Serikali imedhamiria kujitoa kabisa kudhamini elimu ya juu? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Serikali imedhamiria kujitoa kabisa kudhamini elimu ya juu?

Discussion in 'Jukwaa la Elimu (Education Forum)' started by Mphamvu, May 4, 2012.

 1. Mphamvu

  Mphamvu JF-Expert Member

  #1
  May 4, 2012
  Joined: Jan 28, 2011
  Messages: 10,708
  Likes Received: 935
  Trophy Points: 280
  Kufuatia vuguvugu la migomo katika vyuo vikuu, na sababu kubwa ikiwa ni watu kukosa mikopo, au walopata kucheleweshewa fedha za kujikimu, serikali iliunda tume ya kuchunguza matatizo ya sekta ya elimu ya juu iliyoongozwa na Profesa Makenya Mabhoko wa UDSM. Sina hakika, ila nahisi tume ilishamaliza kazi yake na kukabidhi mapendekezo kwa serikali.
  Karibuni, Tume ya Vyuo vikuu nchini ilitoa kitabu cha mwongozo wa kozi na namna ya kudahiliwa kwenye vyuo, kwa mwaka 2012-2015. Nilichokiona kipya humo ni ktabu hiko kuweka wazi nafasi ya kozi husika katika kupata udhamini kutoka bodi ya mikopo (sponsorship status), na katika hilo, kozi nyingi sana, pengine zaidi ya nusu, zimeandikiwa kuwa hazina kabisa udhamini, kwa maneno mengine, kozi hizo sio kipaumbele cha bodi.
  Chuo Kikuu cha Dar es salaam kwa mfano, kozi 28 kati ya 58 zitakazotolewa mwaka ujao wa masomo hazina kabisa mkopo, hii ni karibu nusu. Baadhi ya hizo zenye mkopo, zipo zenye mkopo wa laki 5 na ambazo zinapata udhamini wa 100%...
  Sasa kama haya ndio mapendekezo ya tume iliyoundwa kuchunguza matatizo ya elimu ya juu na kupendekeza masuluhisho...
  Unaweza kupitia kitabu hapo chini (right click, halafu chagua "save target as")
  View attachment 53420 View attachment 53420
  Tulianza taratibu, kwanza waliopata Div I, kikaja kigezo cha umasikini wa familia, tukaja kwa wanaosoma science na ualimu, sasa wameamua kuweka wazi kabisa bila kificho.
   
 2. Perry

  Perry JF-Expert Member

  #2
  May 4, 2012
  Joined: Feb 24, 2011
  Messages: 10,029
  Likes Received: 868
  Trophy Points: 280
  Nawahurumia sana madogo wanaobaki vyuoni hasa wale wanaotoka familia zetu zile.
   
 3. s

  sugi JF-Expert Member

  #3
  May 4, 2012
  Joined: Feb 12, 2011
  Messages: 1,367
  Likes Received: 113
  Trophy Points: 160
  daa inatia uchungu,madogo wanajipinda form six,huku mbele nuru inafifia sasa!
   
 4. m

  mchaga89 Member

  #4
  May 4, 2012
  Joined: May 4, 2012
  Messages: 10
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  msaada jamani nina division 3 point 13 kis D histo C na geo S vp udsm ninaweza kuchaguliwa?
   
 5. Perry

  Perry JF-Expert Member

  #5
  May 5, 2012
  Joined: Feb 24, 2011
  Messages: 10,029
  Likes Received: 868
  Trophy Points: 280
  inategemea na kozi utakayoomba.
   
 6. K

  Kiumbo JF-Expert Member

  #6
  May 5, 2012
  Joined: Feb 4, 2012
  Messages: 561
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 0
  Hata nami nimeiona hiyo nimeshindwa kuelewa b.Com,sociology,journalism,law zenye watu wengi hazina mkopo kabisa dahh naona giza mbele.
   
 7. Msafiri Kasian

  Msafiri Kasian JF-Expert Member

  #7
  May 5, 2012
  Joined: Sep 9, 2011
  Messages: 1,813
  Likes Received: 169
  Trophy Points: 160
  Hii ndo maana mimi nimekosa matumaini na serikali iliyomadarakani(CCM). Na hivi ndivyo walivyozamisha ndoto yangu ya kusoma mambo ya biashara mwaka jana,na sasa wananilazimisha mwaka huu niombe kusomea mambo ya ualimu! Mi nashangaa! je,unaweza kumlazimisha ng'ombe kwenda mtoni na kumlazimisha kunywa maji? Lah hasha! Wasitegemee utendaji mzuri wa kizazi hiki wanachokilazimisha kuwa waalimu.
   
 8. Lukub

  Lukub JF-Expert Member

  #8
  May 9, 2012
  Joined: Feb 5, 2012
  Messages: 646
  Likes Received: 459
  Trophy Points: 80
  Ni muda tu watacma hata facult za science 50% badae 0% halafu loan board itavunjwa na rafiki zangu wa loan board mtakosa ajira du
   
 9. Vegetarian

  Vegetarian JF-Expert Member

  #9
  May 9, 2012
  Joined: Apr 7, 2012
  Messages: 607
  Likes Received: 274
  Trophy Points: 80
  The failed system!
   
 10. Mphamvu

  Mphamvu JF-Expert Member

  #10
  May 11, 2012
  Joined: Jan 28, 2011
  Messages: 10,708
  Likes Received: 935
  Trophy Points: 280
  Kuna suluhisho lolote katika hili? au ndo tukubaliane na hali halisi...
   
 11. Mphamvu

  Mphamvu JF-Expert Member

  #11
  May 11, 2012
  Joined: Jan 28, 2011
  Messages: 10,708
  Likes Received: 935
  Trophy Points: 280
  Na wewe ni graduate Kiumbo?
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 12. Shoo Gap

  Shoo Gap JF-Expert Member

  #12
  May 11, 2012
  Joined: Mar 11, 2009
  Messages: 236
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 35
  Nami jana nilikuwa namsaidia ndugu yangu kufanya application, nikashangaa sana. Ni lazima tuamke jamani, hii hali ya kuwa kimya itatugharimu sana. Ina maana mtoto wa maskini hawezi kusoma hata kama amefaulu. Kama tuition fee kwa kozi za ualimu ni 1.6M unapewa mkopo wa 0.5M mtoto wa maskini itakuwaje? Je! watoto wote wa masikini ndo wakasome ualimu hata kama wamepata div.1? Ni lazima jamii yetu tuamke tupige kelele serikali ya ccm iache kucheza na hatma ya vijana wa Tz. Watetezi wetu wabunge wanafahamu hili?
   
 13. Kinyungu

  Kinyungu JF-Expert Member

  #13
  May 11, 2012
  Joined: Apr 6, 2008
  Messages: 4,381
  Likes Received: 3,341
  Trophy Points: 280
  Hivi huwa inakuwaje mzazi asomeshe mwanaye St. MARY tangu chekechea hadi form six halafu akifika chuo aombe mkopo wa kusoma BA General wa Tshs laki 8? Serikali itumie kigezo kimoja tu kuwapa wanafunzi mikopo na kigezo hicho kiwe ni kuwapa mkopo wanafunzi waliosoma shule za wajela jela basi.
   
 14. OLESAIDIMU

  OLESAIDIMU JF-Expert Member

  #14
  May 11, 2012
  Joined: Dec 2, 2011
  Messages: 19,193
  Likes Received: 184
  Trophy Points: 160
  Kinyungu hii assumption kama yako ndo imesababisha tatizo kubwa tangu awali wengi. Ikumbukwe kuwa wanafunzi wengi husaidiwa A level katika shule nzuri kwa gharama kubwa na ndugu wakijua wakifaulu watapata mkopo, so mtoto akifaulu ndugu hujitoa kwa sababu wanajua kuna mkopo. Kwa kigezo chako wengi sana hubaki kama mayatima na wasio na msaada baada ya kuhukumiwa na historia hii.Hii imetesa wengi sana na bado ipo mpaka sasa.......so lazima kujipanga na kuweka vigezo vitavyoweza kufanya kazi kwa ufasaha HESLB hawajafanya kazi yoyote ya maana katika kurekebisha makosa yake
   
 15. Chiwa

  Chiwa JF-Expert Member

  #15
  May 11, 2012
  Joined: Apr 17, 2008
  Messages: 1,388
  Likes Received: 717
  Trophy Points: 280
  do inauma mno! halafu sina msaada! najiona kama mpumbavu na mkosaji kwa jamii iliyo shule. nashindwa kuelewa tunajenga mfumo gani wa elimu inabidi maskin tujipange upya na hasa tunapowachagua hawa mchwa wetu hawana msaada kabisa na cc. hivi hizi pesa za mfuko wa jimbo ambao kila mbunge anapewa mill 50 haziwezi kujenga uwezo wa kugharamia mikopo hii? binafsi sielewi na nina hasira kiasi kwamba sina hata mchango wa maana wa mawzo
   
 16. Perry

  Perry JF-Expert Member

  #16
  May 11, 2012
  Joined: Feb 24, 2011
  Messages: 10,029
  Likes Received: 868
  Trophy Points: 280
  Watanzania bana!ivi kipindi kile wana Udsm tunapiga kunji ili kuishinikiza serikar iondoe hayo mashart ya kipuuzi ya kugawa mikopo kwa makundi,c ni nyie nyie mlokua mnatuita ce wahuni,wavuta bangi na majina yote mabaya.asa ivi mambo yamekaba zaidi,lawama tena kwa serikari yenu?na kwa nyepes tu zilizoko mtaan ni kwamba,kufikia 2014,serikari itakua imejitoa kufadhiri elimu ya juu,itakua ni kila familia ibebe msalaba wake yenyewe.nawahurumia sana madogo mtakao kosa mikopo,kwa maana maisha ya chuo bila bumu yanakua co kabisa.
   
 17. The secretary

  The secretary JF-Expert Member

  #17
  May 11, 2012
  Joined: Jan 14, 2012
  Messages: 4,161
  Likes Received: 45
  Trophy Points: 145
  Hapo umenena kelele za waliowaita wavuta bangi watatukumbuka
   
 18. Remote

  Remote JF-Expert Member

  #18
  May 11, 2012
  Joined: May 20, 2011
  Messages: 14,875
  Likes Received: 1,562
  Trophy Points: 280
  nakushauri usiombe kabsa mahali hapo, kwa div yako. Mimi mwaka jana mdogo wangu div 2 ya12 kakosa nafac na aliomba education.
   
 19. G

  Godwishes JF-Expert Member

  #19
  May 11, 2012
  Joined: Aug 26, 2011
  Messages: 577
  Likes Received: 52
  Trophy Points: 45
  Student's Govt.Vyuo vyote tz ha tutawaelewa,ikitokea ishu ya namna.Organise Kunji nac tulio uraiani tutawasapot
   
 20. Jimbi

  Jimbi JF-Expert Member

  #20
  May 18, 2012
  Joined: Aug 16, 2010
  Messages: 871
  Likes Received: 23
  Trophy Points: 35
  mwaka 2015 muache tena kujitokeza kupiga kura, nafikiri mmeisoma namba sasa. bravo magamba
   
Loading...