masopakyindi
Platinum Member
- Jul 5, 2011
- 17,906
- 13,211
Kama kuna usafiri unaotumiwa na watu wa hali ya kawaida na chini kwa wingi ni pikipiki, tunazoziita bodaboda.
Huduma hii ni rahisi, haraka na unafika uendako kwa kasi sana ukilinganisha na usafiri binafsi au hata mabasi ya Mwendokasi(DART).
Lakini sekta hii haina uratibu wa aina yoyote nchini, si serikali kuu wala serikali za Mita na hata Jeshi letu la Polisi au wasimamizi wa usafiri LART.
Ni aibu kubwa kwamba itabidi mzungu aje atufundishe jinsi ya kudhiti na kuendeleza huu usafiri pendwa kwa wengi.
Chama Tawala kinawatumia bodaboda kama mtaji wa kisiaa, bila kuangalia athari zake kwa usalama wa hao vijana na abiria wao kwa ujumla.
Wahusika wakuu ni kama ifuatavyo:
1. TRA- Wanasajili tu bodaboda na kuzipa namba bila kuweka ukomo.
2. LATRA-Hawajui wafanye nini juu ya bodaboda maana hawajui hata waanzie wapi kuziratibu.
3. Serikali za Mitaa-Halmashauri hazitengi bodaboda zitumike vipi na wapi, wao hata leseni za biashara kwa bodaboda hawakagui.
4. POLISI - Hawa ndio kabisaa wamenyanyua mikono, hwawagusi bodaboda na sasa bodaboda ni kama panya anyechezea sharubu za paka mchana kweupe.
Sheria zipo,
Leseni - zaidi ya 40% ya bodaboda hawana leseni
Helmet - boda boda karibia 90% hakuna
Viatu - ndala ndio vazi kuu
Protective clothing - hakuna
Eye shields - hakuna
Kutokana na makosa hayo yanayotazamwa tu, boda boda wengi kama sio wote, wakifanya ajali, kitu cha kwanza ni kukimbia! Polisi wapo tu!
5. CCM- Sasa watambue kuwa mtaji wa bodaboda kisiasa umekuwa kero kuwa katika jamii. Lazima hatua za kisiasa zitumike kuwadhibiti na kuratibu kistaarabu.
Ajali iliyotokea leo Morogoro Road karibu na Fire, ni uthibitisho wa jinsi serikali kwa ujumla ilivyoshindwa kupanga na kuliweka katika mipango inayoeeweka usafiri huu wa Bodoboda.
USHAURI WANGU
Serikalini kuna ma PhD mengi tu hadi kwa viongozi wetu,ma PhD ya kuombea na kupata kazi, lakini wenye nayo hawajui waanzie wapi kiujumla namna ya kusaidia katika tatizo kama hili la kijamii, kazi na vijana.
Hivyo kwa vile sisi hatuna werevu wa kujtatulia haya matatizo, tutafute mzungu atufikirie nmna ya kuwapanga hawa vijana wa bodaboda na kupunguza vifo na vurugu katika Jamii.