Hakika molari ya watu kujiandikisha ipo juu sana, mathalani, nyanda za juu kusini, mbeya, watu wanaenda kupanga foleni ya kujiandikisha ktk BVR saa nne usiku pamoja na balidi kali lililopo sasahv ktk kanda hizo na wakati zoezi hilo huwa linaanza saa mbili kamili hata tatu asbh ya siku nyingine mpaka saa kumi na mbili jioni.
Inavyoelekea kuna uwezekano watu wakapiga kura kwa kutumia kadi za BVR na zile za zamani, maana unakuta mtaa wenye watu karbia 1000 walio na umri wa kujiandikisha, watahitaji siku 20 za kujiandikisha ktk hizi mashine za BVR zenye uwezo wa kuandikisha watu 50 kwa siku, sasa hizo mashine zipo kwa siku saba tu kwa kila mtaa ambayo ni sawa na kuandikisha watu 350 ambao ni sawa na asilimia 35 ya hao watu.