The Evil Genius
JF-Expert Member
- Mar 21, 2014
- 5,895
- 19,064
Taarifa nilionayo ni kwamba serikali imeagiza watu wote kubadilishiwa taarif za Tanesco na kusajiliwa taarifu 0 au D1 ambayo haina service charge za kila mwezi.
Mameneja wote wa Tanesco wa wilaya wameagizwa wahakikishe hili linafanikiwa..
Inaweza kuwa habari njema kwa watu wasiopenda service charges.
========
Mameneja wote wa Tanesco wa wilaya wameagizwa wahakikishe hili linafanikiwa..
Inaweza kuwa habari njema kwa watu wasiopenda service charges.
========
Tofauti na ilivyoripotiwa na wachangiaji mbalimbali katika vyombo vya habari, Shirika la Ugavi wa Umeme nchini (TANESCO) limekanusha taarifa kwamba limefuta tozo ya huduma kwa wateja (service charge) ambayo huwa linawatoza wateja wake kila mwisho wa mwenzi pale wanaponunua umeme, FikraPevu linaripoti.
Akizungumza na FikraPevu, Msemaji wa Wizara ya Nishati na Madini, Badra Masoud, amekanusha taarifa hizo zilizosambazwa katika mitandao ya kijamii, ukiwemo mtandao wa JamiiForums, ambao ni mtandao dada na gazeti hili. “Hakuna kitu kama hicho,” alisema kwa kifupi kwa njia ya simu.
Soma zaidi >> TANESCO yakomalia Tozo ya Huduma kwa Wateja