Sisi wazazi tunaosomesha watoto wetu shule ya sekondari Venance Mabeyo tulikaa kikao cha wazazi na kukubaliana kila mzazi kuchangia limu moja kwa kila mtoto ili kufanikisha zoezi la ufundishaji shuleni hapo,cha kushanga watoto wetu wamekuwa wakipigwa kila Mara wanapokuwa kwenye mitihani ikiwa watatumia karatasi zaidi ya moja.Sababu ya kuchapwa watoto ni kuwa shule imekuwa ikuuza rimu pamoja na kupokea pesa za rimu hivyo kuishia kwenye mifuko ya walimu hivyo kupelekea uhaba wa rimu(Karatasi) shuleni
Mfano hivi juzi watoto walifanya mtihani wa Mock mkoa ,shule ilikosa limu na kupelekea sisi wazazi kuingia gharama ya kununua karatasi kwa ajili ya kujibia mitihani.
Kuna taarifa kuwa shuleni hapo hakuna rimu(karatasi) hata moja,zote zimeuzwa mbaya zaidi mwalimu aliyekuwa anahusika na kuchangisha rimu(karatasi) amekuwa akiwataka watoto wampe pesa shilingi 10,000 ili wasidaiwe rimu(karatasi) na matokeo yake huwa anakula hizo pesa.
Wazazi baadhi tulimfuata mkuu wa shule lakini hakuweza kuweka bayana aliahidi kulishughulikia lakini mpaka muda huu hakuna rimu hata moja shuleni hapo ambapo shule hii ina watoto 600,huku watoto waliolipia rimu(karatasi) wakiwa zaidi ya mia nne(400),huku mitihani iliyofanyika shuleni hapo ni mitihani minne tutoka January hadi muda huu ninapoandika uzi huu ila shuleni hakuna hata karatasi moja ,ikumbukwe kuwa rimu moja ina karatasi 500,hata kama iweje mtoto mmoja hawezi tumia karatasi 500,kwa mitihani minne maana yake mtoto ametumia karatasi zaidi ya 125 kwa mtihani mmoja
Hivyo sisi wazazi tunaomba serikali iingilie kati kwani hali hii inatuumiza sisi wazazi na kutukatisha tamaa maana tunajitoa ili kufanikisha elimu lakini walimu wanauza rimu na kutumia pesa kwa matumizi binafsi