Je kunaulazima wowote wa kulazimasha wazazi kununua bidhaa shuleni

Mwanongwa

Senior Member
Feb 15, 2023
169
198
Mwalimu mmoja anayefahamika kwa jina la Yusuph wa shule ya Msingi ZIGA ya mchepuo wa kingereza iliyopo katika mji wa Makambako wilaya ya Wanging'ombe mkoani Njombe,anatuhumiwa na wazazi kwa kukataa kusahihisha madaftari ya wanafunzi ambayo hayana Nembo ya Shule hiyo.

Wazazi hao wamesema kuwa Mwalimu Yusuph amekuwa akigoma kusahihisha madaftari hayo kwa madai kuwa lazima yawe na Nembo ya shule hiyo.

Madaftari hayo yenye Nembo ya Shule yanauzwa kwa kiasi cha shilingi 3500 shuleni hapo, wakati daftari kama hizo ambazo hazina Nembo zinauzwa 2500 mtaani .

Kutokana na utofauti wa bei hizo wazazi wengi wameamua kununua daftari hizo mtaani ambako ni bei rahisi.

Je kunaulazima wowote wa kulazimasha wazazi kununua bidhaa shuleni wakati mtaani ni bei rahisi zaidi
 
Safi kabisa mwalimu. Nchi yenye wajinga wajinga kama hii fanya kila njia uyapige fedha. Kama tatizo dogo kama hili la kumalizwa na kikao cha wazazi na shule wanalalamika chinichini hao ni wajinga tu. Tena ikiwezekana weka masharti kuwa madaftari lazima yawe na nembo yenye picha yako.
 
Wazazi wengine jau sana mwalimu ana maana yake kufanya hivyo hamuwezi kumuelewa mpaka watoto watoke na Sifuri
 
Mwalimu anaforce mradi wa shule upate hela.
Mimi hata mambo ya kulazimisha sare za shule zinunuliwe shuleni siyaelewi kabisa.
 
Hayo mambo ya madaftari, masweter, Viatu (uniform) nk
yanahitaji busara ya kuwasiliana wazazi na uongozi wa Shule ili kila upande usijifanyie unavyo ona ni sawa.
Mf; Kuna shule mzazi akiomba kushona uniform zake anapewa kitambaa (sample) kuhakikisha anashona kinachofanana kabisa na zile zinazotolewa shuleni
na kuna shule ukihitaji kununua madafari unapewa maelekezo ya aina ya madaftari wanayoyahitaji.
Madafatari hayapimwi kwa ukubwa bali ubora wa karatasi. Mara nyingi yale madaftari yenye katasi nyeupe sana yana ubora zaidi kuliko yenye karatasi zenye weupe uliofifia.
 
Back
Top Bottom