Serikali Dar es Salaam yafuatilia kuchanwa mabango ya CCM | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Serikali Dar es Salaam yafuatilia kuchanwa mabango ya CCM

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Safari_ni_Safari, Aug 24, 2010.

 1. Safari_ni_Safari

  Safari_ni_Safari JF-Expert Member

  #1
  Aug 24, 2010
  Joined: Oct 5, 2007
  Messages: 22,451
  Likes Received: 5,842
  Trophy Points: 280
  PICHA za mgombea wa urais kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM) zilizobandikwa katika eneo baadhi ya maeneo zimechanwa na watu wasiojulikana hali ambayo ofisi ya Mkuu wa Mkoa imesema inafuatilia kubaini wanaofanya vitendo hivyo.

  Eneo ambalo gazeti hili limeshuhudia picha hizo zikiwa zimechanwa ni katika chuo cha teknolojia Dar es Salaam.

  Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, William Lukuvi alisema, "tutalifanyia kazi suala hilo na ngoja tuanze kulishughulikia kwa kuwa lipo ndani ya mkoa wangu ina maana lipo chini yangu pia," alisema Lukuvi.


  Gazeti hili lilipita katika maeneo hayo na kushuhudia picha za mgombea huyo zilizobandikwa katika mabati na kuta zilizozunguka eneo hilo zikiwa zimechanwa hali iliyoleta maswali mengi kwa watu wengine waliokatisha katika eneo hilo.


  Wakizungumza na gazeti hili baadhi ya watu hao ambao hata hivyo hawakupenda majina yao yaandikwe gazetini walisema kinachotakiwa kufanywa kwa sasa ni kwa mamlaka zinazohusika kuwatafuta waliofanyakitendo hicho ili wafunguliwe mashitaka.

  Katibu Mkuu wa CCM, Yusuf Makamba alipozungumza na gazeti hili, alisema, "kwa sasa siwezi kusema neno lolote kwa kuwa si mhusika wa mkoa huu, ingekuwa hapo zamani wakati huo mkoa unatambulika kama mkoa wa Mmakamba ningeweza kulisemea suala hilo," aliongeza katibu huyo.


  Maoni
  Acheni hizo na nyie bwana mambo ya CCM yaenze kutumia fedha za serikali kuyashughulikia. CCM watafute namna yao watakayoweza kuyalinda mabango yao. Kama zingechanwa za chadema au CUF serikali ingezishughulikia? Mambo ya nchi ndo yanaponichoshaga hapo.
   
 2. Shapu

  Shapu JF-Expert Member

  #2
  Aug 24, 2010
  Joined: Jan 17, 2008
  Messages: 1,896
  Likes Received: 174
  Trophy Points: 160
  Hiyo "Thanks" yangu nimekugongea ni kwa ajili ya yale maoni yako ya font nyekundu.
   
 3. Zogwale

  Zogwale JF-Expert Member

  #3
  Aug 24, 2010
  Joined: Jul 10, 2008
  Messages: 11,613
  Likes Received: 825
  Trophy Points: 280
  Hizo ndizo kampeni, Bwana, nani kakuambia wana chuo wote wanamuunga mkoni jamaa!!! Msilazimishe watu, acha watu waamue wenyewe. Watashughulikia wangapi wakati najua zitachanwa nyingi tuu? Haya ni mambo pet pet sana!! Shughulikieni ya maana!! Kwanza hayo mabilioni ya kampeni yangesaidia sekta ya afya, elimu, kilimo, you name all!!
   
 4. Safari_ni_Safari

  Safari_ni_Safari JF-Expert Member

  #4
  Aug 24, 2010
  Joined: Oct 5, 2007
  Messages: 22,451
  Likes Received: 5,842
  Trophy Points: 280
  Huyu Makamba muppet kweli....yaani mali yako inaharibiwa unasema wewe huhusiki au anathibitisha kuwa ni kweli ikulu imelipia hayo mabango kwa yule mdosi wa Canada?

  Lukuvi ni muppetx2...anakurupuka tu hili si swala ala kipolisi zaidi....Makamba anatakiwa kushitaki Polisi ili waanze kulifanyia kazi...hii kutu itawatoka lini hawa watu kuwa CCM na serikali ni vitu tofauti kimaslahi??...Argh kamatakamata itaanza na as usual innocents ndio wataumia
   
 5. Ndibalema

  Ndibalema JF-Expert Member

  #5
  Aug 24, 2010
  Joined: Apr 26, 2008
  Messages: 10,916
  Likes Received: 131
  Trophy Points: 160
  Damu ni nzito ndungu zangu.
  Luvuvi ni Mbuge wa CCM, ameteuliwa pia kuwa mkuu wa mkoa ambaye pia ni Mwenyekiti wa Baraza la ulinzi na Usalama wa Jiji la Dar.
  Alipe fadhila gani tena kwa CCM??
   
 6. Fidel80

  Fidel80 JF-Expert Member

  #6
  Aug 24, 2010
  Joined: May 3, 2008
  Messages: 21,976
  Likes Received: 104
  Trophy Points: 145
  Kama mgombea wa CCM anakubalika kwa nini wametandaza mabango kila kona mpaka yamekuwa uchafu.
  Nimeamini kizuri cha jiuza kibaya cha jitembeza.
   
 7. Safari_ni_Safari

  Safari_ni_Safari JF-Expert Member

  #7
  Aug 24, 2010
  Joined: Oct 5, 2007
  Messages: 22,451
  Likes Received: 5,842
  Trophy Points: 280
  Sasa anafanya kazi kupitia magazeti?....Mwenye mali (Makamba) hajui uharibifu huu...yeye Lukuvi atachomaamafuta toka Ilala Boma mpaka DIT kwa kodi zetu?.....Mbona Ngwasuma na Akudo wanachaniana hayo mabango kila siku na yeye hafuatilii?...AISEE... AM VERY ANGRY UNAJUA!!!!!!:mad2::mad2:
   
 8. Mkosoaji

  Mkosoaji JF-Expert Member

  #8
  Aug 24, 2010
  Joined: Aug 24, 2009
  Messages: 363
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  Na mimi pia. Ombwe la uongozi kweli lipo.

  Nimeamini ule msemo wa 'Chama kushika hatamu na serikali kuwa mtekelezaji' bado upo hai.
   
 9. G

  GEOMO Senior Member

  #9
  Aug 24, 2010
  Joined: Jul 11, 2009
  Messages: 102
  Likes Received: 14
  Trophy Points: 35
  Sasa uwanja sawa wa kiushindani ktk siasa uko wapi? Ya chadema na vyama vingine yanalindwa na nani? Nadhani pia hata Aliyeyachana namuunga mkono yanarundikwa mpaka unakuwa uchafu! Kituo kizima kinajazwa bango la aina moja lenye ujumbe huohuo. Mbona jiji wanangoa matangazo ya biashara ya watu wengi tu ambao wanaleseni za biashara na wanalipa kodi. Vp c c m wanayalipia hayo mabango yanayobandikwa kwenye kuta za majengo na vituoni?
   
 10. MANI

  MANI Platinum Member

  #10
  Aug 24, 2010
  Joined: Feb 22, 2010
  Messages: 6,409
  Likes Received: 1,861
  Trophy Points: 280
  Hizo ni salamu tu angoje 31/10/2010 labda wachakachue kura.
   
 11. Safari_ni_Safari

  Safari_ni_Safari JF-Expert Member

  #11
  Aug 24, 2010
  Joined: Oct 5, 2007
  Messages: 22,451
  Likes Received: 5,842
  Trophy Points: 280
  Next to come KOVA......akiwa keshakamata watuhumiwa
   
 12. Ngambo Ngali

  Ngambo Ngali JF-Expert Member

  #12
  Aug 24, 2010
  Joined: Apr 17, 2009
  Messages: 3,194
  Likes Received: 134
  Trophy Points: 160
  Nasikia Manispaa za Dar Es Salaam zilipitisha sheria kuwa kubandika posters katika kuta za nyumba ni kosa la jinai. Anachoshughulikia Lukuvi ni kipi waliondoa hizo posters au waliobandua.

  Kama kweli hiyo sheria ipo naona waliofanya kosa ni wale waliobandika na wala sio waliondoa.

  Hebu tulijadili hilo
   
 13. Zak Malang

  Zak Malang JF-Expert Member

  #13
  Aug 24, 2010
  Joined: Dec 30, 2008
  Messages: 5,410
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 0
  Mrema (wa TLP) last week alilalamika mabango yake yamen'golewa huko Vunjo na watu anaoamini ni wafuasi wa CCM. Jee waliofuatilia suala hili, Polisi walichukua hatua gani?
   
 14. Zak Malang

  Zak Malang JF-Expert Member

  #14
  Aug 24, 2010
  Joined: Dec 30, 2008
  Messages: 5,410
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 0
  Kosa kwa wengine woote - lakini siyo kwa CCM!
   
 15. The Finest

  The Finest JF-Expert Member

  #15
  Aug 24, 2010
  Joined: Jul 14, 2010
  Messages: 21,709
  Likes Received: 43
  Trophy Points: 145
  Aisee nimekugongea thanks kwa ajili ya huo usemi kwenye red hapo
   
 16. M

  MJM JF-Expert Member

  #16
  Aug 24, 2010
  Joined: Mar 30, 2010
  Messages: 461
  Likes Received: 20
  Trophy Points: 35
  Kinachonichosha ni yule aliyekuwa Rais kutofahamika licha tu ya Tanzania nzima bali hata eneo lisilozidi kilometre tatu kutoka Ikulu. Wanaanza kukimbizana mitaani na watu wanaotoa mabango. Hayana jipya hayo. Kwani wanachuo hawajui sera zenu kandamizi kwa watoto wa maskini wanaosoma elimu ya juu.

  Tumieni mabavu yenu haitawasaidia sana. Usitegemee mabango yenu yapendwe na wahanga wa utawala wenu. Sawa na kubandika picha ya Osama msikitini hiyo
   
 17. M

  MJM JF-Expert Member

  #17
  Aug 24, 2010
  Joined: Mar 30, 2010
  Messages: 461
  Likes Received: 20
  Trophy Points: 35
  Kinachonichosha ni yule aliyekuwa Rais kutofahamika licha tu ya Tanzania nzima bali hata eneo lisilozidi kilometre tatu kutoka Ikulu. Wanaanza kukimbizana mitaani na watu wanaotoa mabango. Hayana jipya hayo. Kwani wanachuo hawajui sera zenu kandamizi kwa watoto wa maskini wanaosoma elimu ya juu.

  Tumieni mabavu yenu haitawasaidia sana. Usitegemee mabango yenu yapendwe na wahanga wa utawala wenu. Sawa na kubandika picha ya Osama msikitini ubalozi wa marekani hiyo
   
 18. The Finest

  The Finest JF-Expert Member

  #18
  Aug 24, 2010
  Joined: Jul 14, 2010
  Messages: 21,709
  Likes Received: 43
  Trophy Points: 145
  Hapo kwenye red natumaini ikitokea kwa vyama vingine watafanya hivyo hivyo pia
   
 19. Safari_ni_Safari

  Safari_ni_Safari JF-Expert Member

  #19
  Aug 24, 2010
  Joined: Oct 5, 2007
  Messages: 22,451
  Likes Received: 5,842
  Trophy Points: 280
  Sijui mvua ikiyanyeshea na vile ni ya China watamkamata mungu....
   
 20. The Finest

  The Finest JF-Expert Member

  #20
  Aug 24, 2010
  Joined: Jul 14, 2010
  Messages: 21,709
  Likes Received: 43
  Trophy Points: 145
  Natumaini muda si mrefu utasikia Kova naye ameita press conference na waandishi wa habari kwa ajili ya hili suala ! Phew
   
Loading...