Serikali, hiki mnachokifanya hakikubaliki!

Serikali, hiki mnachokifanya hakikubaliki!

Nilikua nazurura huko Fb nikakutana na video moja nadhani Ni huko Isimani kwa mheshimiwa Lukuvi, kiongozi wa CCM anawahutumia wananchi kuhusu umuhimu wa kuwa na Kadi ya CCM na mpango wa CCM kuhakikisha kwamba ifikapo mwezi wa nane kila mtanzania na kila Mwana CCM atakua nakadi ya CCM .

Miongoni mwa Mambo anayoyataja kiongozi huyu wa chama Ni kwamba Kadi ya CCM inakuwezesha kupata huduma muhimu kumi na nne.

Miongoni mwa huduma anazozitaja Ni Kadi hiyo kutumikaa Kama bima ya afya kwa akina mama, kutumika kwa ajili ya huduma za kibenki kwa maana Ni mbadala wa ATM card , kutumika kama kitambulisho cha mifuko ya hifadhi ya jamii.

Kilichonisitikisha sio yeye kuongea maneno hayo , Bali Ni ujinga na umbumbu wa watu waliokua wanamsikiliza, na kumpigia makofi kwa shangwe kabisa na naamini watajitokeza kujiandikisha na kutoa fedha kwa ajili ya kusubiri kadi za CCM kwa ajili ya matumizi katika huduma zaidi ya kumi na nne.

Unaweza kuona kwamba CCM imewanyima wananchi elimu ya uraia na elimu ya kujitambua na kwa maana hiyo wanaweza kusema na kufanya watakalo pasina kuhojiwa na wananchi ambao ni wanachama na walipa Kodi wako.

Kumbe Ni kwamba determination ya chama Ni uchaguzi tu na kubakia madarkani huku wakidelay kuwaletea wananchi maendeleo ya kweli.

Video hiyo inapatikana kwenye ukurasa wa askofu Emausi Bandekile Mwamakula.

Mh Lukuvi imebidi aangalie kwa masononeko na huruma kubwa kwani anajua kabisa huo Ni ulaghai uliopitiliza.
Mtaji wa Ccm ni ujinga wa Watz, na wanautumia vizuri sana.
 
Ni upuuzi na Ulimbukeni kufikiria kati ya Mashirika hayo tajwa ya Kijasusi ulaya na marekani hayana Kinga. Au majasusi wao hawana kinga.
Ni upotoshaji wa hali ya Juu sana.

Atakaye niwekea Jasusi yeyote yule aliyewahi fanya kazi kati ya taasisi hizo za nje, na kuvunja sheria akiwa kazini na akafunguliwa mashitaka ya jinai aweke hapa. TUSIDANGANYANE na uharakati uchwara.
Hujaelewa na hujui ulichokiandika. Ulichokifanya Ni kuleta hisia zako na kuendelea kuifananisha Tanzania na nchi nyingine wakati Ni level tofauti!

Nchi za wenzetu mathalani US viwango vyao vya uadilifu havitilii Shaka Kama vya nchi zinazoendelea.
Askari yoyote au afisa usalama anapofanya makosa hasa ya kijinai lazima akumbane na mkono wa sheria. Ufungaji wao wa Sheri sio wa kulinda viongozi Bali kulinda nchi na wananchi wake.

Muswada huu Ni mahususi kuwalinda watawala na wale wanaofanya kazi chini yao. Kwamba afisa usalama akiua, akiiba akibaka au akifanya tukio lolote asikumbane na mkono wa Sheria iwe za kiraia au za kijeshi wewe unaona sawa.?

Uzuri Ni kwamba watunga Sheria hizi hudhani kwamba wao watabaki kwenye reign milele, zinapokuja kuwagusa wanakua wakwanza kulia Lia!
 
Mkuu samahani labda Mimi nina tongo tongo!
Ninachojua mimi kwenye mchakato wa kutunga Sheria bunge halitungi Sheria bali linajadili muswada wa sheria na kushauri kipi kiongezwe na kipi kipunguzwe!

Wizara husika hukaa na kuona mahitaji ya kisheria katima wizara au Idara husika!
Wataalamu wa sheria wa wizara wanadraft mapendekezo kwa kishirikina na mwanasheria mkuu wa serikali.

Draft husika huwasilishwa kwenye kikao cha Baraza la mawaziri ambapo Rais ndiye mwenyekiti, baada ya Baraza la mawaziri kuijadili na kukubalika juu ya Hiyo Draft inaandikwa Kama Billl of law au muswada wa sheria.

Wakati wa vikao vya Bunge waziri huwasilishwa muswada huo Bungeni ili wabunge waweze kuusikia na kuujadili kwa pamoja huku wakitoa mapendekezo na marekebisho mbalimbali.

Serikali hurudi na kukaa na kupitia mapendekezo yaliyotolewa na wabunge pamoja na wadau wa swala husika.

Baada ya hapo hurudihswa tena bungeni ili kupigiwa kura na kupitishwa ili kuwa Sheria.
Aidha baada ya kupitishwa muswada huo hurudishwa kwa rais ili atie saini kuwa Sheria hiyo imeanza kutumika.
Kwa mujibu wa katiba yetu na mtiririko huo ni dhahiri kwamba sheria au mapendekezo ya Sheria yanaanza na Rais na sio wabunge unless mbunge aje na hoja binafsi katika sheria husika.

Na inapotokea Bunge na serikali wakashindwa kuelewana katika Sheria husika Rais anaweza kulivunja Bunge na tukarejea kwenye uchaguzi!

Kwa Sheria hii iliyoletwa na Waziri Simba chawene Ni Sheria inayoenda kulinda Maslahi ya Viongozi wa CCM ikiwemo Rais wabunge mawaziri na viongozi waandamizi wa serikali ambao kwa nafasi zao wanaweza kuwatumia watu wa usalama wa taifa katika kutimiza majukumu yao au kutimiza matarajio yao kisiasa.

Kufungua kinacholalamikiwa Ni kuwaongezea kinga za kijinai maafisa wa usalama wa taifa au wafanyakazi wa idara ya usalama wa taifa wanapokua wanatimiza majukumu yao.
Swali je Nani anajua mstari wa majukumu ya afisa wa usalama wa taifa kiusalama au binafsi!? Kwamba anaweza kuutwaa uhai wa mtu lakini katika Mazingira ambayo hayana uhusiano na usalama wa taifa lakini sheria itamlinda! (Kinga ya kutishtakiwa) kwa makosa ya kijinai.


Sheria inaenda kubadilishwa kwamba Idara ya usalama wa taifa haitakua Tena chini ya waziri Bali Rais!

Lakini pia kuna kuongezewa kwa kiapo Cha kutunza siri hata baada ya kustaafu au kuacha kazi, kwamba kwakua watakua na Kinga ya kijinai I maana hata makosa ya hovyo watakayofanya kwa kutumiwa na watawala hakuna namna watatoa taarifa kwa vyombo vingine vya dola au serikali nyingine!
Kwahiyo Sheria hii inaonekana kujenga Mazingira ya kuminya wakisoaji wa serikali kwa namna ya tofauti kuliko wakati uliopita!
Ni sheria ya kijinga sn tuikatae
 
Hujaelewa na hujui ulichokiandika. Ulichokifanya Ni kuleta hisia zako na kuendelea kuifananisha Tanzania na nchi nyingine wakati Ni level tofauti!

Nchi za wenzetu mathalani US viwango vyao vya uadilifu havitilii Shaka Kama vya nchi zinazoendelea.
Askari yoyote au afisa usalama anapofanya makosa hasa ya kijinai lazima akumbane na mkono wa sheria. Ufungaji wao wa Sheri sio wa kulinda viongozi Bali kulinda nchi na wananchi wake.

Muswada huu Ni mahususi kuwalinda watawala na wale wanaofanya kazi chini yao. Kwamba afisa usalama akiua, akiiba akibaka au akifanya tukio lolote asikumbane na mkono wa Sheria iwe za kiraia au za kijeshi wewe unaona sawa.?

Uzuri Ni kwamba watunga Sheria hizi hudhani kwamba wao watabaki kwenye reign milele, zinapokuja kuwagusa wanakua wakwanza kulia Lia!
Tena ni sheria ya kipumbafu sn ifutwe na watu wote washitakiwe
 
Hii nchi wananchi wake ni wajinga na hovyo wa kiwango cha lami inakuaje FBI, CIA na m16 watu wao hawana kinga kabisa ila hili li nchi la kimasikini mnataka kuwawekekea kinga kisa ni .... Kwahiyo wasiojukikana bila shaka wanapewa kinga zaidi wa kufanya uovu wao si ndiyo?

Ila shangaa na wewe wananchi hawajajua chochote kuhusu hii sheria mpya hii nchi ya ajabu sana na itaendelea kuwa masikini milele! Umagufulification.

View attachment 2640506
View attachment 2640511View attachment 2640512
Mswada huu umekuja kipindi kibaya. Kwanza ni kipindi ambacho raia wanayo matumaini kuwa nchi yao inakwenda kufanya mabadiliko ya kukuza demokrasia, utawala wa sheria, haki za binadamu, uwajibakaji na uwazi. Pili mswada umeletwa wakati ambapo raia wanaendelea kusubiri majibu ya jinamizi la "watu wasiojulika" ambapo raia wamepotea katika mazingara yenye mwelekeo wa sababu za kisiasa. Pengine kabla ya kuleta mswada huu mamlaka zingejielekeza kwanza kurudisha imani ya raia kwa kutengua kitendawili cha "watu wasiojulikana". Vinginevyo, itakuwa vigumu kuwaaminisha baadhi ya raia kuwa lengo la mswada siyo pamoja na kuwalinda na kutoa kinga kwa matukio hayo ya watu kupotea, kutekwa na kuuawa
 
Atakaye niwekea Jasusi yeyote yule aliyewahi fanya kazi kati ya taasisi hizo za nje, na kuvunja sheria akiwa kazini na akafunguliwa mashitaka ya jinai aweke hapa. TUSIDANGANYANE na uharakati uchwara.
Kasome hii upunguze ujinga:
 
Hapo kuna tatizo...

Hili ni jambo la Samia na kama hakulipenda alikua na uwezo wa kilibadilisha

Mtu anaposema huu ni umagufulification inategemea amesimama ipande upi...

Nijuavyo, muanzilishi wa Magufulification of africa alikua ni Prof Lumumba na maana yake ilikua kuifanya Africa ijikomboe kifikra na ijitegemee kwa kila kitu...

So unaposema mabdiliko ya sheria hii nayo ni magufulification nashindwa kuelewa...

Kwanini tusiseme hili ni la Mheshimiwa Samia?

Au tunahisi yeye hawezi kuamua hayo?
Sasa MAGUFULI alikuwa na wazo gani lakukomboa Africa
 
Hakulipenda kwa namna lilivyokua linatekelezwa kwa utashi wa mtu mmoja na sio swlaa la kimfumo Sasa amelileta kwa njia ya mfumo! No one will ponit finger at her.

Sahihi Sana unaposema MTU anaposem umagufulication inategemea amesimama upande you! Hii inasadifu hulka yake ya Sheria za hati za dharura na intention ya kuwadhibiti wakosoaji wake ili kulinda madaraka take na political popularity!

Kuhusu swala la Africa kujitegemea yenyewe ilikua Ni nadharia tu ya mdomo na sio in practical sense na hakua na Sera zozote za kiuchumi ambazo Ni feasible. Hakuna basis yoyote ya kifikra aliyoijenga kwa waafrica Bali alinstill fear and intimidation hakuna fikra mpya aliyoijenga tofauti na kuwafanya watu wajione wanyonge na yeye kujiona ndio mkombozi.

Mabadiliko ya Sheria hii ni Magufulication kwa sababu he was the founder of Sheria tata. Na Samia anaweza kuamua hayo na a.eamua kwa msingi huo wa Magufulication!
Wafiwa akili zao walikabidhi kwa marehemu uwezo wao wakufiri na kuchanganua mambo ni mdogo sana
 
Kuna afisa wa tiss anataka kuvunja mahusiano yangu na mzazi mwenzangu

Nadhani hii sheria itampa kiburi zaidi lkn nimwambie tu huyo kachero kuwa ALL OPTION ON THE TEBO
Nimroge
Nimpige shoka
Niweke I'd yake mitandaoni
 
Akina Mramba, Yona, Zombe, Mzuzuri, n.k wote walishtakiwa kipindi cha JK
Ila kipindi cha Magufuli , Polisi, Ma DC na Ma RC walikua miungu watu
Wanaweza kumuweka mtu yoyote ndani kwa sababu yoyote na kwa muda wowote, Polisi pia wakapewa kibali cha kuua yoyote na kuteka yoyote

Acheni tu tuseme Mungu fundi
Pia walikuwa rewarded kwa vyeo baada yakuumiza watu
 
Hua una mawazo kama chizi jamaa yangu...

Umeshawahi kumpindua hata jirani yako kabla hujawaza kupindua nchi?
Jamaa anawaza SULUHISHO baada yakuona sanduku la Kura ni usanii... hebu mpe mbinu mBadala kuondokana na hili zimwi
 
Wafiwa akili zao walikabidhi kwa marehemu uwezo wao wakufiri na kuchanganua mambo ni mdogo sana
Hahaha yaani nimecheka na kutafakari kwa pamoja.

Unakuta jitu zima limeenda Shule limefundishwa critical thinking, limenunua smart phone anawesa kuingia mtandaoni kusoma Mambo na kulinganisha Mambo Ila hafanyi hivyo, kwakua Jambo limeletwa na CCM hahoji Wala Nini anawashambulia kwa matusi wanaoonesha tatizo,! Badala aoneshe hata faida anaishia kutukana
 
Nimeona na mpimbafu mwenzako Yeriko Nyerere amesema Magufulification...

How magufulification katika utawala wa Mh Samia?

Mnataka kutwambia mh samia hana uwezo wa kutafakari na kuamua tofauti na kilichopendekezwa?
Aliposema huu utaratibu ni Magufulification, ana maanisha haya mambo ya kuongeza kunga yalianzishwa na Magufuli na sasa Samia anayaendeleza kwa kupeleka kunga kwa maafisa usalama and who knows, baadaye watakuja mawaziri, wakuu wa mikoa, wakuu wa wilaya wakati hao mdiyo waharifu na maadui wakuu wa nchi, then wamekingwa.

Hapo sheria za uharifu zitakuwa ni za kazi gani tena? Labda wana mpango wa kufuta kabisa sheria ya makosa ya jinai nchini
 
Vinginevyo, itakuwa vigumu kuwaaminisha baadhi ya raia kuwa lengo la mswada siyo pamoja na kuwalinda na kutoa kinga kwa matukio hayo ya watu kupotea, kutekwa na kuuawa
Lengo kubwa hasa Ni hili kwa sababu kumekua na kelele kubwa kutaka uchunguzi ufanyike.

Kwa maana hiyo Ni dhahiri kwamba ile regime ya awamu ya Tano ilitumia kikosi maalumu kutoka Idara ya usalama wa taifa ili kudeal na wapinzani wake au wale aliodhani Ni wapinzani wake, au kutekeleza ujambazi wa kidola ambao uliwaangusha wengi kwenye plea bargain! Sheria hii ikishapita ndio habari hizo zinakua zimeisha technically!
 
Sisi bado tunaona shida Raisi kutokushitakiwa halafu mnataka waongeze idadi ya watu ambao hawatashitakuwa mtaani ,hii nafikiri itakuwa ni balaa kubwa uzingatia wabongo wengi SI watu wakuaminika kivile,huu unaweza kutumikia kama mwavuli wa watu kufanya maovu,tujifunze Kwa wenzetu wakenya kulikuwa na taski force waliunda na baadaye iligeuka kama kichaka Cha kufanya uovu,mimi nafikiri ni Bora tubaki na utamadini ambao tumekaa nao Kwa zaidi ya miaka 50 bila mashaka
 
Hahaha yaani nimecheka na kutafakari kwa pamoja.

Unakuta jitu zima limeenda Shule limefundishwa critical thinking, limenunua smart phone anawesa kuingia mtandaoni kusoma Mambo na kulinganisha Mambo Ila hafanyi hivyo, kwakua Jambo limeletwa na CCM hahoji Wala Nini anawashambulia kwa matusi wanaoonesha tatizo,! Badala aoneshe hata faida anaishia kutukana
Miongoni mwa hasara KUBWA aliyotuachia Magu ni hizo za watu kutokuwa na uwezo wakufikiri
 
Back
Top Bottom