Uongo serikali haijafuta service charge zaidi shilika linabadili tariff tu kama ifuatavyo
KUBADILISHA TARIFF KWA WATEJA WANAOISHI VIJIJINI
Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) linapenda kuwataarifu wateja wake wote wa maeneo ya vijijini kuwa kuanzia tarehe 20 Januari, 2016 wateja wote wa maeneo ya vijiji watakaounganishiwa umeme kwa kutumia njiamoja (single phase) wataingizwa kwenye ‘Tariff D1’ kuanzia mwanzo.
Wateja wa umeme wa njia moja wa maeneo ya vijijini ambao kwa sasa wapo kwenye ‘Tariff T1’ na ambao matumizi yao ya umeme hayazidi wastani wa uniti 75 kwa miezi mitatu mfululizo, watahamishiwa ‘Tariff D1’. Kazi ya kuwahamisha wateja hao tayari imeanza na inatarajiwa kukamilika ifikapo mwishoni mwa mwezi Machi 2016.
Mteja wa kijijini atakaye hamishiwa kwenye ‘Tariff D1’ atapewa namba maalum (Key Change Number) kwa ajili ya kubadilisha Tariff kwenye mita yake pia. Namba hizo pamoja na maelezo yake zitatolewa wakati mteja atakaponunua umeme kwa mara ya kwanza baada ya kuhamishwa kwenye ‘Tariff D1’.
Mteja anaweza pia kupata Key Change Number pamoja na maelezo yake kwenye kituo cha huduma kwa njia ya simu kwa kupiga simu namba 022 2194400 au 0768 985100.
Imetolewana: OFISI YA UHUSIANO TANESCO – MAKAO MAKUU.