Serikali ianzishe mfumo wa "internship" kwa Walimu wahitimu kuliko kujitolea

Kajeba

JF-Expert Member
Oct 15, 2020
827
1,965
Habari JF,

Hakuna kitu kinaumiza kama msomi na mwalimu aliyesomea na kufuzu mafunzo ya ualimu na kwenda kufanya kazi katika shule za serkali kwa kujitolea bure

Hakika hii haikubaliki, ni unyonyaji wa kiwango kisichoelezeka. Mtu kufanya kazi bure ndani ya nchi hii ni kinyume na haki za binadamu kwamba kila mtu anahaki ya ajira na kulipwa

Ni vema serkali kupitia TAMISEMI ikaanzisha mfumo rasmi wa kuwataka walimu waihudumie serkali kwa malipo kidogo ndani ya mwaka mmoja.

Hii itasaidia kujenga uzoefu kwa walimu na kupunguza uhaba wa walimu, pia hakutakuwa na ukanjanja katika kada hii
 
Wazo lako ni zuri ila lina ubinafsi sana kwa kuona hao wa kada nyingine hawastahili kulitumikia taifa hili
 
Naunga mkono hoja, hii iende sambamba na kuundwa ile Bodi ya kitaaluma itakayosimamia mchakato huu wa Internship.

Baada ya hapo ndio watatakiwa wasajiliwe na kupewa leseni ndipo waingie sokoni.

Taaluma zingine wanafanya, kwa nini walimu wakwame?
 
Kada zingine nyingi zinautaratibu wa namna hii, ualimu tu ndio upoupo
Wazo lako ni zuri ila lina ubinafsi sana kwa kuona hao wa kada nyingine hawastahili kulitumikia taifa hili
 
Hoja yako ni ya msingi Sana mkuu,ajira zinatangazwa na kigezo kikubwa Cha kupata uwe unajitolea kiukweli hapo wanaumiza Sana unajitoleaje bure ,mda huo unakula kwa Nan,familia yako inaishije,kiukweli hapo serikal bado inahji kubadili mfumo huo..
 
Pamoja kwamba baadhi ya maneno yamenichekesha ila nakuunga mkono 100% kwa hoja yako .Na hii ingekuwa pia kwa fani nyingine zenye upungufi wa watumishi kama kilimo/ mifugo nk
 
Back
Top Bottom