Waziri Nape: Elon Musk hakuwa na mpango wa kuweka ofisi Tanzania

Nyendo

JF-Expert Member
Jun 4, 2017
1,194
4,112
Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Nape Nnauye amesema mfanyabiashara, Elon Musk hakuwa na mpango wa kuweka ofisi ya Starlink nchini katika hatua yake ya kuwekeza katika utoaji wa huduma ya intaneti kupitia satelite.

Akizungumza na ITV Waziri Nape amesema mpango wa Elon Musk ulikuwa ni kuweka ofisi nchini Marekani hali ameielezea kuwa ingeweza kuleta usumbufu pale ambapo wateja wangehitaji msaada zaidi.

“Kwenye mipango yao walikuwa hawana mpango wa kuweka ofisi hapa, sasa mimi nawauliza ikitokea fault (tatizo) yoyote hawa wateja wenu mnataka waje ofisini kwangu? Wekeni ofisi hapa, mnawekaje ofisi Marekani? Hawa Waswahili mnaowahudumia watapiga simu Marekani walalamike kwamba mbona nimelipa sijapata bando langu, mtaniletea mimi shida,” amehoji.

Aidha, amesema jambo lingine ambalo hawakuorodhesha katika mpango wao ni jinsi gani wataweza kulinda data wanazozikusanya kutoka kwa wateja wao na wapi zinakwenda.

Hivi karibuni kupitia mtandao wa Twitter bilionea Musk alisema anasubiri kibali cha Serikali kuwekeza nchini, lakini Waziri Nape alimjibu kuwa Serikali nayo inasubiri awasilishe nyaraka alizotakiwa kuambatanisha kama sehemu ya maombi.
 
Najua hiyo STARLINK inapigwa vita kisawasawa na VODACOM, TIGO ,HALOTEL AIRTEL na kampuni zote za mitandao maana ndizo zimehodhi soko.
Wairi atueleze manufaa halisi kwa wateja wa StarLink, huduma zao zitawatofautishaje na hawa wezi wa bando.
 
Vodacom wanaofisi Tanzania lakini anaelewa ugumu wa kuwapata customer care unapo kuwa na shida?

Kuna wa vietnam wanamtandao wa kitapeli wa Hallotel ukikwangua vocha yao inakwanguka na namba ukiwapigia wanakwambia nenda duka lao, ko mimi nilipie nauli kufuata vocha ya buku?

Yafaa nini hizo ofisi kama hazitatui matatizo. Mh. Waziri kwa hili hapana sie tunataka huduma ya huyu tajiri wanao subiri ofisi zake wasubiri.

Mh Nape sie vifurushi ghali vya hawa wahuni hatuvimudu tunakuomba kama wewe unapesa ya bando la voda endelea sie tunataka kitu cha mmarekani tafadhari
 
Kwani Nape hajui kama hao Starlink watawasiliana na wateja wao kwa njia ya mtandao?

Hawa jamaa kila siku wanatuambia tuhamie kidigitali, sasa Nape anaturudisha tulipotoka.

Kwani watumiaji wakitaka kuwasiliana na mitandao ya nje huwa wanafanyaje? au hao Starlink hawatakuwa na email address?
 
Basi kama ni hivyo vodacome wafunge matawi yao yote tz warudi south, halotel wafungashe virago warudi china, airtel warudi kwao asia. Wafunge ofice zote halaf uone hizo huduma zitavyokuwa rahisi kupatikana
 
Vodacom wanaofisi Tanzania lakini anaelewa ugumu wa kuwapata customer care unapo kuwa na shida?

Kuna wa vietnam wanamtandao wa kitapeli wa Hallotel ukikwangua vocha yao inakwanguka na namba ukiwapigia wanakwambia nenda duka lao, ko mimi nilipie nauli kufuata vocha ya buku?

Yafaa nini hizo ofisi kama hazitatui matatizo. Mh. Waziri kwa hili hapana sie tunataka huduma ya huyu tajiri wanao subiri ofisi zake wasubiri.

Mh Nape sie vifurushi ghali vya hawa wahuni hatuvimudu tunakuomba kama wewe unapesa ya bando la voda endelea sie tunataka kitu cha mmarekani tafadhari
Siku hizi mitandao yoote ukipata shida let say pesa mtandaoni imekula kwako wala hawajali.

Halotel ndio hamna kabisa.
 
Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Nape Nnauye amesema mfanyabiashara, Elon Musk hakuwa na mpango wa kuweka ofisi ya Starlink nchini katika hatua yake ya kuwekeza katika utoaji wa huduma ya intaneti kupitia satelite.

Akizungumza na ITV Waziri Nape amesema mpango wa Elon Musk ulikuwa ni kuweka ofisi nchini Marekani hali ameielezea kuwa ingeweza kuleta usumbufu pale ambapo wateja wangehitaji msaada zaidi.

“Kwenye mipango yao walikuwa hawana mpango wa kuweka ofisi hapa, sasa mimi nawauliza ikitokea fault (tatizo) yoyote hawa wateja wenu mnataka waje ofisini kwangu? Wekeni ofisi hapa, mnawekaje ofisi Marekani? Hawa Waswahili mnaowahudumia watapiga simu Marekani walalamike kwamba mbona nimelipa sijapata bando langu, mtaniletea mimi shida,” amehoji.

Aidha, amesema jambo lingine ambalo hawakuorodhesha katika mpango wao ni jinsi gani wataweza kulinda data wanazozikusanya kutoka kwa wateja wao na wapi zinakwenda.

Hivi karibuni kupitia mtandao wa Twitter bilionea Musk alisema anasubiri kibali cha Serikali kuwekeza nchini, lakini Waziri Nape alimjibu kuwa Serikali nayo inasubiri awasilishe nyaraka alizotakiwa kuambatanisha kama sehemu ya maombi.
Hivi kuna waziri hapa kweli yaani elon musk ashindwe kuweka ofisi TZ?
 
Basi kama ni hivyo vodacome wafunge matawi yao yote tz warudi south, halotel wafungashe virago warudi china, airtel warudi kwao asia. Wafunge ofice zote halaf uone hizo huduma zitavyokuwa rahisi kupatikana
Hao Vodacom wenyewe kila siku wanatuambia twende kidigitali.. ofisi wanaiweka kwa wazito kubadilika kama wewe wasiojua maana ya dunia ni kijiji, bado mpo mpo kama mbuzi zizini.
 
Tunataka tujue ofisi za Meta (Facebook , whatsaap , Instagram) zipo sehemu Gani ?

Kama hizo hazipo , Ofisi za google (alphabet )je ?

Mi naona Nape anadhani Kila mtu mjinga ndio maana anasema hivyo.
  • Kuna yeyote aliyejibu?
  • Hao mabeberu wakiamua, hizo hadithi za Nape hazitosikika, na Nape anaweza rudi huko Mtama kwa miguu.
  • Ni vyema viongozi wakatoa majibu kwa weledi mkubwa, wakijua kuwa wanawajibu wakubwa zao.
 
Vodacom wanaofisi Tanzania lakini anaelewa ugumu wa kuwapata customer care unapo kuwa na shida?

Kuna wa vietnam wanamtandao wa kitapeli wa Hallotel ukikwangua vocha yao inakwanguka na namba ukiwapigia wanakwambia nenda duka lao, ko mimi nilipie nauli kufuata vocha ya buku?

Yafaa nini hizo ofisi kama hazitatui matatizo. Mh. Waziri kwa hili hapana sie tunataka huduma ya huyu tajiri wanao subiri ofisi zake wasubiri.

Mh Nape sie vifurushi ghali vya hawa wahuni hatuvimudu tunakuomba kama wewe unapesa ya bando la voda endelea sie tunataka kitu cha mmarekani tafadhari
Halotel Ni wezi kuliko wengine wote, vocha zao hazikwanguki
 
Najua hiyo STARLINK inapigwa vita kisawasawa na VODACOM, TIGO ,HALOTEL AIRTEL na kampuni zote za mitandao maana ndizo zimehodhi soko.
Wairi atueleze manufaa halisi kwa wateja wa StarLink, huduma zao zitawatofautishaje na hawa wezi wa bando.
Starlink itakuwa ni game changer kwani yenyewe itatumia Satelite ambayo ni tofauti na zile nyaya za fibre optic na usimamishaji wa mitambo ya simu za mikononi yaani mobile phone masts.

Sasa wategemezi wa minara ambao ni kampuni za simu lazima ziwe na wasiwasi.
 
Back
Top Bottom