Serikali iangalie huduma ya mazishi kwa wasiosali/wasioamini dini

Lakini sikuona pahala mleta mada ameonyesha au kujitambulisha kuwa Mkristo wala kulalamika mazishi ya Kikristo.

Sitakosea nikisema unajistukia wewe na hicho ulichokitaja hapo,mleta mada kuzikwa ni kuzikwa tu hakuna atakaekuacha uzagae zagae hovyo.
Ukienda Msikiti wa Maamur pale Upanga utaona pameandikwa Huduma za Mazishi ni 30,000 ila kama hauna hela ni bure, unapewa Gari ya maiti, facilities za kumsafisha marehemu na mambo mengine. Kifupi kwa waisilamu alichosema mtoa mada hakipo, hatuachi mtu awe mzoga,

Kama mtu sio muisilamu hatutomswalia tu, ila tunamzika.
 
Hivi mkitaka kulalamikia Ukristo wenu kwani ni lazima muutaje na Uislam?

Unaweza kuniambia misikiti inatumiaje kigezo cha mazishi kumkomoa mtu ambaye hajashiriki kikamilifu katika mambo ya dhehebu lake?

Unaujua utaratibu wa Mazishi kwa mujibu wa Uislam?
Ni kweli madhehebu ya wakristo wana ubaguzi wa mazishi na huduma nyingine za kiroho kwa wale ambao wanaonekana kutoshiriki kwa kiwango cha kuridhisha shughuli mbalimbali za madhehebu yao.
 
Ukienda Msikiti wa Maamur pale Upanga utaona pameandikwa Huduma za Mazishi ni 30,000 ila kama hauna hela ni bure, unapewa Gari ya maiti, facilities za kumsafisha marehemu na mambo mengine. Kifupi kwa waisilamu alichosema mtoa mada hakipo, hatuachi mtu awe mzoga,

Kama mtu sio muisilamu hatutomswalia tu, ila tunamzika.
Sasa kilichofanya kushirikisha Ukristo na alichosema mleta mada ulikitoa wapi wakati yeye haku-mention mambo ya imani?

Hapo kwenye bold wote wanafanya hata ambao siyo waislam,binadamu timamu hawezi kuacha kumzika mwenzake kwa sababu ya itikadi,kama serikali wanazika manispaa kama mkazi wa mtaa wanazika wananchi so ulikuwa umwambie tu kwamba asiogope atazikwa hata na serikali siyo kuanza kufananisha vitu.
 
Ni kweli madhehebu ya wakristo wana ubaguzi wa mazishi na huduma nyingine za kiroho kwa wale ambao wanaonekana kutoshiriki kwa kiwango cha kuridhisha shughuli mbalimbali za madhehebu yao.
Tu-assume mleta mada ni atheist na ni ndugu yangu mimi Mkristo,always modern atheist wametokana na familia zinazomuabudu Mungu so kuzaliwa kwake ktk familia ya Kikristo hakumfanyi awe Mkristo akishavuka aged 14,sijawahi hata mara moja kumuona akifanya lolote linalohusiana na Ukristo lakini afe nikalitake Kanisa limsalie akiwa maiti,yaani alipokuwa hai na akili zake timamu hakuwahi hata mara moja kumkiri Mungu lakini leo afe mkusanyane waamini eti mnaombea maiti imkiri Mungu?

Ukristo upo clearly (mimi Mkatoliki wengine sijui) kwamba mimi kwa kinywa changu na kwa matendo yangu niukiri uwepo wa Mungu na siyo kwa kulazimishwa ni kwa utashi wangu mwenyewe na wote Wakatoliki wanalijua hilo siyo nisubiri nife nijifariji ndugu zangu watamkiri Mungu badala yangu hilo halipo na nadhani hata mwenye akili hawezi kukubali kujumuika na watu kulalamika kwanini ndugu yake hajazikwa kwa ibada huku akijua huyo anaezikwa alikuwa mambo hayo hayataki.
 
Mi hoja ya mtoa mada nimeielewa, japo na Mimi sijapenda alipotaja na "misikiti", angetaja makanisa tu.

Hoja... Maeneo ya vijiji vyenye wakristo wengi huwa kuna makaburi ya makanisa tu, hakuna makaburi ya serikali (vijiji), sasa mtu asie muumini au aliyetengwa akifa inabidi azikwe nyumbani kwake, au kwao au kwenye vichaka vya matambiko ya machifu, hii so sawa, lazima kuwa na Sheria inayolazimisha kila Kijiji kuwa na eneo la kuzikia wananchi nje ya maeneo ya makanisa

Ikiwezekana kusiwe na maeneo ya makanisa, kuwe na maeneo ya kiserikali tu kwa watu wote
 
We we si mshirika wa kanisa Wala msikiti ukiwa hai kwann ulazimishe ushiriki ukiwa maiti
 
Mi hoja ya mtoa mada nimeielewa, japo na Mimi sijapenda alipotaja na "misikiti", angetaja makanisa tu.

Hoja... Maeneo ya vijiji vyenye wakristo wengi huwa kuna makaburi ya makanisa tu, hakuna makaburi ya serikali (vijiji), sasa mtu asie muumini au aliyetengwa akifa inabidi azikwe nyumbani kwake, au kwao au kwenye vichaka vya matambiko ya machifu, hii so sawa, lazima kuwa na Sheria inayolazimisha kila Kijiji kuwa na eneo la kuzikia wananchi nje ya maeneo ya makanisa

Ikiwezekana kusiwe na maeneo ya makanisa, kuwe na maeneo ya kiserikali tu kwa watu wote
Ni maeneo ya kijiji, kijiji ndio Serikali,sema kijiji ugawa pande mbili upande wa Wakristo na wa waislamu hata mijini makaburi mengi ni ya serikali na Serikali ya mtaa ndio ugawa pande zote mbili sawa.

Makaburi ya kanisa au msikiti huwa ni makaburi ya Dini moja tu mfano.
Ya kisutu.
Ukiona makaburi yanadini mbili tambua hayo ni ya serikali
 
Katika kufanya utafiti wangu binafsi, Nimegundua kuwa Kuna kundi kubwa sana la jamii ambao hawaamini au hawasali katika dhehebu Wala dini yoyote.

Katika kundi hili wapi wengi ambao hulazimika kwenda Makanisani au msikitini kwa sababu moja tu. Sababu kuu ni hofu ya mazishi pindi wanapokufa au kufiwa na wapendwa wao.

Hata Makanisa na misikiti imekua ikitimia kigezo Cha MAZISHI kama njia ya kumkomoa mtu ambaye hajashiriki kikamilifu katik mambo ya dhehebu lake.

Sas ni wakati maalum wa Serikali au watu binafsi kuanzisha Makampuni ya MAZISHI ili kutoa haki kwa Kila mmoja kustiriwa kadri apendavyo.
Mbona jamii inakuzika tu au nako haukubaliki ?
 
Ukienda Msikiti wa Maamur pale Upanga utaona pameandikwa Huduma za Mazishi ni 30,000 ila kama hauna hela ni bure, unapewa Gari ya maiti, facilities za kumsafisha marehemu na mambo mengine. Kifupi kwa waisilamu alichosema mtoa mada hakipo, hatuachi mtu awe mzoga,

Kama mtu sio muisilamu hatutomswalia tu, ila tunamzika.
Kotekote mkuu

Mtoa mada ana shida , itakuwa hashiriki misiba Wala kuchimba makaburi
 
Mi hoja ya mtoa mada nimeielewa, japo na Mimi sijapenda alipotaja na "misikiti", angetaja makanisa tu.

Hoja... Maeneo ya vijiji vyenye wakristo wengi huwa kuna makaburi ya makanisa tu, hakuna makaburi ya serikali (vijiji), sasa mtu asie muumini au aliyetengwa akifa inabidi azikwe nyumbani kwake, au kwao au kwenye vichaka vya matambiko ya machifu, hii so sawa, lazima kuwa na Sheria inayolazimisha kila Kijiji kuwa na eneo la kuzikia wananchi nje ya maeneo ya makanisa

Ikiwezekana kusiwe na maeneo ya makanisa, kuwe na maeneo ya kiserikali tu kwa watu wote
Sijui kijijini kwenu unakotoka kuna hali gani kiuchumi na uwezo wa serikali kujisimamia but nachojua mimi ktk mkoa ninakotokea wilaya zote zina cemetery centers kwa ajili ya wasiokuwa wakazi wa hizo wilaya eg wafanyakazi wa serikali etc na hazimilikiwi na makanisa wazawa tunazikana kwenye mashamba ya familia.

Tatizo ninyi Watanzania wengine mnaiga mambo ya kigeni,kama umezaliwa kijijini unalilia nini kwenda kuzikwa makaburi ya hadhira haya ni kwa ajili ya wageni na hata kama eneo ni la Kanisa haiziuiliwi maiti kuzikwa hapo taratibu zikifuatwa kwa sababu hakuna anaeweza kuikimbia maiti coz mtu akishakufa anakuwa wa jamii nzima.
 
Kwani waislamu mnasilimisha maiti?
Amesema maiti isiyokuwa ya Muislam wanaizika kama wanavyofanya serikali (kama umewahi shuhudia yale mazishi ya municipal kuzika na grader).

Kwa maneno mengine wanatumia utaratibu ule ule wa madhehebu mengine kutoilazimisha maiti kukiri uwepo wa Mungu wao.
 
Katika kufanya utafiti wangu binafsi, Nimegundua kuwa Kuna kundi kubwa sana la jamii ambao hawaamini au hawasali katika dhehebu Wala dini yoyote.

Katika kundi hili wapi wengi ambao hulazimika kwenda Makanisani au msikitini kwa sababu moja tu. Sababu kuu ni hofu ya mazishi pindi wanapokufa au kufiwa na wapendwa wao.

Hata Makanisa na misikiti imekua ikitimia kigezo Cha MAZISHI kama njia ya kumkomoa mtu ambaye hajashiriki kikamilifu katik mambo ya dhehebu lake.

Sas ni wakati maalum wa Serikali au watu binafsi kuanzisha Makampuni ya MAZISHI ili kutoa haki kwa Kila mmoja kustiriwa kadri apendavyo.
Peleka ujinga wako hukohuko kwenu. Misikiti hatuna ujinga wa kubaguwana.

Hivyo vikwazo mnalzimishwa makanisani kwa ajli ya fungu la kumi, hakuna ujinga huo msikitini.
 
Fungu la kumi ni maagizo ya muumini kama sehem ya ibada.
Kwa shetani wanatoa fungu la 60 yaani unakula 40,60 ni za shetani.
Kwa Mungu unakula 90 ,10 ya Mungu
 
Mi hoja ya mtoa mada nimeielewa, japo na Mimi sijapenda alipotaja na "misikiti", angetaja makanisa tu.

Hoja... Maeneo ya vijiji vyenye wakristo wengi huwa kuna makaburi ya makanisa tu, hakuna makaburi ya serikali (vijiji), sasa mtu asie muumini au aliyetengwa akifa inabidi azikwe nyumbani kwake, au kwao au kwenye vichaka vya matambiko ya machifu, hii so sawa, lazima kuwa na Sheria inayolazimisha kila Kijiji kuwa na eneo la kuzikia wananchi nje ya maeneo ya makanisa

Ikiwezekana kusiwe na maeneo ya makanisa, kuwe na maeneo ya kiserikali tu kwa watu wote
Hakika iwe ni sheria na sio utashi wa kikundi fulani eneo maalumu litengwe.
 
Maiti Hana dini Wala ukienda makaburi ya Wakristo au waislamu unyimwi eneo la kuzika.
Isipokuwa taratibu za ibada huwezi pata kama we si mshirika wa dini hizo
 
Waislam hawana mambo mengi, weee ukiwa na msiba nenda msikitini waambie huna uwezo wa kuzika watakufanyia kila kitu mkuu kila la heri.
 
Back
Top Bottom