DOKEZO Ufisadi wa kutisha jiji la Arusha. Shule, wanafunzi wakamuliwa mamilioni ya fedha za mitihani, wakuu wa shule wahoji ruzuku ya Serikali inafanya nini?

Hili ni dokezo maalum toka kwa mwananchi mtumiaji wa JF mwenye nia ya kuusaidia umma kuwa na taarifa 'maalum'

waziri2020

Senior Member
May 31, 2019
190
451
Wakati serikali ikiingia mfukoni kugharamia elimu bure kwa shule zake za msingi na sekondari hapa nchini kwa kutoa mabilioni ya ruzuku, mambo ni tofauti kabisa kwa jiji la Arusha, ambapo afisa elimu wa jiji hilo, Bakari Hussein ameziagiza shule zote za msingi zipatazo 163 katika jiji hilo, kuhakikisha zinachangia RIMU za mitihani kuanzia Rimu 6 hadi 60 kwa kila shule.

Hatua hiyo imewalazimu wakuu wa shule hizo pamoja na wamiliki wa shule binafsi Jiji la Arusha kutoa kilio chao baada ya kuchoshwa na mashinikizo yanayotolewa na Afisa Elimu huyo, Bakari Hussen huku wakihoji ruzuku ya serikali inayotolewa kila mwezi inaenda wapi?

Aidha wamehoji iweje mambo haya yajitokeze sasa wakati serikali inatoa ruzuku au ni aina nyingine ya upigaji, wamesema toka halmashauri imeanza haijawahi tokea shule moja kutoa karatasi za rimu 30 hadi 57 kwa ajili ya mitihani ya muhula wa kwanza tu tena bila hata kushirikisha wamiliki ama wakuu wa shule.

Pamoja na Rimu hizo kila mwanafunzi wa darasa la saba na la nne ametakiwa kuchangia sh 4,000 kwa ajili ya mitihani ya Mock na shule zote zikitakiwa kulipa haraka iwezekanavyo huku watoto wakitishwa kutofanya mtihani iwapo hawataleta hiyo hela.

Walimu wakuu wamekuwa wakitumiwa jumbe zisizo na maadili za vitisho kutoka kwa maafisa Taaluma hao wakiambuwa wasipofikia malengo watahamishwa vituo vyao vya kazi, jambo linaloonekana ni Maslahi binafsi na sio sera ya serikali.

Pia shule zimeagizwa kugharamia machapisho ya mitihani ambapo kila mtihani ni sh. 2,500 na ipo mitihani 10 hivyo kila shule italazimika kulipa Tsh. 25,000 na kwa shule zote 163 ni sawa na Tsh. 4,075,000/=

Maafisa elimu kata wameagizwa kuhakikisha wanakusanya michango hiyo pamoja na karatazi za RIMU na zinafika kwa wakati jambo ambalo wameiomba serikali kupitia wizara ya elimu kutazama kwa jicho la tatu huu ufisadi unaofanywa na jiji la Arusha kwani hawana imani kama unabaraka za wizara.

Soma orodha ya shule jinsi zilivyopangiwa kuwasikisha rims pamoja na MSG za vitisho kutoka Idara ya Elimu jiji la Arusha, kwenda kwa wakuu wa shule kushinikiza michango ikamilike kwa wakati

Screenshot_20230422_100707_WhatsApp.jpg
Screenshot_20230422_100637_WhatsApp.jpg
 
Elimu tanzania kila afisa elimu anajiamlia atakavyo ,kila mkoa unaamua unavyo jisikia yaani tabu tupu

Kuna mikoa wanafunzi wanatoka saa nane na nusu mikoa mingine saa tisa na nusu

Kuna mikoa siku ya ijumaa wanafunzi wanatoka saa 6 na nusu shule zingine wanatoka saa tisa na nusu

Mikoa mingine mitihani ya MOCK wanachangishwa elfu 7000 halafu baada ya hapo shule zinatumiwa softcopy zi buruze zenyewe yaan kila mkoa inategemeana na afisa elimu mkoa atakavyo jisikia tabu tupu tabu tupu kwenye nchi hii kila kitu kipo hovyo
 
waziri2020 umezidi majungu kuhusu Elimu Jiji la Arusha,
Unafahamu fika Mitihani Arusha inatungwa na kuandaliwa mkoani,idadi ya ream hutokana na idadi ya watahiniwa,fedha zinazotumika ni asilimia ya mitihani mashuleni.Tatizo lako nini?
Jiji la Arusha limeendelea kufanya vizuri katika ufaulu,wahusika uliowataja ndio chachu ya mafanikio hayo.
Nakushauri ujihusishe na shughuli zingine kwani unafahamika vizuri tu na yanayokusibu.
 
Elimu tanzania kila afisa elimu anajiamlia atakavyo ,kila mkoa unaamua unavyo jisikia yaani tabu tupu

Kuna mikoa wanafunzi wanatoka saa nane na nusu mikoa mingine saa tisa na nusu

Kuna mikoa siku ya ijumaa wanafunzi wanatoka saa 6 na nusu shule zingine wanatoka saa tisa na nusu

Mikoa mingine mitihani ya MOCK wanachangishwa elfu 7000 halafu baada ya hapo shule zinatumiwa softcopy zi buruze zenyewe yaan kila mkoa inategemeana na afisa elimu mkoa atakavyo jisikia tabu tupu tabu tupu kwenye nchi hii kila kitu kipo hovyo
Hahaha,ni kama biashara ya uchangudoa, Kila dada poa na bei yake ,Raha Sanaa,
 
Elimu tanzania kila afisa elimu anajiamlia atakavyo ,kila mkoa unaamua unavyo jisikia yaani tabu tupu

Kuna mikoa wanafunzi wanatoka saa nane na nusu mikoa mingine saa tisa na nusu

Kuna mikoa siku ya ijumaa wanafunzi wanatoka saa 6 na nusu shule zingine wanatoka saa tisa na nusu

Mikoa mingine mitihani ya MOCK wanachangishwa elfu 7000 halafu baada ya hapo shule zinatumiwa softcopy zi buruze zenyewe yaan kila mkoa inategemeana na afisa elimu mkoa atakavyo jisikia tabu tupu tabu tupu kwenye nchi hii kila kitu kipo hovyo
Hizo gharama mostly zinaenda kwenye chakula cha wanafunzi na wasimamizi kwa siku mbili za mitihani.Na sehemu kubwa wazazi ndio wamepiga mahesabu na kukubaliana kiasi hicho.
 
Elimu tanzania kila afisa elimu anajiamlia atakavyo ,kila mkoa unaamua unavyo jisikia yaani tabu tupu

Kuna mikoa wanafunzi wanatoka saa nane na nusu mikoa mingine saa tisa na nusu

Kuna mikoa siku ya ijumaa wanafunzi wanatoka saa 6 na nusu shule zingine wanatoka saa tisa na nusu

Mikoa mingine mitihani ya MOCK wanachangishwa elfu 7000 halafu baada ya hapo shule zinatumiwa softcopy zi buruze zenyewe yaan kila mkoa inategemeana na afisa elimu mkoa atakavyo jisikia tabu tupu tabu tupu kwenye nchi hii kila kitu kipo hovyo
Hizo gharama mostly zinaenda kwenye chakula cha wanafunzi na wasimamizi kwa siku mbili za mitihani.Na sehemu kubwa wazazi ndio wamepiga mahesabu na kukubaliana kiasi hicho.
 
Wakati serikali ikiingia mfukoni kugharamia elimu bure kwa shule zake za msingi na sekondari hapa nchini kwa kutoa mabilioni ya ruzuku, mambo ni tofauti kabisa kwa jiji la Arusha, ambapo afisa elimu wa jiji hilo, Bakari Hussein ameziagiza shule zote za msingi zipatazo 163 katika jiji hilo, kuhakikisha zinachangia RIMU za mitihani kuanzia Rimu 6 hadi 60 kwa kila shule.

Hatua hiyo imewalazimu wakuu wa shule hizo pamoja na wamiliki wa shule binafsi Jiji la Arusha kutoa kilio chao baada ya kuchoshwa na mashinikizo yanayotolewa na Afisa Elimu huyo, Bakari Hussen huku wakihoji ruzuku ya serikali inayotolewa kila mwezi inaenda wapi?

Aidha wamehoji iweje mambo haya yajitokeze sasa wakati serikali inatoa ruzuku au ni aina nyingine ya upigaji, wamesema toka halmashauri imeanza haijawahi tokea shule moja kutoa karatasi za rimu 30 hadi 57 kwa ajili ya mitihani ya muhula wa kwanza tu tena bila hata kushirikisha wamiliki ama wakuu wa shule.

Pamoja na Rimu hizo kila mwanafunzi wa darasa la saba na la nne ametakiwa kuchangia sh 4,000 kwa ajili ya mitihani ya Mock na shule zote zikitakiwa kulipa haraka iwezekanavyo huku watoto wakitishwa kutofanya mtihani iwapo hawataleta hiyo hela.

Walimu wakuu wamekuwa wakitumiwa jumbe zisizo na maadili za vitisho kutoka kwa maafisa Taaluma hao wakiambuwa wasipofikia malengo watahamishwa vituo vyao vya kazi, jambo linaloonekana ni Maslahi binafsi na sio sera ya serikali.

Pia shule zimeagizwa kugharamia machapisho ya mitihani ambapo kila mtihani ni sh. 2,500 na ipo mitihani 10 hivyo kila shule italazimika kulipa Tsh. 25,000 na kwa shule zote 163 ni sawa na Tsh. 4,075,000/=

Maafisa elimu kata wameagizwa kuhakikisha wanakusanya michango hiyo pamoja na karatazi za RIMU na zinafika kwa wakati jambo ambalo wameiomba serikali kupitia wizara ya elimu kutazama kwa jicho la tatu huu ufisadi unaofanywa na jiji la Arusha kwani hawana imani kama unabaraka za wizara.

Soma orodha ya shule jinsi zilivyopangiwa kuwasikisha rims pamoja na MSG za vitisho kutoka Idara ya Elimu jiji la Arusha, kwenda kwa wakuu wa shule kushinikiza michango ikamilike kwa wakati

View attachment 2595945View attachment 2595946
 
Back
Top Bottom