Ileje: Walimu wanusurika kutwangana ngumi wakidai kujitoa CWT

Jul 14, 2021
5
5
Baadhi ya Walimu wa Shule za Msingi na Sekondari katika Halmashauri ya Wilaya ya Ileje Mkoani Songwe wanaotaka kujitoa katika Chama cha Walimu Tanzania (CWT) wakiwa katika Ukumbi wa Ofisi ya Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri hiyo wameshinikiza kukubaliwa maombi yao ya kutaka kujitoa CWT, wakidai walituma maombi hayo miezi 5 bila kupewa majibu sahihi.

Walimu hao wamelazimika kwenda kwa Mwajiri (Ofisi ya Mkurugenzi wa Halmashauri) baada ya kudai kuzungushwa na CWT kwa muda mrefu.

Akizungumza kwa niaba ya Walimu Yodan Kalonge amesema "Tulileta fomu za kujiondoa CWT na kuomba kujiunga na CHAKUWAHATA tangu Julai (2023) lakini shida CWT walileta pingamizi tusijiondoe, kwa hiyo mgogoro ndio ulikuwa hapo, tulikaa meza moja kufanya maridhiano lakini CWT hawataki."

Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri hiyo, Herman Njeje amekiri kuwapokea Walimu hao na kuwaelekeza kufuata taratibu.

Mwenyekiti wa CHAKUWAHATA - Ileje, Kalonge Bwenda anasema:

CHAKUWAHATA ni Chama cha Kutetea na Kulinda Maslahi ya Walimu Tanzania kilianzishwa Mwaka 2015, hapo kati kutokana na kujipanga ndio maana hatukuwa tunasikika sana, lakini miaka ya hivi karibuni kasi yetu ya kuboresha chama imekuwa kuwa kutokana na yanayoendelea ndani ya CWT.

CHAKUWAHATA – Ileje tuliunda uongozi na kufanya mchakato wa usajili kisha kuutambulisha kwa Mkurugenzi wa Halmashauri, Julai 2023, akasema tuendelee kuwasilisha fomu za Wanachama wanaojiunga.

Mchakato ukafanyika kwa kufuata taratibu zote lakini ili tuweze kuendelea tukatakiwa kuwasilisha nakala za kujitoa Uanachama wa CWT, wenzetu hao wakagoma kupokea nyaraka zetu, hata tulivyojaribu kutuma kwa EMS napo wakagoma kupokea.

Jumla yetu tulikuwa Walimu 172, sababu ya sisi kusisitiza kujitoa ni kwa kuwa tuliingizwa kwenye chama hicho bila hiyari yetu, hatukujaza fomu.

Pili wanatukata 2.5% kila mwezi katika mshahara wakati CHAKUWAHATA wanakata Tsh. 5,000 kwa kila mtu, hivyo nasi tunahitaji kuongeza kipato kwenye mishahara yetu.

Tatu hatujui kuhusu mapato na matumizi ya CWT, mambo mengi yanaenda kienyeji na pia viongozi wa juu walimdharau Rais, wanateuliwa wanakataa, kuna nini hasa ambacho wanakipata ndani ya chama mpaka wanagomea uteuzi wa Rais?

Wanachama tumechukua, kumbe wana maslahi na mishahara yetu.

Vurugu zilizotokea
Kilichotokea jana (Novemba 10, 2023) ni kwamba walikuwa wanashikilia msimamo wao wa kugoma kupokea nyaraka, wakataka kutuitia Polisi kuwa tumevamia ofisini kwao.

Tukatoka tukaenda kwa Afisa Utumishi na Mkurugenzi kama mwajiri wetu, mwisho tumefikia muafaka wamesema watatuondoa.

Wamekubali tutume nyaraka kwa njia ya Posta na watakubali kupokea na kutuondoa kwenye uanachama wa CWT.

CHAKUWAHATA kimeshaambaa mikoa mingi na mpaka kipo mikoa ya Tanga, Dar, Mbeya, Kigoma, Mwanza, Arusha na kwingineko.
 
Ndani ya chama cha walimu si shwari, walimu wengi hawakipendi chama chao hicho wanakiona ni cha kifisadi. Ukiwa unagombea uongozi kama una mawazo ya kiliberali wahafidhina watahakikisha hushindi ili usilete mabadiliko chamani kuondoa ufisadi. Walimu wengi wanakiona chama chao hicho hakiwasaidii katika maslahi yao ya kikazi kiasi cha kutaka kuanzisha chama kingine wanachoona hakitakuwa cha kifisadi
 
Ndani ya chama cha walimu si shwari, walimu wengi hawakipendi chama chao hicho wanakiona ni cha kifisadi. Ukiwa unagombea uongozi kama una mawazo ya kiliberali wahafidhina watahakikisha hushindi ili usilete mabadiliko chamani kuondoa ufisadi. Walimu wengi wanakiona chama chao hicho hakiwasaidii katika maslahi yao ya kikazi kiasi cha kutaka kuanzisha chama kingine wanachoona hakitakuwa cha kifisadi
...CWT imekuwa kama Kituo Cha Polisi ! Kuingia Rahisi TU, Kutoka ni Shughuli !!
 
...CWT imekuwa kama Kituo Cha Polisi ! Kuingia Rahisi TU, Kutoka ni Shughuli !!
wanasema once unaajiriwa kwenye kazi ya ualimu utakatwa tu ile asilimia mbili ya mshahara wako hata kama wewe si mwanachama rasmi wa CWT. Halafu utaingizwa kwa lazima uanachama utake usitake. Wanadai ukiwa mwalimu unafaidi yale wanayoyapambania kama chama cha walimu automatically, hivyo basi ni lazima uwe mwanachama uendelee kufaidi matunda wanayoyapambania
 
Mi mwenyewe hapa nilinusurika kupigwa na kupinduliwa kabisa kutoka kwenye ukatibu wa CWT baada ya kuwasainisha walimu wenzangu wakatwe asilimia mbili bila wao kutaka. Walijikuta wamesaini, kuja kushituka wamesaini, tayari fomu ziko wilayani na ujanja wa kujitoa hawana. Wakaishia kunilaumu kuwa nimewaingiza kiujanja kwenye chama wasichokitaka wakihisi hela zao zitakatwa bure
 
Back
Top Bottom