo utakaokuja kulipwa na raia wote wa nchi pasipo kujali jinsia eti leo wanaoruhusiwa kuifurahia pesa hiyo wawe wa jinsia moja tu,; tuelewe hata hilo deni ktk mikopo ya nchi italipwa na kodi zinazotokana na wanawake tu?

Huyu mkuu wa waganga ni mbaguzi sana na kuhani wa mtandao wa Extremist hapa duniani. Tz haijawahi kuwa dola la kidini wala la kiitikadi, haya mambo yanapendwa sana huko kwao na wako hivyo na ndio maana waliingiza nchi yao OIC. Hawa watu ni extrimists wa kutupwa na sasa anapromote radical feminism
 
Korea kaskazini ni nchi wanayoishi maisha yao pekee yao na kwa namba yao hawafanyi uchaguzi unaogawanya watu na kupoteza kodi kwenye kampeni wala mda hawacheki na wala rushwa ukila rushwa na kutapeli mali ya umma utaonja adhabu ya kifo hawaigi utamaduni wa nchi nyingine yeyote hawatumii mitandao ya kijamii inayozembesha watu hawana dini inayowagawanya hakuna tv inayorusha matangazo mchana mda wa KAZI hawavai modo kukumbatiana au kubusiana hadharani.

Leo taifa lao lina lina ubavu wa kusimama na kukutunishiana misuli na Marekani

Nambie hakuna BBC, CNN, DW wala UN wala mtandao wowote wa kijamii nchi ina channel tatu tu 2 zinaonesha weekend tu hizo chokochoko za kutibua nchi zinaiingilia wapi?

Ukiwaambia waswahili haya wataona kama unataka kuwapeleka Utumwani,, wamesahau already wapo kwenye Utumwa.

Kuendana na kasi ya Dunia hatuna huo uwezo., tunazidi kupoteza vizazi creative na tuna depend kwa wao.
 
Back
Top Bottom