Mphamvu
JF-Expert Member
- Jan 28, 2011
- 10,702
- 3,288
Kufuatia vuguvugu la migomo katika vyuo vikuu, na sababu kubwa ikiwa ni watu kukosa mikopo, au walopata kucheleweshewa fedha za kujikimu, serikali iliunda tume ya kuchunguza matatizo ya sekta ya elimu ya juu iliyoongozwa na Profesa Makenya Mabhoko wa UDSM. Sina hakika, ila nahisi tume ilishamaliza kazi yake na kukabidhi mapendekezo kwa serikali.
Karibuni, Tume ya Vyuo vikuu nchini ilitoa kitabu cha mwongozo wa kozi na namna ya kudahiliwa kwenye vyuo, kwa mwaka 2012-2015. Nilichokiona kipya humo ni ktabu hiko kuweka wazi nafasi ya kozi husika katika kupata udhamini kutoka bodi ya mikopo (sponsorship status), na katika hilo, kozi nyingi sana, pengine zaidi ya nusu, zimeandikiwa kuwa hazina kabisa udhamini, kwa maneno mengine, kozi hizo sio kipaumbele cha bodi.
Chuo Kikuu cha Dar es salaam kwa mfano, kozi 28 kati ya 58 zitakazotolewa mwaka ujao wa masomo hazina kabisa mkopo, hii ni karibu nusu. Baadhi ya hizo zenye mkopo, zipo zenye mkopo wa laki 5 na ambazo zinapata udhamini wa 100%...
Sasa kama haya ndio mapendekezo ya tume iliyoundwa kuchunguza matatizo ya elimu ya juu na kupendekeza masuluhisho...
Unaweza kupitia kitabu hapo chini (right click, halafu chagua "save target as")
View attachment 53420View attachment 53420
Tulianza taratibu, kwanza waliopata Div I, kikaja kigezo cha umasikini wa familia, tukaja kwa wanaosoma science na ualimu, sasa wameamua kuweka wazi kabisa bila kificho.