Serikali imedhamiria kujitoa kabisa kudhamini elimu ya juu?

Mphamvu

JF-Expert Member
Jan 28, 2011
10,702
3,285
Kufuatia vuguvugu la migomo katika vyuo vikuu, na sababu kubwa ikiwa ni watu kukosa mikopo, au walopata kucheleweshewa fedha za kujikimu, serikali iliunda tume ya kuchunguza matatizo ya sekta ya elimu ya juu iliyoongozwa na Profesa Makenya Mabhoko wa UDSM. Sina hakika, ila nahisi tume ilishamaliza kazi yake na kukabidhi mapendekezo kwa serikali.

Karibuni, Tume ya Vyuo vikuu nchini ilitoa kitabu cha mwongozo wa kozi na namna ya kudahiliwa kwenye vyuo, kwa mwaka 2012-2015. Nilichokiona kipya humo ni ktabu hiko kuweka wazi nafasi ya kozi husika katika kupata udhamini kutoka bodi ya mikopo (sponsorship status), na katika hilo, kozi nyingi sana, pengine zaidi ya nusu, zimeandikiwa kuwa hazina kabisa udhamini, kwa maneno mengine, kozi hizo sio kipaumbele cha bodi.

Chuo Kikuu cha Dar es salaam kwa mfano, kozi 28 kati ya 58 zitakazotolewa mwaka ujao wa masomo hazina kabisa mkopo, hii ni karibu nusu. Baadhi ya hizo zenye mkopo, zipo zenye mkopo wa laki 5 na ambazo zinapata udhamini wa 100%...

Sasa kama haya ndio mapendekezo ya tume iliyoundwa kuchunguza matatizo ya elimu ya juu na kupendekeza masuluhisho...

Unaweza kupitia kitabu hapo chini (right click, halafu chagua "save target as")
View attachment 53420View attachment 53420
Tulianza taratibu, kwanza waliopata Div I, kikaja kigezo cha umasikini wa familia, tukaja kwa wanaosoma science na ualimu, sasa wameamua kuweka wazi kabisa bila kificho.
 
Nawahurumia sana madogo wanaobaki vyuoni hasa wale wanaotoka familia zetu zile.
 
daa inatia uchungu,madogo wanajipinda form six,huku mbele nuru inafifia sasa!
 
msaada jamani nina division 3 point 13 kis D histo C na geo S vp udsm ninaweza kuchaguliwa?
 
Hata nami nimeiona hiyo nimeshindwa kuelewa b.Com,sociology,journalism,law zenye watu wengi hazina mkopo kabisa dahh naona giza mbele.
 
Hii ndo maana mimi nimekosa matumaini na serikali iliyomadarakani(CCM). Na hivi ndivyo walivyozamisha ndoto yangu ya kusoma mambo ya biashara mwaka jana,na sasa wananilazimisha mwaka huu niombe kusomea mambo ya ualimu! Mi nashangaa! je,unaweza kumlazimisha ng'ombe kwenda mtoni na kumlazimisha kunywa maji? Lah hasha!

Wasitegemee utendaji mzuri wa kizazi hiki wanachokilazimisha kuwa waalimu.
 
Ni muda tu watacma hata facult za science 50% badae 0% halafu loan board itavunjwa na rafiki zangu wa loan board mtakosa ajira du
 
Hata nami nimeiona hiyo nimeshindwa kuelewa b.Com,sociology,journalism,law zenye watu wengi hazina mkopo kabisa dahh naona giza mbele.

Na wewe ni graduate Kiumbo?
 
Last edited by a moderator:
Hii ndo maana mimi nimekosa matumaini na serikali iliyomadarakani(CCM). Na hivi ndivyo walivyozamisha ndoto yangu ya kusoma mambo ya biashara mwaka jana,na sasa wananilazimisha mwaka huu niombe kusomea mambo ya ualimu! Mi nashangaa! je,unaweza kumlazimisha ng'ombe kwenda mtoni na kumlazimisha kunywa maji? Lah hasha! Wasitegemee utendaji mzuri wa kizazi hiki wanachokilazimisha kuwa waalimu.
Nami jana nilikuwa namsaidia ndugu yangu kufanya application, nikashangaa sana. Ni lazima tuamke jamani, hii hali ya kuwa kimya itatugharimu sana. Ina maana mtoto wa maskini hawezi kusoma hata kama amefaulu. Kama tuition fee kwa kozi za ualimu ni 1.6M unapewa mkopo wa 0.5M mtoto wa maskini itakuwaje?

Je! watoto wote wa masikini ndo wakasome ualimu hata kama wamepata div.1? Ni lazima jamii yetu tuamke tupige kelele serikali ya ccm iache kucheza na hatma ya vijana wa Tz. Watetezi wetu wabunge wanafahamu hili?
 
Hivi huwa inakuwaje mzazi asomeshe mwanaye St. MARY tangu chekechea hadi form six halafu akifika chuo aombe mkopo wa kusoma BA General wa Tshs laki 8? Serikali itumie kigezo kimoja tu kuwapa wanafunzi mikopo na kigezo hicho kiwe ni kuwapa mkopo wanafunzi waliosoma shule za wajela jela basi.
 
Kinyungu hii assumption kama yako ndo imesababisha tatizo kubwa tangu awali wengi. Ikumbukwe kuwa wanafunzi wengi husaidiwa A level katika shule nzuri kwa gharama kubwa na ndugu wakijua wakifaulu watapata mkopo, so mtoto akifaulu ndugu hujitoa kwa sababu wanajua kuna mkopo.

Kwa kigezo chako wengi sana hubaki kama mayatima na wasio na msaada baada ya kuhukumiwa na historia hii.Hii imetesa wengi sana na bado ipo mpaka sasa.......so lazima kujipanga na kuweka vigezo vitavyoweza kufanya kazi kwa ufasaha HESLB hawajafanya kazi yoyote ya maana katika kurekebisha makosa yake
 
do inauma mno! halafu sina msaada! najiona kama mpumbavu na mkosaji kwa jamii iliyo shule. nashindwa kuelewa tunajenga mfumo gani wa elimu inabidi maskin tujipange upya na hasa tunapowachagua hawa mchwa wetu hawana msaada kabisa na cc. hivi hizi pesa za mfuko wa jimbo ambao kila mbunge anapewa mill 50 haziwezi kujenga uwezo wa kugharamia mikopo hii? binafsi sielewi na nina hasira kiasi kwamba sina hata mchango wa maana wa mawzo
 
Watanzania bana!ivi kipindi kile wana Udsm tunapiga kunji ili kuishinikiza serikar iondoe hayo mashart ya kipuuzi ya kugawa mikopo kwa makundi,c ni nyie nyie mlokua mnatuita ce wahuni,wavuta bangi na majina yote mabaya.asa ivi mambo yamekaba zaidi,lawama tena kwa serikari yenu?na kwa nyepes tu zilizoko mtaan ni kwamba,kufikia 2014,serikari itakua imejitoa kufadhiri elimu ya juu,itakua ni kila familia ibebe msalaba wake yenyewe.nawahurumia sana madogo mtakao kosa mikopo,kwa maana maisha ya chuo bila bumu yanakua co kabisa.
 
Hapo umenena kelele za waliowaita wavuta bangi watatukumbuka
 
msaada jamani nina division 3 point 13 kis D histo C na geo S vp udsm ninaweza kuchaguliwa?
nakushauri usiombe kabsa mahali hapo, kwa div yako. Mimi mwaka jana mdogo wangu div 2 ya12 kakosa nafac na aliomba education.
 
Student's Govt.Vyuo vyote tz ha tutawaelewa,ikitokea ishu ya namna.Organise Kunji nac tulio uraiani tutawasapot
 
mwaka 2015 muache tena kujitokeza kupiga kura, nafikiri mmeisoma namba sasa. bravo magamba
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom