Mag3
Platinum Member
- May 31, 2008
- 13,580
- 23,914
Mchambuzi ha ha haa! kuna njia iliwahi kutumiwa na mbunge moja huko Kenya katika kuhakikisha kuwa mpinzani wake gets the message lakini sidhani kama inaweza kutumika mtandaoni. Hawa watu ni wasanii na kama ilivyo kwa wasanii siku zote, muda utafika na itabidi ama wazinduke au waachwe kwenye mataa na ulaghai wao! Hata huko ndani ya BMLK tayari watu wanaanza kujikuta face to face with reality kwamba hakuna namna ya kuboresha muundo wa serikali mbili bila kwanza kuhakikisha yapo mamlaka yatakayoshughulikia tu mambo ya Tanzania bara (Tanganyika) na humo hawatakiwi wasio wa Tanganyika na hivyo hivyo kwa Tanzania visiwani (Zanzibar).
Eti inapendekezwa bunge moja yenye sehemu tatu ambazo ni Bunge la Muungano kwa masuala ya muungano na humo humo linakuwa na sehemu mbili ambazo ni wabunge wa Zanzibar kwa ajili ya masuala ya Wazanzibari na sehemu ya Tanganyika kwa ajili ya mambo ya bara. Hata hivyo kulingana na ripoti kutoka vyanzo mbalimbali neno tatu tayari linazua kiwewe kwani wajumbe wanachama wa CCM wanaona kama vile hiyo ni sawa na kula matapishi yao kwani unashabihiana na muundo wa muungano wa serikali tatu ambao ulipendekezwa na Tume ya Mabadiliko ya Katiba! Na hapo bado maswala ya Mahakama, Mamlaka ya Raisi na mengineyo...kweli mbio za sakafuni huishia ukingoni.
Mkandara na Kobello hawathubutu kujibu swali la mfuko wa pamoja kwa sababu jibu lolote lile watakalolitoa lina maana ya kuundwa kwa mamlaka tatu ya washiriki kwa pamoja (Tanzania) na washiriki binafsi (Tanganyika na Zanzibar)! Watakimbia, watarukaruka lakini mwisho wa siku watakuta hawana pa kutokea, Tume ilishafanya kazi yake kwa weledi na kuziba mianya yote ya kutokea. Kulingana na rasimu kila jimbo Zanzibar litakuwa na mwakilishi moja tu badala ya wawili kama sasa na ni huyo huyo ataiwakilisha Zanzibar kwenye kikao cha Bunge la Muungano na Bunge la Zanzibar. Hata hii peke yake itapunguza gharama zisizo lazima kwa kiasi fulani.