Serikali yashindwa kununua mahindi kwa wakulima Ruvuma

Serikali yashindwa kununua mahindi kwa wakulima Ruvuma

DR. MWAKABANJE

JF-Expert Member
Joined
Nov 7, 2012
Posts
1,986
Reaction score
3,151
Ikiwa wakulima wa mahindi mkoa wa Ruvuma bado hawajasahau machungu ya mfumo mbovu wa serikali wa ununuzi wa mahindi kwa kutumia mawakala kwa msimu wa mwaka jana, ambao kimsingi uliwanufaisha mawakala huku wakulima wakishindwa kuuza mahindi yao na kwa walio bahatika kuuza ni kwa kiwango kidogo sana (binafsi niliuza gunia 7 serikali na kati ya 100) nilizokuwa nazo.

Mwaka huu, pamoja na pigo lingine walilopata wakulima la kupungua kwa uzalishaji wa mahindi kutokana na zao hilo kushambuliwa na wadudu hasa panya katika hatua za mwanzo, bado soko lake limeendelea kuwa gumu kwani hadi sasa Serikali kupitia NFRA ipo kimya huku mkulima akizidi yumba kiuchumi tangu mwaka jana.
 
Mkiambiwa badilikeni hamsikii,ushabiki mwingi kwa rangi za mbogamboga!mtaendelea kwa mtindo huu?umaskini utaisha?
 
tafuteni masoko sehemu nyingine,pesa yote ipo kwenye kampeni za maccm!
 
Endeleeni kukichagua chama cha wakopaji .....mtalipwa 2020......shauri yenu
 
Back
Top Bottom