Hasara za walimu na waganga wa kujitolea ni kubwa kuliko faida

tpaul

JF-Expert Member
Feb 3, 2008
21,859
18,282
Serikali inapaswa kufikiria mara mbili kabla ya kutekeleza programu ya walimu na waganga wa kujitotea. Kwa mujibu wa utafiti wa haraka nilioufanya, nimebaini hasara zake ni kubwa mara 100 kuliko faida. Utafiti wangu umejikita katika hoja zifuarazo:

Mosi, kwa mujibu wa muongozo uliotolewa na serikali, rasilimali zitakazotumika kuwalipa waajiriwa hawa wa kujitolea ni pamoja na mapato ya ndani ya halmashauri, shughuli za kuongeza mapato shuleni na michango kutoka kwa wazazi na wadau wengine wa maendeleo.

Ukisoma tu namna posho za walimu na waganga hawa wa kujitolea zitakavyopatikana utaona tayari kuna tatizo. Kila mwaka CAG amekuwa akiibua ufujaji wa matrilioni ya fedha za umma kwenye halmashauri, taasisi na mashirika ya umma. Sasa halmashauri wamepata kisingizio kipya cha kufuja fedha za umma – posho za walimu wa kujitolea.

Halmashauri zitaanza sasa kufuja fedha za umma kwa manufaa ya wachumiatumbo wachache kwa kisingizio cha kwamba fedha hizo zimeenda kulipa walimu wa kujitolea kumbe zimeingia mifukoni mwa wajanja wachache kwa maslahi finyu ya matumbo yao makubwa na familia zao.

Kwenye michango ya wazazi nako kuna tatizo. Serikali imekuwa ikijinasibu kutoa elimu bure lakini kimsingi wazazi wanalipa michango mingi mno zaidi ya karo waliyokuwa wakilipa hapo awali. Wakati wazazi wakihangaika na michango ya kawaida, imekuja michango mingine ya kuchangia posho za walimu wa kujitolea. Hii itakuwa balaa juu ya balaa.
1687011926631.jpeg

Mzazi akionyesha hasira za kuchoshwa na michango ya shule

Kumbuka pia bajeti iliyosomwa juzi imewakandamiza wananchi kwa kiasi kikubwa sana. Mwananchi safari hii atakamuliwa hadi atakonda kama ng’onda. Mungu aepushie mbali balaa hili la walimu wa kujitolea.
1687012040278.jpeg

Watanzania tunakamuliwa mno!

Na kibaya zaidi, shule na vyuo wamekuwa wakiwatumikisha wanafunzi kwa muda mrefu bila kusoma kwa kigezo cha kufanya kazi za Elimu ya Kujitegemea (EK) ili wapate mapato. Sasa hali itakuwa mbaya sana huko mashuleni. Watoto watakuwa hawasomi kisa kufanyishwa kazi kutwa nzima kutafuta posho za kuwalipa walimu wa kujitolea. Badala ya elimu kupanda, itakuwa inashuka kila kukicha.
1687012122403.jpeg

Wanafunzi wakitumikishwa kutafuta posho za walimu wa kujitolea

Pili, katika utatuzi wa migogoro serikali imetoa mwongozo kuwa migogoro itatuliwe kwa mazungumzo baina ya mwajiri na mwajiriwa na ikiwa mgogoro utashindwa kutatuliwa upelekwe tume ya tumishi wa walimu (TSC). Na ikiwa TSC watashindwa kuutatua mgogoro husika, basi mwalimu huyo avunjiwe mkataba na kufukuzwa kazi kama mbwa! Hii sio sawa.

Kwa mfano, ikiwa mwalimu husika alikuwa anadai malimbikizo ya posho za kujikimu, atafukuzwa kazi na hatalipwa posho zake ng’o! Huu ni zaidi ya utumwa. Hata kama ajira ni ngumu hakuna haja ya kuwatendea watanzania wenzetu kama mbwa! Kwanini serikali imegoma kupeleka migogoro tume ya usuluhishi na upatanishi (CMA) badala yake wakaamua kuweka masharti kandamizi ya kuwafukuza kama mbwa! Huu ni uhuni uliopitiliza. Kifungu hiki kitawafanya walimu wengi kutokuwa tayari kujitolea.

Tatu, ikiwa serikali ina ubunifu wa kuanzisha vyanzo vya mapato ya kuwalipa walimu wa kjitolea kwanini mapato hayo yasiingizwe kwenye bajeti ya serikali ili walimu hao waajiriwae kwa mikataba ya kudumu? Wanakimbilia mikataba ya muda (kujitolea) kwa sababu wanafahamu ni rahisi kuwakandamiza walimu wakiwa kwenye ajira za kujitolea kuliko wakiwa kwenye ajira za kudumu. Huu ni ukikwaji mkubwa wa haki za binadamu na utawala bora. Inasikitisha serikali inapowageuza job seekers kuwa watumwa ndani ya nchi yao.

Nawasilisha.
1687012387614.png
 
View attachment 2660479
Mzazi akionyesha hasira za kuchoshwa na michango ya shule

Kumbuka pia bajeti iliyosomwa juzi imewakandamiza wananchi kwa kiasi kikubwa sana. Mwananchi safari hii atakamuliwa hadi atakonda kama ng’onda. Mungu aepushie mbali balaa hili la walimu wa kujitolea.
View attachment 2660481
Watanzania tunakamuliwa mno!

Na kibaya zaidi, shule na vyuo wamekuwa wakiwatumikisha wanafunzi kwa muda mrefu bila kusoma kwa kigezo cha kufanya kazi za Elimu ya Kujitegemea (EK) ili wapate mapato. Sasa hali itakuwa mbaya sana huko mashuleni. Watoto watakuwa hawasomi kisa kufanyishwa kazi kutwa nzima kutafuta posho za kuwalipa walimu wa kujitolea. Badala ya elimu kupanda, itakuwa inashuka kila kukicha.
View attachment 2660483
Wanafunzi wakitumikishwa kutafuta posho za walimu wa kujitolea

Pili, katika utatuzi wa migogoro serikali imetoa mwongozo kuwa migogoro itatuliwe kwa mazungumzo baina ya mwajiri na mwajiriwa na ikiwa mgogoro utashindwa kutatuliwa upelekwe tume ya tumishi wa walimu (TSC). Na ikiwa TSC watashindwa kuutatua mgogoro husika, basi mwalimu huyo avunjiwe mkataba na kufukuzwa kazi kama mbwa! Hii sio sawa.

Kwa mfano, ikiwa mwalimu husika alikuwa anadai malimbikizo ya posho za kujikimu, atafukuzwa kazi na hatalipwa posho zake ng’o! Huu ni zaidi ya utumwa. Hata kama ajira ni ngumu hakuna haja ya kuwatendea watanzania wenzetu kama mbwa! Kwanini serikali imegoma kupeleka migogoro tume ya usuluhishi na upatanishi (CMA) badala yake wakaamua kuweka masharti kandamizi ya kuwafukuza kama mbwa! Huu ni uhuni uliopitiliza. Kifungu hiki kitawafanya walimu wengi kutokuwa tayari kujitolea.

Tatu, ikiwa serikali ina ubunifu wa kuanzisha vyanzo vya mapato ya kuwalipa walimu wa kjitolea kwanini mapato hayo yasiingizwe kwenye bajeti ya serikali ili walimu hao waajiriwae kwa mikataba ya kudumu? Wanakimbilia mikataba ya muda (kujitolea) kwa sababu wanafahamu ni rahisi kuwakandamiza walimu wakiwa kwenye ajira za kujitolea kuliko wakiwa kwenye ajira za kudumu. Huu ni ukikwaji mkubwa wa haki za binadamu na utawala bora. Inasikitisha serikali inapowageuza job seekers kuwa watumwa ndani ya nchi yao.

Nawasilisha.
View attachment 2660487
halafu unakuta mapoyoyo ya ccm humu jf yanasema mkataba wa Tanzania na Dpw ni mzuri kumbe yanafanya hivyo ili yalipwe buku saba.
 
Taratibu mwanangu tpaul ajira zimekuwa ngum mno miaka kibao tupo kitaa sasa tunasaka hata hizo za kujitolea lakini wapi.
Sikana kwamba wafanyakazi wa facart mbalimbali wana jitosheleza, ndiyo maana tunaoja bora tupate hata hizo za kuitolea. Japo hatuzipendi tunajipa moyo kwamba huwenda zikatupa mwanga kidogo.
 
Nakuelewa mkuu lakini hizi ajira za kujitolea zinaturudisha enzi za utumwa mamboleo. Tusipochukua hatua sasa serikali itaanza kuwageuza walimu misukule na cheap labour kwenye halmashauri. Wakishaona muitiko ni mkubwa, watasitisha kutoa ajira za kudumu.
 
Hatua gani tuchukuwe?
 
Hatua gani tuchukuwe?
Hatua za kuchukua ni kuichagiza serikali ipunguze matumizi ya matanuzi ili kuokoa fedha zitakazotumika kuajiri walinu mikataba ya kudumimu. Hii milataba ya muda mfupi inahujumu nguvu na ujuzi wa wslimu
 
Hata hizi za kujitolea Bado ni kizungu mkuti. Nipo nahangaikia kazi ya kujitolea sekta flani lengo kusaidia jamii
.Lakini Bado nakatwa chenga kibao wakati nijambo mhimu hata kuipunguzia serikali mzigo.
 
Back
Top Bottom