Serikali fungueni mipaka wakulima wauze wenyewe mahindi, NFRA inawanufaisha wachache

ndenjii handsome

JF-Expert Member
Apr 27, 2021
647
704
Baada ya kusikia serikali imetoa bilioni 50 kwa ajili ya manunuzi ya mahindi.

Nikaona huu ndio wakati muafaka wa kuuza nikajaza howo zangu tatu mzigo kupeleka kwenye kitengo.

Dah nilichokutana nacho tajiri atabaki kuwa tajiri nae maskini atazidi kuwa maskini hasa kwenye nchi zetu za Kiafrika.

Kiufupi mkulima mdogo hauzi wanaopewa kipaombele mwenye junia kuanzia mia nashukuru nilibeba tu gunia 412 nikajiuzia si unajua ukiwa na jina hapa nchini.

Sikuwa mbinafsi nikamfuata mkulima mdogo aliebeba gunia 30 nikaanza piganae stori akaniambia anasiku ya nne na kila akitaka uza vikwanzo kibao mara maind machafu.

Mara punje ndogo kiujumla ni vikwazo tu ambavyo havina msingi

Nikarudi kwa katajili kenzangu ambako nako kalileta maindi akaniambia kaka huu ndio muda wa kupiga pesa.

Akiwa na maana anaenda walalia wakulima wadogo kwa kilo 260 unapeleka kwenye kitengo 500.

Sikujibu kitu nilichokifanya nikaenda kwa yule mkulima nikamkusanya na wenzake nikaenda wauzia asee walinishukuru.

Tuludi kwenye mada
Kwenu watu wa serikali nimewapa hiyi stoli ili mjionee hela mliyotoa haina msaada wala tija na mpate pakuanzia

Ila kama haya yana mkono wenu endeleen kuwaumiza wananchi kwa ufinyu wa akili zenu

Mngekuwa mnataka kumsaidia mwananchi haya tusingeyaona

Ila ipo siku yenu na mm ndio yule mtu aliekuwa akisubiliwa najua hamuwez kuelewa wala kusikia wala kuambiwa
Muda unakujaa

Asante
 
kwnya ukame mkubwa sana hadi ngombe wamekufa..kwanini mahindi hayanunuliwi
 
Ndugu wangu wacha kudanganyika.

Hakuna uhitaji wa mahindi kutoka tanzania.

Uganda kenya nk mahindi wanayo mengi.
nao wanalinda mahindi yanayozalishwa kwao kwanza.

Jaman mvua hii haikunyesha kwenu tu bali na kwao

Mipaka mnaisingizia.ipo free.
hata wewe leo peleka mahindi yako popote mradi tu mamlaka za huko uendako zijiridhishe huna covid

Mkumbuke pia Mamlaka za ugenini zipo too strict na covid pengne unnecessarily.

wewe beba nafaka zako jipelekee.
 
Ukiritimba mkubwa,

Serikali fuatilieni sasa kinachoendelea ni maajabu matupu, kweli nitoke kijijini na mzigo wangu, halafu muanze kusema niandike kwanza barua ya kuomba kuuza mahindi, bado ili barua ipitishwe lazima nitoe rushwa kwa hali hii hatufiki.

Yaani nilime mimi halafu niombe kuuza kwa barua, vikwazo sasa havihesabiki mara punje ndogo, sio meupe wakati nimeyasafisha vizuri hii sio haki kama hamtaki kununua ni afadhali mkasema ili ijulikane wazi.
 
Poleni wakulima wa Mahindi wa Tanzania.

Mwaka huu nasikia kuna makampuni yananunua Soya kupeleka katika Soko la China.

Ulizieni hayo makampuni yanapatikana wapi ili mlime soya na kuyauzia.

Mimi nilishaachana na biashara ya Mahindi.

Kitambo sana.

Biashara ya kuteseka kulima bila kujua unauza wapi.
 
Poleni wakulima wa Mahindi wa Tanzania.

Mwaka huu nasikia kuna makampuni yananunua Soya kupeleka katika Soko la China.

Ulizieni hayo makampuni yanapatikana wapi ili mlime soya na kuyauzia.

Mimi nilishaachana na biashara ya Mahindi.

Kitambo sana.

Biashara ya kuteseka kulima bila kujua unauza wapi.

Ni maajabu kulima nilime mimi bila ruzuku yoyote halafu mimi huyohuyo niandike barua ya maombi ili kuuza mazao yangu utahisi nimeiba bana hapana
 
Ni maajabu kulima nilime mimi bila ruzuku yoyote halafu mimi huyohuyo niandike barua ya maombi ili kuuza mazao yangu utahisi nimeiba bana hapana
Ujue hakuna mnunuzi hapo. Serikali kwa miaka mingi imeshindwa kutafuta soko la mahindi na haisemi.

Wakulima hebu tafuteni zao mtakaloweza kuuza.

Kuliko kupoteza nguvu zenu bila uhakika wa soko.

Kuna aina ya maharage yanauzika kidogo katika soko la ndani.

Hebu fanyeni utafiti miyalime kama nilivyowashauri kwenye zao la Soya hapo juu.

Nawapenda sana wakulima, wanatulisha na mwisho sa siku wanabaki bila maendeleo.
 
Back
Top Bottom