Nguruvi3
Platinum Member
- Jun 21, 2010
- 16,306
- 33,775
Hili la kuelekea S1 dah ni ndoto ninayoomba nisiiote maana naweza kuamka kichwa kikuma. Mwaka 1985 tulijiita Watanzania, leo kuna Watanzania na Wazanzibar.Sheikh Ngruvi3 naona bado "hujanfahamu": mimi siungi mkono "udhalimu" wa Zenj dhidi ya Tanganyika.
Mimi ni muumini wa Muungano. Hofu yangu ni kwamba tukiwa na 3 basi muungano utakufa.
Ninaunga mkono 2 (zisizo na unyonyaji) kama "transitory process towards 1". Naamini baada ya miaka mingi ijayo ndoto hiyo itatimia...baada ya wale wenye "uchu wa madaraka" (kama waitwavyo) na wale "wenye uchungu sana na mapinduzi daima" kuwa wamepisha kizazi kingine ambacho kitajali zaidi maendeleo kwa wananchi kuliko historia.
Ila, kama plan B, ikiwa tumeshindwa kuafikiana kwa 2 au 3, tutafute namna ya kuachana kwa amani. Tujipe kama miaka 10 kama twataka Muungano na kwa muundo upi. Tutaachana kwa kura ya maoni kwa wananchi, na tujiulize baadaye kwa kura ya maoni kama twataka kuungana tena kwa mtindo upi. Katika kipindi hicho cha miaka 10 kila upande uendeshe mambo yake na baada ya miaka 10 iitishwe kura ya maoni.
Mwaka 1990 tulikuwa na mambo 22, leo yanaitwa unyonyaji tunataka yapungue.
Mwaka 200 tulikuwa na katiba ya JMT, leo kuna katiba ya JMT na Katiba kuu ya JMTZNZ
Ndoto hizo mungu aniepushe nazo.
Hapo mwisho umemealizia vizuri sana, hata mimi nashauri tuvunje jahazi tugawane mbao.
Hatuna sababu za kuungana twaweza ishi kama tuishivo na Msumbiji.
Mimi sioni tabu hata kidogo wznz wakiondoka zao. Na sioni kama kuna Mtanganyika anayeona tabu isipokuwa wale watu wanaoona haya dhidi ya Utaifa wao.
Yule kichwa panzi wa BB-zanzibar kasema, znz itastawi kutokana na misaada kwasababu ni kisiwa kidogo.
Hapa JF wapo wanaodhani znz ni bora ikipata misaada, na hata kudhani misaada ni jambo la fahati! phwe
Wapo wanaodhani znz inahitaji kiti IMF, WB ili itambulike
Watanganyika wanasema waacheni wapate vitu hivyo, na wala wasisumbuliwe.
Tusichotaka kusikia ni kasehemu kadogo kakichukua kodi za Watanganyika, kuchangia zero na kulalamika 100%
Itafika mahali wznz wanalala tu, kwasababu Watanganyika wanawalipia kodi. Upuuzi huo sasa mwisho.