Mchambuzi ha ha haa! kuna njia iliwahi kutumiwa na mbunge moja huko Kenya katika kuhakikisha kuwa mpinzani wake gets the message lakini sidhani kama inaweza kutumika mtandaoni. Hawa watu ni wasanii na kama ilivyo kwa wasanii siku zote, muda utafika na itabidi ama wazinduke au waachwe kwenye mataa na ulaghai wao! Hata huko ndani ya BMLK tayari watu wanaanza kujikuta face to face with reality kwamba hakuna namna ya kuboresha muundo wa serikali mbili bila kwanza kuhakikisha yapo mamlaka yatakayoshughulikia tu mambo ya Tanzania bara (Tanganyika) na humo hawatakiwi wasio wa Tanganyika na hivyo hivyo kwa Tanzania visiwani (Zanzibar).
Na maswali nilowauliza mimi je mbona hamyazungumzii? tatizo lenu hamjui kujadili hata kidogo kila swala ni la Mkandara wakati tunajadili hoja zilizopo mbele yetu. sasa kama wewe hufahamu nini mfuko wa pamoja na kwa ajili gani tunajadili kitu gani maana hata nikikueleza hutaelewa maana hukuelewa toka mwanzo. Na wala sio swala la kuepa isipokuwa ni kufahamu kwamba nazungumza na kipofu juu ya ukubwa wa tembo.
Mkuu sio kweli kabisa ya kwamba hatuwezi kujibu mfuko wa pamoja unawahusu nchi gani, nadhani niliwahi kueleza huko nyuma ya kwamba Mfuko wa pamoja ni sawa kabisa na hesabu unaweza tumika ktk muundo wowote wa serikali iwe hata 1 maana hadi sasa kila mkoa unachangia mfuko wa Tanganyika na inajulikana kila mkoa makusanyo yake. Na serikali 2 au 3 ni swala la kusema 1+8= 9 ama 9-1 kinachobakia ni nini.Mchambuzi ha ha haa! kuna njia iliwahi kutumiwa na mbunge moja huko Kenya katika kuhakikisha kuwa mpinzani wake gets the message lakini sidhani kama inaweza kutumika mtandaoni. Hawa watu ni wasanii na kama ilivyo kwa wasanii siku zote, muda utafika na itabidi ama wazinduke au waachwe kwenye mataa na ulaghai wao! Hata huko ndani ya BMLK tayari watu wanaanza kujikuta face to face with reality kwamba hakuna namna ya kuboresha muundo wa serikali mbili bila kwanza kuhakikisha yapo mamlaka yatakayoshughulikia tu mambo ya Tanzania bara (Tanganyika) na humo hawatakiwi wasio wa Tanganyika na hivyo hivyo kwa Tanzania visiwani (Zanzibar).
Eti inapendekezwa bunge moja yenye sehemu tatu ambazo ni Bunge la Muungano kwa masuala ya muungano na humo humo linakuwa na sehemu mbili ambazo ni wabunge wa Zanzibar kwa ajili ya masuala ya Wazanzibari na sehemu ya Tanganyika kwa ajili ya mambo ya bara. Hata hivyo kulingana na ripoti kutoka vyanzo mbalimbali neno tatu tayari linazua kiwewe kwani wajumbe wanachama wa CCM wanaona kama vile hiyo ni sawa na kula matapishi yao kwani unashabihiana na muundo wa muungano wa serikali tatu ambao ulipendekezwa na Tume ya Mabadiliko ya Katiba! Na hapo bado maswala ya Mahakama, Mamlaka ya Raisi na mengineyo...kweli mbio za sakafuni huishia ukingoni.
Mkandara na Kobello hawathubutu kujibu swali la mfuko wa pamoja kwa sababu jibu lolote lile watakalolitoa lina maana ya kuundwa kwa mamlaka tatu ya washiriki kwa pamoja (Tanzania) na washiriki binafsi (Tanganyika na Zanzibar)! Watakimbia, watarukaruka lakini mwisho wa siku watakuta hawana pa kutokea, Tume ilishafanya kazi yake kwa weledi na kuziba mianya yote ya kutokea. Kulingana na rasimu kila jimbo Zanzibar litakuwa na mwakilishi moja tu badala ya wawili kama sasa na ni huyo huyo ataiwakilisha Zanzibar kwenye kikao cha Bunge la Muungano na Bunge la Zanzibar. Hata hii peke yake itapunguza gharama zisizo lazima kwa kiasi fulani.
Mkandara,Na maswali nilowauliza mimi je mbona hamyazungumzii? tatizo lenu hamjui kujadili hata kidogo kila swala ni la Mkandara wakati tunajadili hoja zilizopo mbele yetu. sasa kama wewe hufahamu nini mfuko wa pamoja na kwa ajili gani tunajadili kitu gani maana hata nikikueleza hutaelewa maana hukuelewa toka mwanzo. Na wala sio swala la kuepa isipokuwa ni kufahamu kwamba nazungumza na kipofu juu ya ukubwa wa tembo.
Hii yanionyesha kumbe muda wote napoteza muda kujadili na watu ambao hawajui tunachokijadili isipokuwa wanabisha tu ili mradi wanaunga mkono Ukawa. Well, kwanza someni nini maana ya mfuko wa pamoja muelewe kazi yake kisha tutaendelea kujadili hizi tofauti za serikali 2 au 3 maana ni upuuzi mtupu kujadili hili ikiwa mtu haelewi serikali ya Muungano inahitaji mfuko wa pamoja!
Haya umeruka toka tulipokuwa na kuingia sehemu nyingineyo.. kama unataka tujadili kichwa cha mada yangu karibu na nitakuwa radhi kuendelea na mjadala huo niwe objective vipi zaidi ya kuelezea jinsi ya kutatua mapungufu na kero zetu?. Usiruke ruke unapojiona umebanwa.Mkandara,
Unazidi kufilisika kihoja, kwanza hadi sasa kichwa cha uzi wako hakibebi hoja yoyote ya maana juu ya gharama za serikali Tatu kwa mwananchi from an economic and statistical perspective, badala yake ni porojo za kisiasa tu na Imani ambazo ni utopian. Pili, haupo objective Bali subjective and very emotional hasa kuhusiana na suala la Zanzibar; kwa maana nyingine, una double standards, mengine kwa znZ sawa, kwa Tanganyika sio sawa. Umeshindwa Kabisa kuelewa Kwamba bila ya Tanganyika, mamlaka kamili ya znZ hayapo kwani ukamili wa Zanzibar ni wa pembe Tatu zikijumuishwa Tanganyika na muungano Kama serikali. Kutokana na mapungufu yako kihoja nika kusaidia na a framework of analysis kuhusiana na joint.finance commission na kukuuliza maswali specifically dirccted to you. Ukakwepa kwepa lakini tumekubana, na sasa unasema Kwamba mjadala ni wa wote. Hakuna aliyekataa Hilo, lakini Kama mwanzisha mjadala, maswali ya msingi una wajibu wa kujadili, sio kuomba msaada au kukwepa kijanja janja tu.
Hapo juu Mag3 kajadili suala la msingi sana kuhusiana na Mapato, matumizi na mchango wa muungano. Kama kawaida yako umekuja na hoja nyepesi nyepesi sana Kwamba haijalishi serikali Zipo Ngapi, mfuko wa pamoja ni mfuko wa pamoja, na Ukatoa mfano Kwamba Tanzania kuna mikoa mingi lakini michango yake Inaenda kwenye kapu moja. Hapo awali nilikuuliza huu mfuko wa pamoja ni baina ya Nani na Nani? Umekimbia swali. Sasa unapojadili Kwamba mikoa inachangia Mfumo mmoja, kwa vile hauna umakini Katika hoja zako, unasahau Kwamba mfuko wa serikali kuu unaotokana na michango ya mikoa na local government authorities, wachangiaji wake wanajulikana kwa:
1. Idadi Yao
2. majina Yao
3. Kiasi wanachochangia.
Kwa mfano, kuna mikoa at least 24 bara, na michango kwenda serikali kuu inapokewa by name (jina la mkoa), kiasi cha mchango, sambamba na taarifa za Mapato na matumizi ya kila mchangiaji; tuna local govnt authorities 135, na zote zinajulikana kwa - majina, Mapato, matumizi, na michango. Hata Kama mfuko ni mmoja serikali kuu - je:
Katika muktadha wa muungano, haya yapo wapi?
Local government authorities pamoja na Kwamba zinapeleka fedha kwenye Mfumo mmoja, as I have demonstrated tayari, kila moja inatambulika kisheria na kila moja Ina "jurisdiction" yake. Isitoshe, local gvnt authorities zilianzishwa kwa Mujibu wa Sheria to provide public services within the areas of their jurisdiction, je mfuko wa pamoja wa muungano haukulenga suala la jurisdiction?jibu ni Kwamba jurisdictions were considered lakini umekwama kwa sababu jurisdiction ya Tanganyika haipo.
Mkandara, uwe Unafanya utafiti Kabla ya kujadili mambo; hiyo mikoa unayojadili Kiholela holela unasahau Kwamba Ipo under a "local government revenue collection system", na muhimu zaidi, local government development bank Ipo njiani kuwa established na hizi local gvnt authorities zitatakiwa "kuchangia" 5.2 bil shillings out of the total required 44.8b, huku serikali kuu ikipanga kuchangia 17b na vyanzo Vinginevyo 17b. Kumbuka, kila mkoa utakuwa na info juu ya Mapato yake, matumizi yake, na mchango wake, na mwisho wa siku ni kwa ajili ya kuendesha "serikali kuu" huku local gvnt authorities zikiwa ni serikali shiriki Katika muktadha husika.
Je chini ya JFC, again, kuna nini kina chofanania na haya kuonyesha upamoja transparently?
ni Nani wanatakiwa kuchangia? Kiasi gani? Kwa matumizi gani?
Sent from my iPhone using JamiiForums
Mkuu labda nichukue nafasi hii kuelezea matatizo yako wapi. Hili sii swala la muundo wa serikali bali ni tatizo la kiutawala na nimesema sana huko nyuma. Nakuombeni mnisome vizuri sana kisha tujiangalie sisi wenyewe na hizi mila na tamaduni zetu mbovu ambazo zinatukwaza nchi zote za Kiafrika - UBINAFSI.Kwa kiangalia mgawanyiko wa kiutawala na mapato na matumizi ya serikali mimi nashauri serikali moja, na hapo nina hakika tutajenga utaifa wetu
Mkuu utetezi wako kwa znz hauna mashiko. Sijui ulitaka znz inufaike vipi zaidi ya ilivyo sasa.Mkuu labda nichukue nafasi hii kuelezea matatizo yako wapi. Hili sii swala la muundo wa serikali bali ni tatizo la kiutawala na nimesema sana huko nyuma. Nakuombeni mnisome vizuri sana kisha tujiangalie sisi wenyewe na hizi mila na tamaduni zetu mbovu ambazo zinatukwaza nchi zote za Kiafrika - UBINAFSI.
Kutofaidika kwa Zanzibar kwa mambo 22 sio jambo geni kabisa katika nchi za Kiafrika na ndizo zimepelekea kuvunjika kwa miungano mingi tu kutokana na kwamba kila kiongoz anayeshika madaraka hutazama kwanza kwao na ataweza vipi kutumia rasilimali za taifa kunufaisha ailikotoka hata kama hakuchaguliwa na watu wa kwao. Tunayaona huko Nigeria, Sierra Lione, Sudan, Kenya, Uganda na sasa yameingia Tanzania na hizi ni nchi zenye miundo yote ya serikali 1 au 3.
Swala la mundo wa serikali limetokana na kero ya Wazanzibar kutofaidika na hayo mambo 22 jambo ambalo hata sisi bara tumelisema kuwa ni kero kutokana na kwamba Zanzibar hawachangii kitu wala hakuna mfumo wa kuchangia gharama wala kugawana mapato yake. Hivyo haa ukifanya serikali 1 bado watu ni wale wale wenye kufikiria kutumia rasilimali za taifa kujinufaisha wao, makwao alikotoka ama kabila lake ama dini yake. Haya yanaonekana wazi sasa hivi japo hatutaki kukubali na Nyerere alituonya juu ya mgawanyiko huu ambao zamani thatujawahi kuwa nao ila Tanzania kwanza.
Hivyo, kinachotakiwa ni mfumo bora wa utawala, sheria zinazotaka uadilifu na Uzalendo kwa taifa kuwa sifa ya kwanza ya kiongozi. Kuwezesha tuloshindwa kwa kuiwezesha Zanzibar ifaidike na hayo mambo 22 badala ya kugawana mbao ama kunyoosheana vidolekuwalaumu Wazanzibar ambao kwao kama hawafaidiki na imeshindikana basi bora yasiwepo hayo mambo 22 ya Muungano kila mtu ajitawale.
Binafsi yangu sioni ugumu wa kuyafanya hayo mambo 22 ya Muungano yatufaidhishe sote na wala sio hapo tu bali hata gas ya Mtwara iwafaidishe wananchi wa Mtwara na tiafa badala ya fedha hizo kwenda kujenga bandari Bagamoyo ama kupeleka mapato ya gas hiyo Dar es salaam. Dhahabu nayo iwafaidishe wananchi wa Mara na kadhalika ili kuepuka makosa yalowahi kufanywa na wenzetu ndani ya mfumo huu wa Kibepari ambao ndio chanzo cha migogoro ya nchi hizo, sisi tumebahatika toka mwaka 1984 pamojanakero kuzaana tumeweza kuhimili mikiki iliyopo kutokana na kile waasisi wetu walikianzisha. Umoja huo taratibu unaanza kuvunjika na utavunjika kabisa hadi mikoani kama tusipoangalia.
Tanzania kwanza inahitaji mfumo madhubuti ambao unatazama interest za nchi nzima na Ubinafsi uwe adui mkubwa wa haki. Uadilifu hautokani na hulka bali muundo uliopo maana sisi wenyewe tumekuja nchi za wenzetu na kukuta sheria tofauti kabisa kiasi kwamba imetulazimu sisi tubadilike. Ustaarabu haufundishwi wala hauna muundo bali ni mfumo mzima wa maisha ambao UTU umetukuzwa kwanza na sii ubinafsi. Tukiweza kuondokana na Ubinafsi basi hilo la serikali 1, 2 au 3 ni swala dogo kabisa ambalo litatokana na kuweka muundo bora wa kufikisha maendeleo haraka na kwa ufasaha kwa wananchi.
Haya na wewe umeruka kamba vile vile sasa unataka mimi nikueleze kipi? Unapoondoa mambo 22 ambayo Zanzibar hawakufaidika nayo ili yabakie 7 wakati mfumo ni ule ule, sii kesho watasema kwamba hata haya 7 hawafaidiki nayo? kero zitarudi palepale na sintofahamu uchangiaji na ugawanaji utabakia pale pale?. ebu nijibu kwanza hapa..Sii wingi wa kero unaotukwaza bali tunahitaji mfumo bora unaotuwezesha sote tufaidike na mambo yanayotuweka pamoja. Kuyaondoa ama kuyapunguza mambo sio suluhu bali tunajigawa wenyewe na kesho itakuwa mikoani na wilaya. Hata kama likibakia jambo moja la mungano kama bado mfumo ni ule ule wa nchi moja kutofaidika bado litakuwa tatizo (kero) la kuuvunja muungano.Mkuu utetezi wako kwa znz hauna mashiko. Sijui ulitaka znz inufaike vipi zaidi ya ilivyo sasa.
Tumekuonyesha kuwa katika mambo 22 yameondolewa na kubaki 7.
Katika 15 yaliyoondolewa, tumekuuliza Tanganyika imepoteza nini. Hukuwa na jibu
Tukakuuliza katika mambo 15 Zanzibar imenufaika na nini au imepoteza nini. Hukujibu.
Huwezi kuwa na taifa moja kukawa na sehemu moja inayochukua tu na wala si kuchangia.
Mkoa wa Dar es Salaam unachangia pato kubwa sana la taifa hili. Mgao wake kwa mwaka ukilinganisha na znz ni 1:30
Hapo unataka znz wanufaike vipi.
Tumekuuliza deni la ndani na nje znz inanufaika au kupata hasara gani. Huna jibu.
Hakuna sababu za Tanganyika kuwanyonya wznz, na njia nzuri ni kuwapa nafasi ya kutumia resource zao kujiendeleza.
Hilo linawezekana endapo tu tutatenga mambo ya JMT na Tanganyika. Kinyume chake ni kutaka resource za Tanganyika ziwe za zanzibar.
Na mwisho, kwani nani anataka mamlaka kamili? Kwanini usiwasote kidole wznz wanaotaka mambo yapunguzwe unasota kidole waliotaka mambo yote yawe ya muungano.
Halafu mkuu hoja zinakuishia sana. Upo katika rekodi(ukitaka nitaweka hapa) ukisema kuwa ni makosa kuongeza mambo kinyemela. Kwamba yalikuwa 11 na sasa ni 22. Kwa maana hiyo znz imenyimwa fursa ya kujitafutia maendeleo yake kwa kuchukua mambo yao na kuyafanya ya muunagano.
Leo unabadilika na kusema mambo 22 hawafaidiki nayo na ni vema yangewafaidisha. Yale yale uliyowahi kusema yameongezwa kinyemela unataka yawafaidhishe na si kuondolewa.
Mkuu unasimama wapi? upo kila mahali.
Karibu sana mkuu nimefanya marekebisho kidogo sehemu nilizokosea kuandika. natanguliza samahani.Kwa kweli ninashukuru mkuu kwa kunielewa haswa nilikuwa nataka kufikisha ujumbe huu kwa raia. Pia nimefurahi umejitahidi kuonesha ukweli halisi wa wapi tatiZo limejikita hadi tunafikia kudai muundo fulani wa uongozi.
Shida yetu Afrika ni kunyoosheana vidole kila leo badala ya kuondoa tofauti zetu na kuungana kwa pamoja ili tuweze kuwa na maisha yenye umoja na amani. Ninahisi ni wakati sahihi sasa Tanzania inabidi tujenge muundo sahihi wa serikali ambayo itatujenga wote kuwa kitu kimoja.
Mkuu wangu sasa unataka kunambia mnataka serikali 3 pasipo kujua kwamba kuna lazima ya serikali kuu kuwa na mfuko wa pamoja kutokana na kodi zetu? Yaani serikali 3 pasipo kujua gharama zake kwa wananchi ndio maana mnabisha au?
Mkuu wangu hakuna kosa kabisa isipokuwa mnaomba lisilowezekana, sijui kama mnanielewa. maadam hili haliwezekani kupitia maridhiano na CCM kwa nini msikubali hilo la serikali 2 kisha katiba iandikwe halafu wananchi waje kuzikataa hizo serikali 2 maana sababu zote zimekwisha semwa na wananchi wanajua wao wanataka nini. Kama mna hakika kabisa kwamba wananchi wanataka serikali 3 basi waachieni wao waamue huko mbele. Kugoma kuendelea inadhihirisha UKAWA hawana hakika ya wananchi isipokuwa hili ni swala la kisiasa zaidi.
tatizo lako husomi na kuelewa hoja ya mwenzako na ndio amana nasema hujui tunachozungumzia wala hufuatilii isipokuwa kubisha tu ili mradi ubishane. Wakati tuna mambo 22 ilikuwa wakati wa Nyerere na serikali yake ya chama kimoja ilikuwa ikiimiliki kila kitu toka vyanzo hadi mauzo hivyo tofauti kubwa sana imekuja tokea wakati wa mabadiliko ya kiuchumi na siasa yetu. haya ni mageuzi makubwa ambayo hatukuyafanyia marekebisho makubwa ya kikatiba isipokuwa kwa wanasiasa wenyewe.Halafu mkuu hoja zinakuishia sana. Upo katika rekodi(ukitaka nitaweka hapa) ukisema kuwa ni makosa kuongeza mambo kinyemela. Kwamba yalikuwa 11 na sasa ni 22. Kwa maana hiyo znz imenyimwa fursa ya kujitafutia maendeleo yake kwa kuchukua mambo yao na kuyafanya ya muunagano.
Leo unabadilika na kusema mambo 22 hawafaidiki nayo na ni vema yangewafaidisha. Yale yale uliyowahi kusema yameongezwa kinyemela unataka yawafaidhishe na si kuondolewa.
Mkuu unasimama wapi? upo kila mahali.
Hawachangii muungano, naomba kuweka sawa hilo. Hakuna suala la uchangiaji wao ni mdogo.Nguruvi3, tatizo lako husomi na kuelewa hoja ya mwenzako na ndio amana nasema hujui tunachozungumzia wala hufuatilii isipokuwa kubisha tu ili mradi ubishane. Wakati tuna mambo 22 ilikuwa wakati wa Nyerere na serikali yake ya chama kimoja ilikuwa ikiimiliki kila kitu toka vyanzo hadi mauzo hivyo tofauti kubwa sana imekuja tokea wakati wa mabadiliko ya kiuchumi na siasa yetu. haya ni mageuzi makubwa ambayo hatukuyafanyia marekebisho makubwa ya kikatiba isipokuwa kwa wanasiasa wenyewe.
Hivyo yale mambo 22 ya Jamhuri yalipokuwa sii ya Muungano tena, ndipo Wenzetu wa kizazi kipya wakahoji kuwa yale 11 yaliongezwa Kinyemela maana muungano wetu ulitaja 11 tu. Wamehoji hadi hati ya muungano yote ni kutokana na kutofaidika. JK katueleza ukweli jinsi mambo yale yalivyoongezwa lakini kwao Wazanzibar wamechukulia kwamba ilikuwa mambo 11 ya mkataba hawafaidiki nayo sasa yamekuwa 22 yote kwa bara.
Hii yote ni kutokana na kwamba hatukuwa na mfumo wa kufaidika sote hivyo ndivyo navyosema na ndivyo nilivyosema awali. Kwani kuna shida gani Zanzibar kufaidika na mambo ya Muungano? ama mnaona uchangaji wao utakuwa mdogo lakini ktk mapato watavuta nyingi zaidi ya uchangiaji maana kuna hesabu kubwa ya misaada na mikopo ktk hayo mambo 22 ya Muungano?
Wasichotaka akina Mkandara ni kuona znz inawajibika.
Thats just Bologna!Sababu juu ya kwanini mfuko wa pamoja haufanyi kazi ni Kwamba ni Vigumu kutenganisha masuala ya Tanganyika na ya muungano. Kwa maana nyingine, mfuko wa pamoja ni hekaya za abunuwasi bila ya uwepo wa Tanganyika kwani ni impossible kubaini ya pamoja ni yepi na ya kila upande kivyake ni yepi chini ya serikali Mbili. Ni Vigumu kuelewa kwanini watu makini Kama wewe na Mkandara mnashindwa ona Hilo.
Na sasa, uwepo wa nchi Mbili serikali Mbili Ndio umeua Kabisa hata hiyo ndoto ya joint finance commission. Nyinyi Hali hii inazidi kuwapa matumaini Kwamba JFC can work, na pia Kwamba serikali moja inawezekana, na several other impractical and utopian views.
Uzi wa gharama tulio ahidi upo pale pale, hakuna kilichobadilika zaidi ya suala la timing kutokana na mchakato mzima wa BLK kuingia nyongo. Vinginevyo maandalizi yapo pale pale na Uzi utapanda ndani ya siku Tatu na utaweka sawa masuala mengi ambayo mmekuwa mnayakwepa Kama sio kuyapotosha.
Sent from my iPhone using JamiiForums
Hapo kwenye nyekundu hapo!!Mchambuzi ha ha haa! kuna njia iliwahi kutumiwa na mbunge moja huko Kenya katika kuhakikisha kuwa mpinzani wake gets the message lakini sidhani kama inaweza kutumika mtandaoni. Hawa watu ni wasanii na kama ilivyo kwa wasanii siku zote, muda utafika na itabidi ama wazinduke au waachwe kwenye mataa na ulaghai wao! Hata huko ndani ya BMLK tayari watu wanaanza kujikuta face to face with reality kwamba hakuna namna ya kuboresha muundo wa serikali mbili bila kwanza kuhakikisha yapo mamlaka yatakayoshughulikia tu mambo ya Tanzania bara (Tanganyika) na humo hawatakiwi wasio wa Tanganyika na hivyo hivyo kwa Tanzania visiwani (Zanzibar).
Eti inapendekezwa bunge moja yenye sehemu tatu ambazo ni Bunge la Muungano kwa masuala ya muungano na humo humo linakuwa na sehemu mbili ambazo ni wabunge wa Zanzibar kwa ajili ya masuala ya Wazanzibari na sehemu ya Tanganyika kwa ajili ya mambo ya bara. Hata hivyo kulingana na ripoti kutoka vyanzo mbalimbali neno tatu tayari linazua kiwewe kwani wajumbe wanachama wa CCM wanaona kama vile hiyo ni sawa na kula matapishi yao kwani unashabihiana na muundo wa muungano wa serikali tatu ambao ulipendekezwa na Tume ya Mabadiliko ya Katiba! Na hapo bado maswala ya Mahakama, Mamlaka ya Raisi na mengineyo...kweli mbio za sakafuni huishia ukingoni.
Mkandara na Kobello hawathubutu kujibu swali la mfuko wa pamoja kwa sababu jibu lolote lile watakalolitoa lina maana ya kuundwa kwa mamlaka tatu ya washiriki kwa pamoja (Tanzania) na washiriki binafsi (Tanganyika na Zanzibar)! Watakimbia, watarukaruka lakini mwisho wa siku watakuta hawana pa kutokea, Tume ilishafanya kazi yake kwa weledi na kuziba mianya yote ya kutokea. Kulingana na rasimu kila jimbo Zanzibar litakuwa na mwakilishi moja tu badala ya wawili kama sasa na ni huyo huyo ataiwakilisha Zanzibar kwenye kikao cha Bunge la Muungano na Bunge la Zanzibar. Hata hii peke yake itapunguza gharama zisizo lazima kwa kiasi fulani.
Mheshimiwa, Nyerere alijaribu kufanya hivyo. Hakuna kiongozi Afrika aliyependa Uafrika na Waafrika kama Nyerere.Kwa kweli ninashukuru mkuu kwa kunielewa haswa nilikuwa nataka kufikisha ujumbe huu kwa raia. Pia nimefurahi umejitahidi kuonesha ukweli halisi wa wapi tatiZo limejikita hadi tunafikia kudai muundo fulani wa uongozi.
Shida yetu Afrika ni kunyoosheana vidole kila leo badala ya kuondoa tofauti zetu na kuungana kwa pamoja ili tuweze kuwa na maisha yenye umoja na amani. Ninahisi ni wakati sahihi sasa Tanzania inabidi tujenge muundo sahihi wa serikali ambayo itatujenga wote kuwa kitu kimoja.