Umenena ukweli kabisa,Mtu hawezi kusema kuwa mshahara umechelewa au serikali imechelewa kulipa mishahara wakati hata mwezi tu haujaisha, serikali yetu chini ya uongozi shupavu na madhubuti Ni lazima ipongezwe Sana kwa namna ambavyo imekuwa ikiwahisha mishahara kwa watumishi wa umma.
Ni Tanzania pekee chini ya mama yetu shupavu na mchapa kazi ambapo watumishi wa umma wanapata na kupokea mishahara Yao kabla ya mwezi kuisha,Ni Tanzania pekee chini ya uongozi wa mama yetu na Rais wetu ambapo huwezi ukaona mwezi ukiisha pasipo kuwalipa mishahara ya watumishi wa umma.
Watumishi wa umma Wana kila sababu ya kumshukuru na kumpongeza Sana mh Rais wetu kwa namna anavyowajali ,ikiwepo kuwalipa mishahara kwa wakati,kuwapandishia mishahara,kuwa pandisha madaraja na kuwalipa kulingana na madaraja,kuwalipa malimbikizo Yao yote,kuwalipa posho mbalimbali n.k
Kwa hakika mama yupo kazini, serikali ipo macho na inamtazama kila mtu na kila sehemu.
Watumishi Wa umma waendelee kuchapa kazi na kujituma, waendelee kufanya kazi kwa uadilifu na Nidhamu,watangulize mbele maslahi ya Taifa na kuwa wanyenyekevu kwa watanzania wafuatapo huduma katika ofisi za umma. Mama ana mipango mizuri na watumishi wa umma ,anawapenda na kuwajali sana ndio maana amewaahidi mengi mazuri na makubwa.kila Mtumishi wa umma anakwenda kucheka na kutabasamu mwaka huu na kila mmoja ataandika jina la Rais wetu mama Samia kwa machozi ya furaha katika moyo wake.