Serikali imeungana na Dunia ya Kwanza kuwakandamiza Masikini. Acha wakandamizwe tu

Robert Heriel Mtibeli

JF-Expert Member
Mar 24, 2018
21,340
51,891
SERIKALI IMEUNGANA NA DUNIA YA KWANZA KUWAKANDAMIZA MASIKINI. NAMI NASEMA WAMALIZENI KABISA

Na, Robert Heriel

Kusoma wakati mwingine sio kuelimika, ninaushahidi wa kutosha usiotia Shaka kuwa wasomi wanashindwa na mambo mengi zaidi ya Wale wasiosoma.

Sio kwenye ndoa, sio kwenye kazi, sio kwenye uongozi.

Unajua ni kwanini?

Kwa sababu wasomi wengi wamesomea upumbavu kama sio ujinga.

Ni Kwa sababu wasomi wamefundishwa kuwa Uniform, kufanana, kuwa kama Fulani (hasa kuwa kama Wazungu) ni nadra elimu ya wasomi wengi Kwa jamii zetu zikamfundisha mtu kuwa mbunifu zaidi ya kukariri mambo.

Ndio maana wasomi wengi na Wale wanaojiona hivyo na wenye kutumainiwa kwenye taifa hili, wasomi mashuhuri, iwe maarufu kwenye mitandao wengi hujionea fahari kujiona wasomi Kwa kukariri na kujisarehesha na Wazungu.

Wengi huwa na mtazamo kuwa Uzungu ndio usomi na hapo ndipo upumbavu wao unapodhihirika.

Wazungu wanafahamu wazi kuwa elimu waliyotupa ni mtego wao muhimu na wapekee kutufanya tuwe watu wasioweza kufikiri vizuri, tuwe watu wa bendera fuata UPEPO.

Yaani Mzungu akifanya nawe unaiga kunya Kwa Tembo.

Wasomi wengi ni waiga kunya Kwa Tembo. Siwalaumu Kwa sababu ndio wameshaathirika kisaikolojia.

Afrika haiwezi kuendelea Kwa sababu maendeleo yake niya bendera fuata UPEPO, kuiga Kwa Tembo.

Ni nadra Sana umkute msomi asiyeiga kunya Kwa Tembo, nadra Sana.

Mzungu akisema Uzazi wa mpango, bendera fuata UPEPO nao HAO.
Mzungu akisema haki Sawa, bendera fuata UPEPO hao.
Mzungu akisema Demokrasia, waiga kunya Kwa Bata HAO.
Mzungu akisema haki za wapenzi WA jinsia moja, wasomi uchwara nao HAO.
Mzungu akisema waliopewa mimba waendele na Shule, wenzangu na miye HAO wanarukia makida.

Huwezi iga watu ambao mpo tofauti nao Kwa karibu kila kitu.

Huwezi leta Demokrasia kwenye jamii ya watu masikini na wajinga Kama nchi za Afrika huko ni kuikandamiza Afrika na Nchi yako.

Hivi masikini tangu lini akawa na demokrasia?

Tangu lini masikini na mjinga akapewa demokrasia nauliza.

Demokrasia ya Wazungu ilikuja baada ya maendeleo kukua, baada ya watu kupata elimu.

Unaletaje Haki Sawa baina ya mwanamke na Mwanaume kwenye jamii ya watu masikini na wajinga. Ajabu Sana hii.

Haki Sawa inawafaa watu walioendelea kiasi na walioikimbia UMASIKINI.

Kwenye umasikini lazima mfumo mmoja utumike IMA ni mfumo jike au mfumo Dume.

Sasa unaruhusu wanawake wafanye kazi Kama wanaume alafu muda huo huo sheria hubadili unaacha Kama zilivyokuwa; mwanaume ndiye anawajibu WA kumtunza mwanamke! Hivi hiyo ni Akili kweli ndugu zangu.

Hivi hamuoni kuwa Kama mwanamke kwenye jamii masikini akipewa nafasi ya za kuajiriwa automatically tatizo la Ajira litajitokeza,

Hamfikirii kuwa Kuruhusu wanawake wafanye kazi automatically ni kuangusha taasisi ya ndoa. Hamuoni kuwa Vijana watachelewa kuoa kwani Ajira zitakuwa hakuna?

Wasomi lazima tuelewe kuwa, huwezi taka nchi yako masikini ifanane kimifumo na Nchi zilizoendelea.

Nchi zilizoendelea zinazouwezo wa kufanya hivyo Kwa sababu zimeshaendelea, kwenye maendeleo ndio kuna haki Sawa. Hata wanawake wakiajiriwa ni Sawa Kwa sababu serikali inajua wapi itapata pesa iwe Kwa kudhulumu na kunyonya nchi masikini au kuzitawala kabisa.

Sasa kanchi Kako hata uwezo wa kuvamia taifa jingine ili waibe Mali hakana unataka kuiga mambo ya nchi kubwa. Wasomi tuweni Sirius tunaongoza Nchi.

Kama serikali na wasomi ingekuwa inawapenda watoto wakike, ingeweka mipango na mikakati wasijiingize kwenye ngono zembe mapema, wangezuia watoto wasifanye zinaa ili wasipate matokeo ya zinaa ambayo huweza kuwa chanya au Hasi.

Wazungu sio kwamba wanaakili kutuzidi Waafrika isipokuwa viongozi na wasomi wa Afrika wengi wao ni bendera fuata UPEPO.

Msomi na serikali lazima tujiulize kuwa Mzungu na mataifa makubwa yanapotuamrisha Jambo Fulani, labda ni Uzazi wa mpango, au ushoga, ya Kuruhusu waliopewa mimba kuendelea na masomo, tujiulize mataifa hayo kipindi yakiwa na uchumi Kama wetu yaliruhusu mambo hayo?

Au ndio wametuhusu sasa hivi Kwa sababu washaelimisha jamii zao zikaelimika kiasi kwamba wanajua kabisa jamii zao mpaka watoto wanauelewa na elimu ya Uzazi wa mpango,

Wasomi na serikali lazima tujue kulinganisha na kutofautisha.

Lazima tujiulize, wakati Uingereza au USA ikiwa na Hali Kama yetu, ikiwa na miaka 60 tangu ipate Uhuru iliruhusu mambo ambayo inataka tuyafanye?

Sio wenzanu wamefikia level ya Kula mifupa na ninyi mpo level ya kunyonya maziwa na kunywa uji alafu wanawashinikiza mle mifupa wakati hamna Meno. Tuweni Makini Sana.

Jamii yoyote changa inahitaji sheria Kali zisizo na huruma.
Jamii na taifa likiwa masikini na ujinga mwingi linahitaji sheria Kali zisizo na huruma, huku elimu ikiendelea kutolewa.

Jamii ikishaendelea kiuchumi na kielimu ndio unaanza Kupunguza ukali wa SHERIA. Unatoa demokrasia, ndio mambo yanavyoenda hivyo.

Ustaarabu haumfai mtu mjinga na masikini Hilo kila siku ninasema na nitasema.

Serikali ninaiomba iache kuungana na Dunia ya kwanza kuikandamiza jamii yake.

Wazungu wanatabia ya kujifanya wanakusaidia kumbe Kwa nyuma yake wanaagenda ya Siri kabisa ambayo huko mbeleni huwa mtego Kwetu.

Tangu zamani Wazungu walitumia serikali

Dini, mashirika binafsi, watu mashuhuri, Elimu, misaada n.k kutawala Afrika.

Serikali ingejikita zaidi kuweka sheria kali, wala isijali hawa wasomi fuata UPEPO wa Wazungu Kama bendera.

Nipumzike sasa.

Ni Yule Shahidi kutoka Nyota ya Tibeli.

Robert Heriel
Taikon wa Fasihi
Kwa sasa, KARIAKOO, DAR ES SALAAM
 
Alivyokuwa mama katika usichana wake ndivyo atakavyo kuwa binti yake chini ya malezi ya mama yake. Hakuna jipya chini ya jua.
 
Magufuli alikosea kipengele kimoja tuu na huko nilimpinga lakini kwingine kote alifanya vizuri.

Miaka mitatu ya Mwanzo JPM ndio alikosea lakini baada ya hapo alifanya marekibisho makubwa sana
Yap man hujakosea nchi ya watu wenye akili haifundishwi namna ya kuendelea mfano nzuri korea kaskazini
 
Huu ndio ukweli. Nchi karibu zote Ulaya zilitumia ukatili mkubwa kupata maendeleo, utumwa, ukoloni hadi sasa ukoloni mamboleo.

Kwa zaidi ya miaka 500 nchi nying zilizoendelea sasa ziliongozwa kiditekta. Madikteta wenye dhamira nzuri, kusaidia nchi zao watu wao. Uarabuni, China, Japan, Korea wote walikuwa ni madikteta ila wameendeleza nchi zao.

Ni lazima ufikie level flani, kielimu, kiuchumi, kujitambua kupewa hii Western Democracy. Mtoto wako haumpi democracy mpaka afikie level flani ya kujitambua.

Nchi inaruhusu kila kitu kisa Wazungu wamesema na nchi ya ajabu sana.
 
Vipi jamaa hawakufikiria demokrasia ya watumwa, ukoloni, mifumo kandamizi ya dunia ya sasa.
Korea kaskazini ni nchi wanayoishi maisha yao pekee yao na kwa namba yao hawafanyi uchaguzi unaogawanya watu na kupoteza kodi kwenye kampeni wala mda hawacheki na wala rushwa ukila rushwa na kutapeli mali ya umma utaonja adhabu ya kifo hawaigi utamaduni wa nchi nyingine yeyote hawatumii mitandao ya kijamii inayozembesha watu hawana dini inayowagawanya hakuna tv inayorusha matangazo mchana mda wa KAZI hawavai modo kukumbatiana au kubusiana hadharani.

Leo taifa lao lina lina ubavu wa kusimama na kukutunishiana misuli na Marekani

Nambie hakuna BBC, CNN, DW wala UN wala mtandao wowote wa kijamii nchi ina channel tatu tu 2 zinaonesha weekend tu hizo chokochoko za kutibua nchi zinaiingilia wapi?
 
Korea kaskazini ni nchi wanayoishi maisha yao pekee yao na kwa namba yao hawafanyi uchaguzi unaogawanya watu na kupoteza kodi kwenye kampeni wala mda hawacheki na wala rushwa ukila rushwa na kutapeli mali ya umma utaonja adhabu ya kifo hawaigi utamaduni wa nchi nyingine yeyote hawatumii mitandao ya kijamii inayozembesha watu hawana dini inayowagawanya hakuna tv inayorusha matangazo mchana mda wa KAZI hawavai modo kukumbatiana au kubusiana hadharani

Leo taifa lao lina lina ubavu wa kusimama na kukutunishiana misuli na marekani

Nambie hakuna bbc cnn dw wala un wala mtandao wowote wa kijamii nchi ina channel tatu tu 2 zinaonesha weekend tu hizo chokochoko za kutibua nchi zinaiingilia wapi?

Hatuna haja ya kujitenga, hatuwezi kujitenga.

Sisi ni sehemu muhimu sana Afrika yote, duniani. Muhimu tuwe na vigezo vya kulinda maadili yetu, utamaduni wetu, mila na desturi zetu, sheria zetu wakati huohuo tunawakaribisha wageni wote, wawekezaji wote kwa vigezo, masharti yetu.
 
Ni kati ya watu wachache Tanzania wenye akili timamu. Nchi zote Ulaya zilitumia ukatili mkubwa kupata maendeleo, utumwa, ukoloni hadi sasa ukoloni mamboleo.

Kwa zaidi ya miaka 500 ziliongozwa kiditekta. Madikteta wenye dhamira nzuri, kusaidia nchi zao watu wao. Uarabuni, China, Japan, Korea wote walikuwa ni madikteta ila wameendeleza nchi zao.

Ni lazima ufikie level flani, kielimu, kiuchumi, kujitambua kupewa hii Western Democracy. Mtoto wako haumpi democracy mpaka afikie level flani ya kujitambua.

Nchi inaruhusu kila kitu kisa Wazungu wamesema na nchi ya ajabu sana.
Wewe utakuwa ni Msukuma, yaani unataka uishi kama mtumwa, aisee kuna msemo unasema wakati wa utumwa kuna watumwa walikataa kuachiwa huru. Nadhani hata wew ungekataa.
 
Korea kaskazini ni nchi wanayoishi maisha yao pekee yao na kwa namba yao hawafanyi uchaguzi unaogawanya watu na kupoteza kodi kwenye kampeni wala mda hawacheki na wala rushwa ukila rushwa na kutapeli mali ya umma utaonja adhabu ya kifo hawaigi utamaduni wa nchi nyingine yeyote hawatumii mitandao ya kijamii inayozembesha watu hawana dini inayowagawanya hakuna tv inayorusha matangazo mchana mda wa KAZI hawavai modo kukumbatiana au kubusiana hadharani

Leo taifa lao lina lina ubavu wa kusimama na kukutunishiana misuli na marekani

Nambie hakuna bbc cnn dw wala un wala mtandao wowote wa kijamii nchi ina channel tatu tu 2 zinaonesha weekend tu hizo chokochoko za kutibua nchi zinaiingilia wapi?
Kwanini usihamie huko sasa?
 
SERIKALI IMEUNGANA NA DUNIA YA KWANZA KUWAKANDAMIZA MASIKINI. NAMI NASEMA WAMALIZENI KABISA.

Na, Robert Heriel.

Kusoma wakati mwingine sio kuelimika, ninaushahidi wa kutosha usiotia Shaka kuwa wasomi wanashindwa na mambo mengi zaidi ya Wale wasiosoma.
Sio kwenye ndoa, sio kwenye kazi, sio kwenye uongozi.
Unajua ni kwanini?
Kwa sababu wasomi wengi wamesomea upumbavu Kama sio ujinga.
Ni Kwa sababu wasomi wamefundishwa kuwa Uniform, kufanana, kuwa kama Fulani (hasa kuwa kama Wazungu) ni nadra elimu ya wasomi wengi Kwa jamii zetu zikamfundisha mtu kuwa mbunifu zaidi ya kukariri mambo.

Ndio maana wasomi wengi na Wale wanaojiona hivyo na wenye kutumainiwa kwenye taifa hili, wasomi mashuhuri, iwe maarufu kwenye mitandao wengi hujionea fahari kujiona wasomi Kwa kukariri na kujisarehesha na Wazungu.
Wengi huwa na mtazamo kuwa Uzungu ndio usomi na hapo ndipo upumbavu wao unapodhihirika.

Wazungu wanafahamu wazi kuwa elimu waliyotupa ni mtego wao muhimu na wapekee kutufanya tuwe watu wasioweza kufikiri vizuri, tuwe watu wa bendera fuata UPEPO.

Yaani Mzungu akifanya nawe unaiga kunya Kwa Tembo.
Wasomi wengi ni waiga kunya Kwa Tembo. Siwalaumu Kwa sababu ndio wameshaathirika kisaikolojia.

Afrika haiwezi kuendelea Kwa sababu maendeleo yake niya bendera fuata UPEPO, kuiga Kwa Tembo.

Ni nadra Sana umkute msomi asiyeiga kunya Kwa Tembo, nadra Sana.

Mzungu akisema Uzazi wa mpango, bendera fuata UPEPO nao HAO.
Mzungu akisema haki Sawa, bendera fuata UPEPO hao.
Mzungu akisema Demokrasia, waiga kunya Kwa Bata HAO.
Mzungu akisema haki za wapenzi WA jinsia moja, wasomi uchwara nao HAO.
Mzungu akisema waliopewa mimba waendele na Shule, wenzangu na miye HAO wanarukia makida.

Huwezi iga watu ambao mpo tofauti nao Kwa karibu kila kitu.

Huwezi leta Demokrasia kwenye jamii ya watu masikini na wajinga Kama nchi za Afrika huko ni kuikandamiza Afrika na Nchi yako.

Hivi masikini tangu lini akawa na demokrasia?
Tangu lini masikini na mjinga akapewa demokrasia nauliza.

Demokrasia ya Wazungu ilikuja baada ya maendeleo kukua, baada ya watu kupata elimu.

Unaletaje Haki Sawa baina ya mwanamke na Mwanaume kwenye jamii ya watu masikini na wajinga. Ajabu Sana hii.
Haki Sawa inawafaa watu walioendelea kiasi na walioikimbia UMASIKINI.

Kwenye umasikini lazima mfumo mmoja utumike IMA ni mfumo jike au mfumo Dume.

Sasa unaruhusu wanawake wafanye kazi Kama wanaume alafu muda huo huo sheria hubadili unaacha Kama zilivyokuwa; mwanaume ndiye anawajibu WA kumtunza mwanamke! Hivi hiyo ni Akili kweli ndugu zangu.
Hivi hamuoni kuwa Kama mwanamke kwenye jamii masikini akipewa nafasi ya za kuajiriwa automatically tatizo la Ajira litajitokeza,

Hamfikirii kuwa Kuruhusu wanawake wafanye kazi automatically ni kuangusha taasisi ya ndoa. Hamuoni kuwa Vijana watachelewa kuoa kwani Ajira zitakuwa hakuna?

Wasomi lazima tuelewe kuwa, huwezi taka nchi yako masikini ifanane kimifumo na Nchi zilizoendelea.
Nchi zilizoendelea zinazouwezo wa kufanya hivyo Kwa sababu zimeshaendelea, kwenye maendeleo ndio kuna haki Sawa. Hata wanawake wakiajiriwa ni Sawa Kwa sababu serikali inajua wapi itapata pesa iwe Kwa kudhulumu na kunyonya nchi masikini au kuzitawala kabisa.

Sasa kanchi Kako hata uwezo wa kuvamia taifa jingine ili waibe Mali hakana unataka kuiga mambo ya nchi kubwa. Wasomi tuweni Sirius tunaongoza Nchi.

Kama serikali na wasomi ingekuwa inawapenda watoto wakike, ingeweka mipango na mikakati wasijiingize kwenye ngono zembe mapema, wangezuia watoto wasifanye zinaa ili wasipate matokeo ya zinaa ambayo huweza kuwa chanya au Hasi.

Wazungu sio kwamba wanaakili kutuzidi Waafrika isipokuwa viongozi na wasomi wa Afrika wengi wao ni bendera fuata UPEPO.

Msomi na serikali lazima tujiulize kuwa Mzungu na mataifa makubwa yanapotuamrisha Jambo Fulani, labda ni Uzazi wa mpango, au ushoga, ya Kuruhusu waliopewa mimba kuendelea na masomo, tujiulize mataifa hayo kipindi yakiwa na uchumi Kama wetu yaliruhusu mambo hayo?
Au ndio wametuhusu sasa hivi Kwa sababu washaelimisha jamii zao zikaelimika kiasi kwamba wanajua kabisa jamii zao mpaka watoto wanauelewa na elimu ya Uzazi wa mpango,

Wasomi na serikali lazima tujue kulinganisha na kutofautisha.

Lazima tujiulize, wakati Uingereza au USA ikiwa na Hali Kama yetu, ikiwa na miaka 60 tangu ipate Uhuru iliruhusu mambo ambayo inataka tuyafanye?

Sio wenzanu wamefikia level ya Kula mifupa na ninyi mpo level ya kunyonya maziwa na kunywa uji alafu wanawashinikiza mle mifupa wakati hamna Meno. Tuweni Makini Sana.

Jamii yoyote changa inahitaji sheria Kali zisizo na huruma.
Jamii na taifa likiwa masikini na ujinga mwingi linahitaji sheria Kali zisizo na huruma, huku elimu ikiendelea kutolewa.

Jamii ikishaendelea kiuchumi na kielimu ndio unaanza Kupunguza ukali wa SHERIA. Unatoa demokrasia, ndio mambo yanavyoenda hivyo.

Ustaarabu haumfai mtu mjinga na masikini Hilo kila siku ninasema na nitasema.

Serikali ninaiomba iache kuungana na Dunia ya Kwanza kuikandamiza jamii yake.

Wazungu wanatabia ya kujifanya wanakusaidia kumbe Kwa nyuma yake wanaagenda ya Siri kabisa ambayo huko mbeleni huwa mtego Kwetu.

Tangu zamani Wazungu walitumia serikali,
Dini, mashirika binafsi, watu mashuhuri, Elimu, misaada n.k kutawala Afrika.

Serikali ingejikita zaidi kuweka sheria Kali, wala isijali hawa wasomi fuata UPEPO wa Wazungu Kama bendera.

Nipumzike sasa.

Ni Yule Shahidi kutoka Nyota ya Tibeli.

Robert Heriel
Taikon wa Fasihi
Kwa sasa, KARIAKOO, DAR ES SALAAM
Una hisi tunaweza kwenda tofauti?,how?.
 
Back
Top Bottom