The Finest
JF-Expert Member
- Jul 14, 2010
- 21,605
- 6,071
Sijui mvua ikiyanyeshea na vile ni ya China watamkamata mungu....
ound:ound:ound:ound:
Sijui mvua ikiyanyeshea na vile ni ya China watamkamata mungu....
Kwa maoni hayo umesema jambo la maana maana ni ukweli ulio wazi.PICHA za mgombea wa urais kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM) zilizobandikwa katika eneo baadhi ya maeneo zimechanwa na watu wasiojulikana hali ambayo ofisi ya Mkuu wa Mkoa imesema inafuatilia kubaini wanaofanya vitendo hivyo.
Eneo ambalo gazeti hili limeshuhudia picha hizo zikiwa zimechanwa ni katika chuo cha teknolojia Dar es Salaam.
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, William Lukuvi alisema, tutalifanyia kazi suala hilo na ngoja tuanze kulishughulikia kwa kuwa lipo ndani ya mkoa wangu ina maana lipo chini yangu pia, alisema Lukuvi.
Gazeti hili lilipita katika maeneo hayo na kushuhudia picha za mgombea huyo zilizobandikwa katika mabati na kuta zilizozunguka eneo hilo zikiwa zimechanwa hali iliyoleta maswali mengi kwa watu wengine waliokatisha katika eneo hilo.
Wakizungumza na gazeti hili baadhi ya watu hao ambao hata hivyo hawakupenda majina yao yaandikwe gazetini walisema kinachotakiwa kufanywa kwa sasa ni kwa mamlaka zinazohusika kuwatafuta waliofanyakitendo hicho ili wafunguliwe mashitaka.
Katibu Mkuu wa CCM, Yusuf Makamba alipozungumza na gazeti hili, alisema, kwa sasa siwezi kusema neno lolote kwa kuwa si mhusika wa mkoa huu, ingekuwa hapo zamani wakati huo mkoa unatambulika kama mkoa wa Mmakamba ningeweza kulisemea suala hilo, aliongeza katibu huyo.
Maoni
Acheni hizo na nyie bwana mambo ya CCM yaenze kutumia fedha za serikali kuyashughulikia. CCM watafute namna yao watakayoweza kuyalinda mabango yao. Kama zingechanwa za chadema au CUF serikali ingezishughulikia? Mambo ya nchi ndo yanaponichoshaga hapo.
Nakumbuka mwaka 2005 Chadema ilibandika posters nchi nzima zenye portraits za Freeman Mbowe (mgombea urais wa chama hicho) zikimuonyesha Mbowe akiwa mbele ya bendera ya taifa (siyo bendera ya Chadema). Lewis Makame wa Tume ya uchaguzi (NEC) alikuja juu na kusema kufanya hivyo ni kwenda kinyume cha kanuni za kampeni!
Makame alishangaza wengi! Kukataza bendera ya taifa ambayo daima nu kitu cha kuonyesha mshikamano wa wananchi pamoja na tofauti zao za kisiasa?
Kule Marekani,mwaka 2008 kampeni za vyama vyote viwili Democrat na Republican walikuwa wanapeperusha bendera za taifa. Kulke Lebanon, wakati wa mikutano wafuasi wa vyama vya siasa wamepgwa marufuku kubeba bendera za vyama, isipokuwa zile za taifa tu!!!!
Lakini baadaye Makame aliona kosa lake na hakufuatilia. Lakini inaonyesha jinsi mtu huyu alivy na reflex action katika dosari zote azionazo katika vyama vya upinzani, kuliko zile za chama tawala, kilichomuweka pale.
aliamriwa na mukapa...
Upinzani sio kuwa na tabia ya kihuni.
Upinzani sio kuwa na tabia ya kihuni.
Ni kosa la jinai kuharibu mabango ya kampeni; haijalishi ni ya chama au mgombea gani.