Serikali ianzishe posho ya walimu ili kudumisha uzalendo kwa kizazi cha Watanzania

Bando la wiki

JF-Expert Member
May 23, 2023
319
884
Watoto wa Kitanzania wanafundishwa na walimu wenye msongo mwingi wa mawazo kwa kufanya kazi huku wakiwaza future ya maisha yao.

Watoto hawawezi kuja kuwa wazalendo nchi hii kwa sababu, walimu ambao ndio role model wao (kwa sababu wanakao nao muda mrefu wa makuzi yao) muda wote wanailamu serikali kwa kuwatelekeza kwa mishahara midogo.

Ndo maana kila anayepewa nafasi nchi hii anawaza ni kivipi atajivutia pande lake hata kama ni kwa kuiba mali za umma.

Nini cha kufanya;
1. Serikali ithamini mchango wa mwalimu wa nchi hii kwa kuwa ndie mwenye jukumu muhimu la kushape ni kwa namna gani jamii ya kitanzania iwe.

2. Serikali ithamini mchango wa mwalimu kwa kuanzisha posho maalum ijulikanayo kama UALIMU ALLOWANCE. Hii posho itakuwa flat rate kwa kila mwalimu kuanzia msingi hadi sekondari, kiasi cha tshs 200,000 kitaingizwa kwenye kila account ya mwalimu ifikapo katikati ya mwezi.

3. Hiki kiasi sio cha kuchukulia mkopo ndo maana kitakuwa kikitolewa katikati ya mwezi ili ku boost kipato cha walimu ambao wengi wao mishahara yao midogo imeathiriwa na makato lukuki ya benki.

Serikali nadhani posho hii kwa walimu ni muhimu kuliko posho mnazolipana ninyi viongozi wetu na wenza wenu.

Ni muda muwe mnafikiria kizazi mnachopanda kitakuja kuweje, maana kinapita kwenye mikono ya walimu wengi maskini na wazazi masikini.
 
Kada ipi ina allowance tofaut na vyombo vya ulinzi na usalama
 
Ukiondoa posho ya utawala kwa viongozi, hizi posho wanazolipwa vyombo vya dola ni kutokana na ugumu wa kazi yao(night duties&higher risk of being killed for the sake of raia) na kukosa muda wa kujitafutia kipato nje ya mshahara muda mwingi hutumia wakiwa kazini.

Njoo kwa walimu;kwa mwaka wanalikizo 4 na kwa mwaka huenda likizo ya siku 28(mwezi),kazini hutoka saa 9:30 kwahiyo mtaona ni kwa kiasi gani walimu wana muda mwingi wa kujitafutia riziki nje ya mshahara.

Haiwezi kutoa nchi hii serikali ikalipa posho kwa walimu wote,posho hulipwa kwa kuzingiatia vigezo.

Anyway, Inshaallah!! Mom Kizimkazi atuone sisi walimu.
 
Acha wivu, unateseka ukiwa wapi ndugu. By the way walimu Wana future ya kizazi kijacho. Wakilipwa hivyo viposho wewe utapungukiwa Nini? Hebu mara moja moja uwe unawajulia hali walimu waliokufundisha na kufikia hapo ulipo.
Kila la kheri.
 
Waalimu walistahili posho hizi
  • Posho ya nyumba 300,000/-
  • posho ya maji/umeme/gesi 250,000/-
  • posho ya chakula 300,000/-
  • Extraduty 800,000/-
 
Mkuu sema serikali irudishe posho ya walimu. Hii posho ilikuwapo enzi za mh. Ally Hassan Mwinyi ila ikaondolewa na Mkapa. Ilikuwa inaitwa teaching allowance na ni 50% ya basic salary.
 
Mkuu sema serikali irudishe posho ya walimu. Hii posho ilikuwapo enzi za mh. Ally Hassan Mwinyi ila ikaondolewa na Mkapa. Ilikuwa inaitwa teaching allowance na ni 50% ya basic salary.
Ni jambo la ajabu sana viongozi wa Tanzania kujipendelea wenyewe
 
Back
Top Bottom