Serikali haina uwezo kuajiri walimu vyuo vikuu au sio kipaumbele?

maroon7

JF-Expert Member
Nov 3, 2010
11,144
15,144
Katika kitu kinashangaza ni hili la vyuo vya umma vya elimu ya juu kuwa na upungufu mkubwa mno wa waalimu. Yaani kitu ninachojiuliza ni kwamba serikali haina uwezo kuajiri kuziba huu upungufu mkubwa wa waalimu au ni kwamba sio kipaumbele chao. Inashangaza zinatolewa ajira za walimu wa sekondari na msingi tu halafu huku juu ambako ndio wataalamu wanatengenezwa hakuna waalimu,na bila aibu naibu spika anatoa kauli ya kwamba waliostaafu warudishwe huku wakijua kwa uhaba uliopo hata wastaafu hawawezi kuziba pengo ipasavyo. Isitoshe vijana wanatakiwa kuanza kuandaliwa mapema ili waje kuwa wasomi wabobezi kama hawa wastaafu tunaowang'ang'ania huku tukijua vijana wetu hawana ajira. Kauli ya leo pia ya mbunge kule mwanza kwenye mkutano wa Rais Samia na vijana inaonesha jinsi gani mzaha ulivyo mkubwa kwenye kuandaa kizazi kijacho cha wataalam. Chuo kikuu cha mkwawa nao wametoa nafasi nyingi za kuomba waalimu wanaotaka kuhamia chuoni hapo ili kuziba mapengo,bila kujali sehemu nyingine linatengenezwa pengo jingine maana vibali vya serikali kuajiri waalimu vyuo vikuu havijatoka miaka mingi sio UDSM, DIT,SUA etc, vyuo vingi kwa sasa vimejaza waalimu wa part time wastaafu na wengine wanaosubiri kuajiriwa. Hili ni bomu kwa elimu yetu ni suala la muda tu tutakuja kujuta graduates wetu ni vilaza.
 
Chuo Kikuu muhimu BOOM tu, mengine ni porojo tu… notisi za kudanilodi kutoka lecture za Ulaya!
 
Tafadhali sana weka vituo na paragraphs.
 
Back
Top Bottom