Serikali, hiki mnachokifanya hakikubaliki!

Serikali, hiki mnachokifanya hakikubaliki!

Na Bado. Mzee wa watu katuongoza vizuri tu. Figusu, lawama, kukatazwa wizi na ufisadi mkakataa na hata kudiriki kumuombea mabaya. Sasa mnalalamika Nini?! Endeleeni kama TBC runinga na radio kumsifia kama nabii na mtume!😂😂😂🤣🤣🤣
 
Nimeona na mpimbafu mwenzako Yeriko Nyerere amesema Magufulification...

How magufulification katika utawala wa Mh Samia?

Mnataka kutwambia mh samia hana uwezo wa kutafakari na kuamua tofauti na kilichopendekezwa?
Si ndio legacy mzee? Sheria za ajabu ajabu za kuifanya Tanzania iwe kama Korea Kaskazini ni ikiwemo ile ya kulinda viongozi wengine wa serikali ni mambo ya Magufuli
 
mama ameona awahi mapema ili watu wake , wawe salama , ukiangalia yy aliwabuluza kwa mahakama watumishi watiifu kwa mtangulizi wake!! Ha ha ha ha ha . maana kisasi kilikuwa lazima kilipwe.


alert nyingine .ni tukio la juzi . kimasihara na kujifanya king'ang'anizi aka r.ip
 
Kabla yake ni kiongozi gani amewahi kushitakiwa mahakamani?
Akina Mramba, Yona, Zombe, Mzuzuri, n.k wote walishtakiwa kipindi cha JK
Ila kipindi cha Magufuli , Polisi, Ma DC na Ma RC walikua miungu watu
Wanaweza kumuweka mtu yoyote ndani kwa sababu yoyote na kwa muda wowote, Polisi pia wakapewa kibali cha kuua yoyote na kuteka yoyote

Acheni tu tuseme Mungu fundi
 
Akina Mramba, Yona, Zombe, Mzuzuri, n.k wote walishtakiwa kipindi cha JK
Ila kipindi cha Magufuli , Polisi, Ma DC na Ma RC walikua miungu watu
Wanaweza kumuweka mtu yoyote ndani kwa sababu yoyote na kwa muda wowote, Polisi pia wakapewa kibali cha kuua yoyote na kuteka yoyote

Acheni tu tuseme Mungu fundi
si 1-1 lkn. au mechi bado!?
 
Polisi, Ma DC na Ma RC walikua miungu watu
Wanaweza kumuweka mtu yoyote ndani kwa sababu yoyote na kwa muda wowote, Polisi pia wakapewa kibali cha kuua yoyote na kuteka yoyote
Sheria ya wakuu wa wilaya kuweka watu ndani ilitungwa wakati wake?

Sasa hivi imefutwa?

Polisi hawateki na kuua siku hizi?
 
Hapo kuna tatizo...

Hili ni jambo la Samia na kama hakulipenda alikua na uwezo wa kilibadilisha

Mtu anaposema huu ni umagufulification inategemea amesimama ipande upi...

Nijuavyo, muanzilishi wa Magufulification of africa alikua ni Prof Lumumba na maana yake ilikua kuifanya Africa ijikomboe kifikra na ijitegemee kwa kila kitu...

So unaposema mabdiliko ya sheria hii nayo ni magufulification nashindwa kuelewa...

Kwanini tusiseme hili ni la Mheshimiwa Samia?

Au tunahisi yeye hawezi kuamua hayo?
Akili ya sheria za namna hii inafahamika ilikuwa ya Magufuli. Mama Samia naye anapita humo humo, maana kwa sasa CCM haikai madarakani tena kwa ridhaa ya umma, bali hivyo vyombo vya ulinzi na usalama, ikiwemo hao TISS. Sheria mbovu za kujilinda hivi ni baada ya kugundua inabidi michezo michafu itumike ili kuendeleza kubaki madarakani kwa shuruti.

Namna pekee ya sheria za aina hii kuondolewa ni serekali kupinduliwa, ama kutokea machafuko ili kuanza upya kiutawala. Lakini kwa mazingira haya, tutegemee sheria mbaya na hatari zaidi ya hizi.
 
Hakulipenda kwa namna lilivyokua linatekelezwa kwa utashi wa mtu mmoja na sio swlaa la kimfumo Sasa amelileta kwa njia ya mfumo! No one will ponit finger at her.

Sahihi Sana unaposema MTU anaposem umagufulication inategemea amesimama upande you! Hii inasadifu hulka yake ya Sheria za hati za dharura na intention ya kuwadhibiti wakosoaji wake ili kulinda madaraka take na political popularity!

Kuhusu swala la Africa kujitegemea yenyewe ilikua Ni nadharia tu ya mdomo na sio in practical sense na hakua na Sera zozote za kiuchumi ambazo Ni feasible. Hakuna basis yoyote ya kifikra aliyoijenga kwa waafrica Bali alinstill fear and intimidation hakuna fikra mpya aliyoijenga tofauti na kuwafanya watu wajione wanyonge na yeye kujiona ndio mkombozi.

Mabadiliko ya Sheria hii ni Magufulication kwa sababu he was the founder of Sheria tata. Na Samia anaweza kuamua hayo na a.eamua kwa msingi huo wa Magufulication!

Uko sahihi kabisa katika haya maelezo yako.
 
Hii nchi wananchi wake ni wajinga na hovyo wa kiwango cha lami inakuaje FBI, CIA na m16 watu wao hawana kinga kabisa ila hili li nchi la kimasikini mnataka kuwawekekea kinga kisa ni ........kwahiyo wasiojukikana bila shaka wanapewa kinga zaidi wa kufanya uovu wao si ndiyo?

Ila shangaa na wewe wananchi hawajajua chochote kuhusu hii sheria mpya hii nchi ya ajabu sana na itaendelea kuwa masikini milele! Umagufulification

# mods acheni uzi upepe#
Inasikitisha Kwa kweli,hii ndio hasara ya ujamaa wa Mwalimu ndio unatutesa Hadi Sasa..

Kwa staili hii Tunaenda kufugwa kama mifugo.
 
Akili ya sheria za namna hii inafahamika ilikuwa ya Magufuli. Mama Samia naye anapita humo humo, maana kwa sasa CCM haikai madarakani tena kwa ridhaa ya umma, bali hivyo vyombo vya ulinzi na usalama, ikiwemo hao TISS. Sheria mbovu za kujilinda hivi ni baada ya kugundua inabidi michezo michafu itumike ili kuendeleza kubaki madarakani kwa shuruti.

Namna pekee ya sheria za aina hii kuondolewa ni serekali kupinduliwa, ama kutokea machafuko ili kuanza upya kiutawala. Lakini kwa mazingira haya, tutegemee sheria mbaya na hatari zaidi ya hizi.
Hua una mawazo kama chizi jamaa yangu...

Umeshawahi kumpindua hata jirani yako kabla hujawaza kupindua nchi?
 
Sheria ya wakuu wa wilaya kuweka watu ndani ilitungwa wakati wake?

Sasa hivi imefutwa?

Polisi hawateki na kuua siku hizi?

DC kuweka mtu ndani ipo kisheria lakini sio kiholela kama kipindi cha Jiwe
Kuua na kuteka vilikuwa juu zaidi kipindi cha Magufuli kuliko kipindi chochote
 
Hii nchi wananchi wake ni wajinga na hovyo wa kiwango cha lami inakuaje FBI, CIA na m16 watu wao hawana kinga kabisa ila hili li nchi la kimasikini mnataka kuwawekekea kinga kisa ni ........kwahiyo wasiojukikana bila shaka wanapewa kinga zaidi wa kufanya uovu wao si ndiyo?

Ila shangaa na wewe wananchi hawajajua chochote kuhusu hii sheria mpya hii nchi ya ajabu sana na itaendelea kuwa masikini milele! Umagufulification

# mods acheni uzi upepe#
Wewe Nesi nenda katibu watu maswala ya Usalama waachie wenyewe
 
DC kuweka mtu ndani ipo kisheria lakini sio kiholela kama kipindi cha Jiwe
Kuua na kuteka vilikuwa juu zaidi kipindi cha Magufuli kuliko kipindi chochote
Wazanzibar walikua wakimbizi kipindi cha magufuri?

Unajua Lipumba na Slaa walijeruhiwa kipindi gani?

Nani alimuua Mwangosi

Kipigo cha ulimboka na sumu ya mwakiembe?

Vp kuhusu Filikunjombe?

Umeyasahau au hukuwepo?
 
Hakuna mswada wowote wa Sheria Tanzania unakuja kwa Bahati mbaya na Kama nilivyoeleza pale juu, utaratibu wetu wa kutunga Sheria huwa unaanzia kwa Rais then unakuja kwa wananchi

Hii Sheria imekuja mahususi kabisa kwa sababu maalum na sababu kubwa Ni ku-maintai status quo! Na kuwalinda wenye madaraka kwa namna ambayo hautaleta ukakasi!
Wala taharuki kwa jamii, hasa ukizingatia matumizi ya Polisi yamekua na changamoto kubwa Sana kwani wanakosa weledi wa baadhi ya Mambo.
Sasa watu wa system wanaenda kutumika na hata kuruhusiwa kukamata na kuweka kizuizini au hata kuua na kuharibu Mali kwani Sheria inawalinda na watakua chini ya ofisi ya Rais!

Polisi watafanya uchunguzi na wahusika watajulikana Ila litakuja swala la kifungu kinachozuia kumshtaki afisa wa Idara ya usalama wa tafa kwa makosa ya JINAI na madai kali zaidi Ni kifungu kinachozuia afisa huyu kutoa taarifa kwa MTU yeyote ama akiwa kazini au baada ya kustaafu au kuacha kazi kwa namna yoyote ile.
Hapa rais anaongezewa madaraka kuwa mfalme au malkia. Akituma watu wake hakuna wa kuwagusa na yeye mwenyewe haguswi. Ngoja mpate rais chizi ndio mtajua utamu wa sheria hiz. Kwa Magu hakuna aliejifunza, ss subirin
 
Mkuu samahani labda Mimi nina tongo tongo!
Ninachojua mimi kwenye mchakato wa kutunga Sheria bunge halitungi Sheria bali linajadili muswada wa sheria na kushauri kipi kiongezwe na kipi kipunguzwe!

Wizara husika hukaa na kuona mahitaji ya kisheria katima wizara au Idara husika!
Wataalamu wa sheria wa wizara wanadraft mapendekezo kwa kishirikina na mwanasheria mkuu wa serikali.

Draft husika huwasilishwa kwenye kikao cha Baraza la mawaziri ambapo Rais ndiye mwenyekiti, baada ya Baraza la mawaziri kuijadili na kukubalika juu ya Hiyo Draft inaandikwa Kama Billl of law au muswada wa sheria.

Wakati wa vikao vya Bunge waziri huwasilishwa muswada huo Bungeni ili wabunge waweze kuusikia na kuujadili kwa pamoja huku wakitoa mapendekezo na marekebisho mbalimbali.

Serikali hurudi na kukaa na kupitia mapendekezo yaliyotolewa na wabunge pamoja na wadau wa swala husika.

Baada ya hapo hurudihswa tena bungeni ili kupigiwa kura na kupitishwa ili kuwa Sheria.
Aidha baada ya kupitishwa muswada huo hurudishwa kwa rais ili atie saini kuwa Sheria hiyo imeanza kutumika.
Kwa mujibu wa katiba yetu na mtiririko huo ni dhahiri kwamba sheria au mapendekezo ya Sheria yanaanza na Rais na sio wabunge unless mbunge aje na hoja binafsi katika sheria husika.

Na inapotokea Bunge na serikali wakashindwa kuelewana katika Sheria husika Rais anaweza kulivunja Bunge na tukarejea kwenye uchaguzi!

Kwa Sheria hii iliyoletwa na Waziri Simba chawene Ni Sheria inayoenda kulinda Maslahi ya Viongozi wa CCM ikiwemo Rais wabunge mawaziri na viongozi waandamizi wa serikali ambao kwa nafasi zao wanaweza kuwatumia watu wa usalama wa taifa katika kutimiza majukumu yao au kutimiza matarajio yao kisiasa.

Kufungua kinacholalamikiwa Ni kuwaongezea kinga za kijinai maafisa wa usalama wa taifa au wafanyakazi wa idara ya usalama wa taifa wanapokua wanatimiza majukumu yao.
Swali je Nani anajua mstari wa majukumu ya afisa wa usalama wa taifa kiusalama au binafsi!? Kwamba anaweza kuutwaa uhai wa mtu lakini katika Mazingira ambayo hayana uhusiano na usalama wa taifa lakini sheria itamlinda! (Kinga ya kutishtakiwa) kwa makosa ya kijinai.


Sheria inaenda kubadilishwa kwamba Idara ya usalama wa taifa haitakua Tena chini ya waziri Bali Rais!

Lakini pia kuna kuongezewa kwa kiapo Cha kutunza siri hata baada ya kustaafu au kuacha kazi, kwamba kwakua watakua na Kinga ya kijinai I maana hata makosa ya hovyo watakayofanya kwa kutumiwa na watawala hakuna namna watatoa taarifa kwa vyombo vingine vya dola au serikali nyingine!
Kwahiyo Sheria hii inaonekana kujenga Mazingira ya kuminya wakisoaji wa serikali kwa namna ya tofauti kuliko wakati uliopita!
Watawala wa Ccm wanajilimbikizia mamlaka.
 
Hua una mawazo kama chizi jamaa yangu...

Umeshawahi kumpindua hata jirani yako kabla hujawaza kupindua nchi?
Mawazo yake huwezi kuyaita kuwa Ni ya chizi, kikawaida ukiangalia nchi zilizoingia katika machafuko ziliingia kutokana na watu Kama wewe ambao hawataki kuwaambia watawala wanakosea!

Kundi la watu Fulani litafika mahali na kushindwa kuridhika na kuendelea kuvumilia yanayofanywa na watawala. Mara nyingi hii inakua Ni force within! Wale waliodhani Sheria walizojitungia zktawalinda na kuwapa fursa, zinakua Ni Sheria zinazowaumiza, migongano hiyo ya kimaslahi husababisha machafuko katika nchi au hata Mapinduzi!

Ukiangalia kwa makini Idara ya usalama wa taifa inaenda kugeuka jeshi chini ya Rais, haikiwi tena chombo cha kukusanya taarifa kuzichakata na kuishauri serikali kama ilivyo jukumu lake la msingi.
Itahusika katika kazi wanazofanya polisi . Ndio mana wanatunguwa Sheria ya kulindwa dhidi ya mashtaka ya kijinai wakati wakitekeleza majukumu yao ambyo mimi na wewe hatujui mipaka yake!

Majeshi yote yakiyobakia hayana Kinga yankutishtakiwa wakiwaa waatekeleza majukumu yao na kusababishia jinai! Wanashtakiwa kwenye Mahakama za kiraia au za kijeshi!

Itakapofikia mahala wakadai na wao haki na Kinga yankutishtakiwa kama walivyofanya watu wa Idara ya usalama wa taifa na viongozi wa juu wa kisiasa na serikali ujue nchi inaelekea kubaya. Kwahiyo badala yankumtukana mtoa hoja Ni vyema ukapanua uwezo wako wa kufikiri na kuwaza kesho!

Kuna watu wanaitwa wenyeviti wa kamati za ulinzi na usalama ambapo wanausalama wote Wana kazi chini yao (wakuu wa wilaya na mikoa) ambao wanatokana na chama na hawana taaluma ya usalama wa nchi. Watu Hawa watawatumia vibaya mad-so na mar-so kukidhi matakwa yao binafsi na ya kisiasa sababu watakua wanalindwa na Sheria.
 
Back
Top Bottom