Serikali imeiuza Kariakoo kwa Wachina

Serikali imeiuza Kariakoo kwa Wachina

Winga haumii chochote mkuu .wanaoumia ni wafanyabiashara wenye mitaji mkubwa

Maana mchina kakuuzia vitu toka kiwandani kwake ili uje uuze nchini.na yeye anakuja nchini tena anakuja kuuza kwa bei ya chini tena Hadi mikoani kwa wateja wadogo.wewe utauza wapi?
Na hii ndologistic ambayo watu hawaelewizwewe ukileta mali hapa unapigwa ushuru mrefu hujalipa kodi bado manispaa sijui ulinzi afu bei ulioipanga sokoni anaingia mchina anauza bei aliokuuzia kiwandani
 
Huko wapi kuna movement kubwa England ya kupinga wageni na waamiaji haramu

Marekani taifa lenye uchumi mkubwa wanalalamikia wageni nenda ujerumani afd chama cha mrengo wa kulia kinapinga wageni

Kama hizo nchi kubwa duniani zinapinga wageni kwanini ni kosa kwa Tanzania
Nina wazungumzia ni wageni wanao ishi kihalali. Hizo movements unazo sema za kibaguzi ukiwa ulaya ni kitu cha kuishi nacho. Serikali huwa ina waa assure nyie wageni walio halali usalama wenu na kuwahimiza kuendelea na shughuli zenu. Hata Trump anawatimua wale illegal immigrants tu.
 
Hapa Tanzania kuna Waarabu na Wahindi wenye lineage kubwa kukuzidi wewe hapo. Utakuta hata baba yake babu yako humjui.

Mansoor Daya mwaka 1962 kaanzisha kiwanda cha kwanza cha kutengeneza madawa ya binadamu hapa Tanzania. Kabla na baada ya hapo alikuwa Mtanzania hadi umauti unamfika 2024.

Kina GSM baba yao kaanza biashara mwaka 1955 na bado wapo.

Mzee Dewji kaanzisha METL miaka ya 1970s na bado yupo.

Mchina gani ana ukoo Tanzania vizazi vinne hata vitatu?
Unahukaka wahindi ukiowataja wana uchungu na TZ, Hao ni wawekezaji tu ukiwatibua wananyanyuka kama alivyofanya manji. Wana network kubwa sana nje ya nchi kuliko hata TZ mababu na jamaaa zao wapo india
 
Sawa, Wachina ndio wana uchungu na Tanzania si ndio?

Tanzania tunapata uhuru tulikuwa na Wahindi 110,000 ila wakaja fukuzwa, ondoka na kuhama baada ya Nyerere kuleta ujamaa. Wahindi kwa sasa ni wachache kuliko mwaka tunapata uhuru, walitakiwa wawe kwenye milioni moja na point ila walikimbia mazingira magumu ya nchi.

Similarly na hawa Wachina sio ndugu zetu, watanyonya kisha waache mashimo. Waje kuwekeza ila sio kuuza kuanzia pilipili kichaa, umachinga, kumiliki ardhi na migodi.
 
Jifunze namna ya kuishi nayo hiyo system inga mbinu zao ama sivyo jiunge nao mshirikiane kibiashara. Hii ya mwisho nadhani ni ngumu kwani sisi Watanzania ni wavivu na wezi kwa ufupi si waaminifu..
Umeongeza point ya muhimu sana.
 
Haiwezekani Kariakoo wachina wanaishi kama kwao.

Mbaya zaidi hawalipi kodi ipasavyo. TRA haina kanuni za asiye raia kulipa kodi kama mzawa

Hii ni sawa tu na kusema Kariakoo imeuzwa

Acheni wageni wapumue kidogo, mmewakalia kooni utafikiri tutaishi milele, hapo kwa asilimia kubwa unatumia vifaa vya mchina
 
Sawa, Wachina ndio wana uchungu na Tanzania si ndio?

Tanzania tunapata uhuru tulikuwa na Wahindi 110,000 ila wakaja fukuzwa, ondoka na kuhama baada ya Nyerere kuleta ujamaa. Wahindi kwa sasa ni wachache kuliko mwaka tunapata uhuru, walitakiwa wawe kwenye milioni moja na point ila walikimbia mazingira magumu ya nchi.

Similarly na hawa Wachina sio ndugu zetu, watanyonya kisha waache mashimo. Waje kuwekeza ila sio kuuza kuanzia pilipili kichaa, umachinga, kumiliki ardhi na migodi.

Kwani mchina akiuza pilipili kuna shida? Mbona tunakua wabinafsi hivyo mkuu!
 
Kwani mchina akiuza pilipili kuna shida? Mbona tunakua wabinafsi hivyo mkuu!
National interests ni muhimu kuliko ujamaa na kutokuwa mbinafsi. Hao Wachina wenyewe wana sera za kuwekeza kwao na lazima uzifuate.

Mbona hatuwaiti wabinafsi kwa kuzuia WhatsApp, kuwa na control ya real estate nchini kwao, kulazimisha transfer of technology kwa wawekezaji, kukiuka patents, kuiba rights na teknolojia.
 
Haiwezekani Kariakoo wachina wanaishi kama kwao.

Mbaya zaidi hawalipi kodi ipasavyo. TRA haina kanuni za asiye raia kulipa kodi kama mzawa

Hii ni sawa tu na kusema Kariakoo imeuzwa
Hehehe.......Ngoja nicheke
 
Acha kulegeza makalio dogo. Pambana ufanye biashara, hizo longolongo hutoboi popote.

Angalia Mchina anafanya nini nawe iga
Mkuu habari, hivi unaweza kuingia kwenye nchi ya mtu na kuanza kufanya biashara ndogo ndogo ndani ya mipaka ya hiyo nchi?
 
Mkuu habari, hivi unaweza kuingia kwenye nchi ya mtu na kuanza kufanya biashara ndogo ndogo ndani ya mipaka ya hiyo nchi?
Wachina wanafanya nchi ya kigeni kadri ya mazingira waliyoyakuta. Wamekuta sheria ziko loose wanapita humo humo.

Hili siyo tatizo la Tanzania bali ni la dunia nzima. Nenda majiji makubwa kama Newyork, Chicago London utazikuta China towns au Chinese restaurants zina shamiri tu
 
Mkuu kitu kama hujui ungenyamaza Tu
Hivi bakhresa anaezalisha ngano akianza kuuza chapati nyumba kwa nyumba huoni kuna madhara kwa watu maelfu wanaouza chapati?
Mchina ana kiwanda yeye auze kwa agent .agent auze kwa mtu wa jumla .yaani kinachotakiwa ni biashara ifate mkondo wake.wala winga hausiki hapa
Tatizo huku mna wivu na matajiri WA kariakoo
Why umpangie mtu auezeje hakuna mwenye wivu, ukiona mtu anakuchukia hizo ni feedback za matendo yako yaani hisia hazidanganyi Bali akili inadanganya.
Jiulize why mtu akuchukie yaani from nowhere akuchukie.
Imagine Kuna memory kadi ya 128gb nimeletewa na mchina akaniambia nimrudishie aliyonunulia kwao ambayo ni 15k nikashangaa mno nikamwambia kuwa hapa ni 87k akashangaa mno.
Kuna jamaa aliagiza Ile huwaei akalipa 400k iyo simu hapa inauzwa muda huo sh 1.6M.
So why mtu asifurahie kupata unafuu yaani watu wengi mno hawajui biashara,
Biashara ni mzunguko usikomalie faida kubwa mno,
Mie nikiagiza kitu cha laki nne nikipata hata faida 25-50 inanitosha mno Sina haja ya kuuza 1.6M.

Tulia Sasa si mlikuwa mnafurahia acha Sasa ivi na wengine wafurahie.

Pia hakuna tajiri hapo kariakoo , hebu niambie Kuna watu wangapi Wana miliki Dola bilioni moja kwenda juu.
Hao watu mnaowaona matajiri wakienda huko nje wanapoteana wanakuwa Kama machinga tu hapa bongo kwa nje.
Ni sawa na Yule jamaa ambaye ama duka Kijijini ana kigari ama boda yake basi anavimba anajiona yu tajiri kwa walimu wa primary au wakulima Ila akija hata mjini kidogo like bukoba mjini hata hakuna anayejua kuwa Kuna mtu mwenye hela.
Dar ni Kijijini MNo kulingnisha na huku mjini Stockholm.
Sema unamiliki dola laki 2-6 Ila unavimba na wewe unajiona ni tajiri .
Matajiri Africa wapo wachache like baresa, mo, Dangote wenye Dola bilioni moja and upward Ila hizo hela zako hata huwezi miliki mjengo New York Manhattan Wala hata sikuelewi Kama unazo hela.
Yaani unazo hela za kubadilisha mboga na wewe unajiona una hela.
Watu wanatoa misaada mpaka bilioni kadhaa za kitanzania Wana hela Sasa wewe hata kutoa msaada milioni moja ama laki moja ni kipengele
 
Sheria za uwekezaji nchini Tanzania ziko wazi kabisa: mgeni anayetaka kufanya biashara hapa ni lazima apitie TIC na awekeze kwenye miradi mikubwa kama viwanda, uzalishaji, au huduma za kimkakati. Lengo la sera hizi si kubana mtu, bali ni kulinda soko la ndani, kukuza uchumi wa taifa, kuleta ajira, na kuongeza mapato ya kodi serikalini. Tunapowaruhusu wageni kuingia kwenye biashara ndogondogo kama kuuza sokoni au kuzungusha bidhaa mitaani, tunaharibu mfumo wa kiuchumi na kukiuka misingi ya sheria za uwekezaji.

Biashara ndogondogo ni mhimili wa uchumi kwa Watanzania wa kawaida vijana, wamama, na familia zinazotegemea kipato cha kila siku. Tukifumbia macho uingiaji wa wageni kwenye eneo hili, tunaua ajira, tunapunguza mzunguko wa fedha mtaani, na hatimaye tunadhoofisha uwezo wa taifa kuzalisha bidhaa zetu wenyewe. Wageni wanapaswa kuleta mitaji mikubwa, kukuza teknolojia, kufungua viwanda na kutoa ajira si kushindana na mama ntilie au kijana wa bodaboda katika fremu za Kariakoo.

Tunaposema haya, si kwa sababu ya chuki wala wivu, bali kwa uzalendo na uchungu wa kulinda mustakabali wa uchumi wetu. Taifa linapofaidika kupitia kodi kubwa, ajira nyingi, na viwanda vinavyozalisha bidhaa zenye ubora, kila Mtanzania ananufaika. Hii ndiyo maana sera za uwekezaji ziliundwa ili zitoe mwongozo wa kulinda maslahi ya taifa, si kuacha masoko yetu ya ndani yakimezwa kimyakimya na wageni wanaotumia mianya ya udhaifu wa mifumo yetu. Tuwe wakarimu, lakini tuwe makini.
 
Kwani mchina akiuza pilipili kuna shida? Mbona tunakua wabinafsi hivyo mkuu!
Swali la "kwani Mchina akiuza pilipili kuna shida?" linaonekana rahisi, lakini lina mzizi mpana wa kisera na kisheria. Sio kwamba kuna shida kwa mtu kuuza pilipili, bali ni nani anayeuza, chini ya utaratibu gani, na kwa madhumuni gani. Sheria za Tanzania kuhusu uwekezaji haziruhusu raia wa kigeni kufanya biashara ndogondogo kama kuuza pilipili sokoni, kuuza mitaani au kufungua fremu ndogo hizi ni biashara zilizotengwa kwa wazawa kwa lengo la kulinda ajira na soko la ndani.

Uwepo wa mgeni kwenye eneo la biashara ndogondogo unamaanisha ushindani usio sawa kwa Mtanzania wa kawaida anayelipa kodi, anayetegemea biashara hiyo kwa kuendesha familia, na ambaye hana mtaji mkubwa wa kupambana na bidhaa kutoka viwandani China. Huu sio ubinafsi, ni uzalendo. Kama tunaruhusu kila mgeni kufanya biashara za mtaani, basi hatuwezi kulinda wazawa, hatuwezi kukuza viwanda, na hatuwezi kuongeza kodi ya maana kwa taifa letu.

Kwa hiyo, hoja si pilipili hoja ni kanuni, usawa na heshima kwa sera za nchi yetu. Kama mgeni anataka kuuza pilipili, ajenge kiwanda cha kusindika pilipili, aajiri Watanzania, alipe kodi kubwa, na aingie kwa taratibu sahihi kupitia TIC. Hapo hakuna atakayemlaumu. Tuko kwenye safari ya kuijenga Tanzania ya viwanda na uchumi wa kati hatuwezi kufika huko kwa kuruhusu kila mmoja kuingia tu kwenye biashara bila mwelekeo wa kitaifa.
 
Acheni wageni wapumue kidogo, mmewakalia kooni utafikiri tutaishi milele, hapo kwa asilimia kubwa unatumia vifaa vya mchina
Ni kweli kabisa kuwa dunia ya sasa imeunganishwa sana kiuchumi, na hatuwezi kukwepa kutumia bidhaa kutoka nje, ikiwemo China. Lakini hoja ya msingi hapa si chuki wala uonevu kwa wageni ni kusimamia sheria, kulinda soko la ndani, na kutetea ajira kwa Watanzania wa kawaida. Kama taifa, hatuwezi kuacha kila mtu afanye anachotaka bila kufuata sera na taratibu tulizojiwekea kwa faida ya wote.

Sera ya uwekezaji Tanzania iko wazi: mgeni anatakiwa kuja kuwekeza kwenye miradi mikubwa kama viwanda, si kushindana na vijana wa mtaani kwenye fremu, vibanda au kuuza sokoni bidhaa za bei ya chini. Tunaposema hivyo hatusemi wageni wasipumue bali wasifanye kazi ambazo kisheria zimetengwa kwa wazawa. Hili si suala la "kuwakalia kooni," ni kusimamia haki ya taifa na kuhakikisha kuwa uchumi wetu unajengwa kwa msingi wa usawa na utaratibu.

Watanzania wana haki ya kufanya biashara kwa mazingira yenye ushindani wa haki. Tukiendelea kuruhusu kila mgeni kuingia kwenye biashara ndogondogo, tutajikuta tumewatupa nje wazawa waliopaswa kuwa nguzo ya uchumi wa taifa. Tunahitaji wawekezaji wa kweli, si wachuuzi wa kimataifa wanaotumia mianya ya sheria kujinufaisha binafsi. Tuwapokee wageni kwa mikono miwili, lakini tuwaongoze kufuata utaratibu sahihi unaolinda taifa letu kwa vizazi vijavyo.
 
Back
Top Bottom