Serikali 3 na gharama zake

Serikali 3 na gharama zake

Kuhusu wabunge wa Zanzibar kuwa 20 ... unachekesha sana tena sana!! ... hao jamaa ni kama 50% ya wabunge wote kwa sababu hakitapita kitu chochote bila 2/3rd yao kukubali. Usijidanganye, hiyo ni 50/50 kwenye bunge la muungano. na wala msijaribu kuanzisha lower house kwa sababu wanaweza kugawa majimbo yao kwa kutumia mitaa na msifanye chochote kile. LOL that Draft has a lot of holesto be filled.
Mkuu umesema wewe upo ndani ya chaki. Nadhani ulipoandika bandiko hili ulifungia chaki kabatini.

Hoja ya Mag3 ni kuwa kwasasa Tanganyika inalipia wabunge 81 kutoka znz.
Rasimu inasema hakuna cha wabunge wa BLW au JMT. Kutakuwa na mbunge mmoja tu kwa jimbo.

Kwa mujibu wa rasimu wabunge wa znz ni 20. Kwasasa tunahudumia 81.
Ukiondoa 60 unapunguza zigo kwa Mtanganyika.

Sasa wakiwa 81 bado ni 2/3. Wakiwa 20 bado ni 2/3. Kwa weledi usiohitaji chaki, kuwa na 20 ni bora kwa gharama.

Matokeo ya 81 au 20 ni 2/3. Gharama ndizo zinabadilika mkuu.
 
Mkandara;10369929]Mkuu wangu hakuna kosa kabisa isipokuwa mnaomba lisilowezekana, sijui kama mnanielewa. maadam hili haliwezekani kupitia maridhiano na CCM kwa nini msikubali hilo la serikali 2 kisha katiba iandikwe halafu wananchi waje kuzikataa hizo serikali 2 maana sababu zote zimekwisha semwa na wananchi wanajua wao wanataka nini. Kama mna hakika kabisa kwamba wananchi wanataka serikali 3 basi waachieni wao waamue huko mbele. Kugoma kuendelea inadhihirisha UKAWA hawana hakika ya wananchi isipokuwa hili ni swala la kisiasa zaidi.
Hocus pocus !Tume iliundwa na nani na kwa nini? Si CCM ndio waliongoza mchakato. Kama wana uhakika wa S2 kwanini wasingeacha taratibu ziendelee ili kura ya maoni itungue rasimu ?
Mkuu, kwani tume ilipomkabidhi mwenyekiti wa CCM rasimu, ilikabidhi rasimu ya mfumo wa S2?

Mkuu soma tena ulichoandika halafu ujiulize kama ulimaanisha hivyo au ni kughalifikiwa.
Naogopa maswali yako mhh watu wasijeangua vicheko
 
Mkuu wangu hakuna kosa kabisa isipokuwa mnaomba lisilowezekana, sijui kama mnanielewa. maadam hili haliwezekani kupitia maridhiano na CCM kwa nini msikubali hilo la serikali 2 kisha katiba iandikwe halafu wananchi waje kuzikataa hizo serikali 2 maana sababu zote zimekwisha semwa na wananchi wanajua wao wanataka nini. Kama mna hakika kabisa kwamba wananchi wanataka serikali 3 basi waachieni wao waamue huko mbele. Kugoma kuendelea inadhihirisha UKAWA hawana hakika ya wananchi isipokuwa hili ni swala la kisiasa zaidi.

sasa mnapokataa na kugoma kwa sababu ya tanganyika inatuweka pabaya zaidi kwa sababu katiba Mpya haitaandikwa na haitawafikia wananchi hivyo BLK litalazimika kutunga sheria nyinginezo ambazo ni za uchaguzi 2015 na kwa ajili yao wanasiasa, sisi nwananchi tutabakia na muundo wa serikali 2 na madudu yote ya katiba iliyopo ambayo kwanza haina miiko wala Maadili ya Uongozi na kibaya zaidi tutaendelea na wakuu wa mikoa wilaya, Tiss na Polisi kuendelea kuwa vombo cha chama tawala na nguvu kubwa ya rais pale pale - Tumefanya nini? Sii mnadai katiba hii ni ya wananchi kwa nini hamuwapi nafasi wao wafanye maamuzi wanataka serikali gani mana hta haya mabadiliko sura ya uchaguzi sidhani kama ni yatahitaji ridhaa ya wananchi.

Pasipo katiba mpya msitegemee kabisa kwamba CCM wataondoka madarakani maana iliyopo inawapa nafasi kibao za kugeuza kila kitu hata matokeo japo hao UKAWA wanafikiri wataweza kuhakikisha Uchaguzi huru unapatikana. Hilo tusahau..na najisikia vibaya zaidi tunapopigania tanganyika kwa sababu ya Wazanzibar ambao kwao mimi naiona hoja yao kuwa ya maana kabisa na rahisi kabisa kuimaliza kwani taabu iko wapi?.

Hizi ndio hekima na Busara tunazozungumzia kila siku.. fikiria mbali zaidi ya marefu ya mkono.

..tunataka kitu kilicho bora.

..mimi nadhani kulazimisha hizi 2 wakati zimetuletea matatizo na migogoro kwa miaka arobaini siyo busara hata kidogo.

..hebu fikiria ni kamati na tume ngapi zimeundwa kuchunguza matatizo ya serikali 2 na gharama[rasilimali na muda] tulizotumia?

..unless unataka kuvunja muungano, lakini kila aliyetafuta namna ya kuunusuru muungano wetu, ameishia na pendekezo la serikali 3[tanganyika, zanzibar, muungano].

..hata CCM sasa hivi wanahangaika na kujitutumua lakini mapendekezo wanayokuja nayo yanaangukia kwenye serikali 3[tanganyika, zanzibar, muungano]. pendekezo mojawapo tulilosikia toka kwa wana CCM walioko bunge la katiba ni kuwepo kwa lower house[bunge la tanganyika] na upper house[bunge la muungano]. sasa katika mazingira hayo kwanini isiundwe serikali ya tanganyika?

..wapo wanaodai serikali 3 ni gharama. lakini mimi kwa uelewa wangu hata serikali 2 nazo ni gharama. sasa kama tatizo ni gharama mbona hakuna pendekezo hata moja tulilosikia la kupunguza gharama katika hizi serikali 2 tulizonazo??

cc Mchambuzi, Nguruvi3, Mag3
 
Last edited by a moderator:
..
..hata CCM sasa hivi wanahangaika na kujitutumua lakini mapendekezo wanayokuja nayo yanaangukia kwenye serikali 3[tanganyika, zanzibar, muungano]. pendekezo mojawapo tulilosikia toka kwa wana CCM walioko bunge la katiba ni kuwepo kwa lower house[bunge la tanganyika] na upper house[bunge la muungano]. sasa katika mazingira hayo kwanini isiundwe serikali ya tanganyika
Hili la lower na upper house tumeliongea sana siku za nyuma.
UKishakuwa na bunge la Tanganyika, lazima uwe na bajeti yake, uongozi wa bunge, serikali ndani ya bunge, mawaziri n.k. Huwezi kuwa na bunge jina.

CCM wameshakubali kuwa S2 hazikubaliki na haziwezekani. Njia yoyote watakayotumia itawaelekeza S3.
Hakuna option itakayowaacha salama bila S3.
 
..tunataka kitu kilicho bora.

..mimi nadhani kulazimisha hizi 2 wakati zimetuletea matatizo na migogoro kwa miaka arobaini siyo busara hata kidogo.

..hebu fikiria ni kamati na tume ngapi zimeundwa kuchunguza matatizo ya serikali 2 na gharama[rasilimali na muda] tulizotumia?

..unless unataka kuvunja muungano, lakini kila aliyetafuta namna ya kuunusuru muungano wetu, ameishia na pendekezo la serikali 3[tanganyika, zanzibar, muungano].

..hata CCM sasa hivi wanahangaika na kujitutumua lakini mapendekezo wanayokuja nayo yanaangukia kwenye serikali 3[tanganyika, zanzibar, muungano]. pendekezo mojawapo tulilosikia toka kwa wana CCM walioko bunge la katiba ni kuwepo kwa lower house[bunge la tanganyika] na upper house[bunge la muungano]. sasa katika mazingira hayo kwanini isiundwe serikali ya tanganyika?

..wapo wanaodai serikali 3 ni gharama. lakini mimi kwa uelewa wangu hata serikali 2 nazo ni gharama. sasa kama tatizo ni gharama mbona hakuna pendekezo hata moja tulilosikia la kupunguza gharama katika hizi serikali 2 tulizonazo??

cc Mchambuzi, Nguruvi3, Mag3
Mkuu shukran sana unapokuja na hoja badala ya hawa jamaa zangu hoja yao ni kina Mkandara tunasema nini wakimaanisha mimi na CCM wakati hili sii swala langu mimi wala la CCM ila la wananchi wote na tunaitaka katiba Bora na sii vinginevyo.
Yawezekana sio Busara kulazimisha serikali 2 lakini busara hutumika kwa kutazama mbali na sio kilichopita, maamuzi yenye busara ni kutazama mabadiliko tunayokusudia yana athari gani mbele ya faida zake hivyo tunajenga kinga mbele ya hatua. Serikali 3 zimekubalika na wengi kama mnavyosema lakini sio suluhisho la matatizo ya Muungano wetu ndio jibu langu. Hakuna mahala popote serikali 3 inaondoa mapungufu ya utekelezaji wa serikali 2 isipokuwa kutenganisha mahitaji na matumizi kutokana na kero hivyo hapatakuwa na ufanisi wa serikali hizi kwa wananchi ikiwa bado tuna mambo ya muungano yasiokuwa ya Muungano ambayo ndio chanzo cha kero. Sijui umenielewa - Mambo ya muungano, yasokuwa ya Muungano!

Kinachotakiwa kutazamwa hapa ni sababu gani zimezua kero hizi zilizopo, nalo ni kuwepo kwa mambo ya Muungano ambayo yana mamlaka ya upande mmoja, kugharamiwa na upande mmoja, na kufaidisha upande mmoja na sababu zimetolewa tumezisoma sote. Tukiunda serikali 3 hiyo ya Muungano itakuwa na lawama hizo hizo iwe ktk jambo moja ama 7 kwa sababu ugonvi wa viongozi wetu ni katika mamlaka yake na kufaidisha pande zote mbili. Na kama nilivyosema toka awali tulikuwa na 22 toka wakati wa Mwalimu lakini wakati ule chama tawala ndio kilimiliki njia kuu za uchumi hawakutegemea kodi za wananchi hivyo waliweza kutumia kwa kutazama mahitaji ya nchi nzima. Serikali ilikuwa ndio ikifanya biashara na hivyo mapato yake ndio yalipanga matumizi ya mapato hayo. Hali imegeuka sasa hatuna tena Ujamaa wala serikali haitakiwi kumiliki njia za uchumi isipokuwa kutunga na kusimamia sharia na kukusanya kodi zake huku ndiko tunapwaya kisheria.

Na tumekuja gundua pia kwamba haya mambo ya Muungano sii ya Muungano tena bali ni ya Tanganyika na yamekuwa yakigharamiwa na serikali ya Tanganyika (JMT) kwa hiyo ni kodi za watanganyika ndio zimekuwa zikiiendesha serikali hii ya JMT, hivyo hatukuwa na kitu serikali ya Muungano maana hata mfuko wake haukuwepo. Na hivyo Zanzibar hawakuwa na sio tu mamlaka nayo bali hata kufaidika nayo maana sababu tunazopewa ati hawakuwa wakichangia. Haya ndio makosa yalokuwepo na yanahitaji kufanyiwa marekebisho. Sijui kama ananifuatilia.

Sasa ili tuweze kuondoa kero hizi, watanganyika wamedai kujua jinsi ya uchangiaji wa gharama za serikali hii ua muungano na mgawanyo wa mapato. Wananchi wa Zanzibar pia wamedai kutaka kujua jinsi ya uchagiaji na mgawanyo wa mapato kwa seriklai hii ya muungano. Haya yote yapo ktk orodha ya kero na yameelezwa na tume ya Warioba walipokwenda kumuona rais na tumeelezwa bungeni. Hivyo basi nachosema mimi hata kama tukibakiza 7 na ikawepo serikali kuu ya 3 ambayo ndiyo yenye dhamana ya haya mambo 7 bado mambo haya yatakuwa mzigo wa Tanganyika na mamlaka yake yatakuwa chini ya Tanganyika kwa sababu zile zile tunazojenga leo hii.

Kiukweli kabisa matatizo makubwa yalozua kero zetu yametokana na haya mambo 7 ambayo ni muhimu sana ktk ujenzi wa Muungano na yataendelea kuwepo ikiwa hatutafikiria mfumo mpya kutuwezesha sote tufaidike nayo. Zanzibar wataendelea kudai OIC laa sivyo wapewe mamlaka kamili ya kutafuta marafiki zao, jambo ambalo wizara ya mambo ya Nje haikubaliani nalo na tutarudi pale pale ndani ya serikali 3 au 2. Sasa Je, ili Zanzibar wapate hili inatakiwa tufanye nini? ndio nasema Sheria mama iache mamlaka hayo kwa nchi zake pasipo kuwepo sharia juu ya mahusiano na hivyo( litakuwa sii jambo la muungano) ama sheria mama iruhusu OIC kuwa ni swala la taifa, hivyo OIC iruhusiwe kuwa na matawi yake bara na visiwani (linakuwa jambo la Muungano).

Kuna mahala watu wanazungumzia Jeshi letu ati Zanzibar wanachangia kiasi gani?.. Hivi kweli tunaweka kambi za majeshi yetu mahala kutokana na mchango wao? jeshi letu lenye kambi Zanzibar ni Jeshi la Muungano, na Zanzibar ni sehemu muhimu ktk ulinzi wetu sio kwa sababu nyingineyo. Hilo jina la KMKM ni jina la kambi ya jeshi la maji. Na ikitokea vita, jeshi hilo linakwenda popote kwa amri ya rais kama kambi za majeshi mengineyo. Hatukuweka kambi Ruvuma kwa sababu Ruvuma inachangia kiasi fulani bali tunahitaji wapi kambi zetu ili kufanikisha mahitaji yetu ya Usalama wa Taifa. Kwa fikra hizi nadhani ndio maana mnataka serikali 3 ili kutenganisha tu ya Zanzibar na Tanganyika, I mean mnanichanganya sana wajamaa nyie.

Nijuavyo mimi, mambo ya Muungano ni sharia mama ambayo itagusa sehemu zote za Jamhuri iwe Elimu, Afya, Utalii na kadhalika, sheria ambazo haziwezi kuvunjwa na nchi yoyote mshirika ndani ya katiba yake ama sheria zake. Sheria mama ikisema ELIMU ni bure kwa wote basi sii bara wala Zanzibar wanaruhusiwa kukiuka sharia hiyo, hili linakuwa jambo la Muungano, lakini sharia mama ikiacha miaya juu ya private school basi kila nchi inaruhusiwa kutunga sharia zake juu ya shule za watu binafsi pasipo kukiuka sheria mama ilowekwa. Hii haina maana mkiunda serikali 3 ndio utakuwepo ufanisi mzuri zaidi kwa wananchi wakati kazi kubwa ya serikali katika mfumo huu wa Kibepari ni kutunga policies na kusimamia utekelezaji wa policies hizo, hivyo bado hatuja tazama wapi tunahitaji ushirika kwa mahitaji ya wananchi bali mahitaji ya watawala. Sasa hivi pato la serikali linatokana na kodi zetu sisi wananchi na hivyo kwa kila mnachoomba kumbukeni ni kodi zenu ndizo zitaendesha serikali hizi. Huko mbele tunatarajia serikali zetu kutoendesha biashara ya aina yoyote.

Hivyo, nachokiona mimi hapa ni watu kutaka kugawana madaraka tu sio ufanisi, ni kujenga njia za ulaji kwa sababu ati serikali 3 zinatupa picha kamili ya nchi washirika lakini haiondowi matatizo ya wananchi, jambo ambalo mimi ningependa sana upande huo wa S3 wajenge hoja zinazo tusaidia wananchi tuwe na uhuru zaidi, haki zaidi, tusilipe kodi zaidi ili kuziwezesha serikali hizi katika utekelezaji wa majukumu yake. Tunazua majukumu tukidanganywa hapatakuw ana gharama, hii sio kweli maana naishi ktk nchi zenye ukiritimba na gharama kubwa ya serikali kuu.

Nachokisoma na kuelewa toka kwa hawa jamaa zangu ni madai yasokuwa na msingi, ni sawa na familia yako iwe na matatizo ya ndani ktk matumizi mkasema toka leo tutatenganisha Mr na Mrs badala yake mkeo atatumia jina lake na wewe utatumia jina lako ilihali kinachodaiwa ni mkeo kusema ‘Mume wangu mbona nyumba zote mume wangu ziko ktk majina yako?' Sasa unapotenganisha majina na kusema haya mimi na wewe tutakutana katika mambo haya, - Kwani katika nyumba hizi wewe ilichangia hata senti moja? Hapa ndipo mnaponiacha hoi na kuona kumbe tuna sisi tatizo la Ubwana na sii vinginevyo.
 
Mkuu umesema wewe upo ndani ya chaki. Nadhani ulipoandika bandiko hili ulifungia chaki kabatini.

Hoja ya Mag3 ni kuwa kwasasa Tanganyika inalipia wabunge 81 kutoka znz.
Rasimu inasema hakuna cha wabunge wa BLW au JMT. Kutakuwa na mbunge mmoja tu kwa jimbo.

Kwa mujibu wa rasimu wabunge wa znz ni 20. Kwasasa tunahudumia 81.
Ukiondoa 60 unapunguza zigo kwa Mtanganyika.

Sasa wakiwa 81 bado ni 2/3. Wakiwa 20 bado ni 2/3. Kwa weledi usiohitaji chaki, kuwa na 20 ni bora kwa gharama.

Matokeo ya 81 au 20 ni 2/3. Gharama ndizo zinabadilika mkuu.
Soma vizuri 105(3) na (4) halafu uniambie kitakachoizuia serikali ya Zanzibar kufanya kila mtaa kuwa wilaya na pia uniambie hiyo 20 umeitoa wapi?? Je, kukiwa na wilaya 40 Zanzibar mtafanya nini?

Kuhusu 2/3, hivi ni wabunge wangapi wa Zanzibar wanaotakiwa kupitisha bajeti au kutoa/kubadili matumizi ya consolidated fund? Kupitisha sheria yeyote zaidi ya Kubadilisha katiba?? two thirds ya Zanzibar ni kwenye mambo ya katiba. Kwa hiyo 2/3rd is not just 2/3rd ..... kwenye bunge la muungano lililopendekezwa 2/3rd ya Wazanzibari ni kwenye kila kitu ... it's like 50/50.

Gharama hazijabadilika Zanzibar au Tanganyika wana uhuru wa kuanzisha majimbo yao kadri wanavyotaka .... who knows we may have 200 Members of The Parliament, nani atawazuia?

Kwa hiyo mkuu mimi nadhani majitaka ni majitaka tu!, Waliozoea siasa za majitaka kama Mag3 HUWA WAKO TOO SUPERFICIAL,HAWAANGALII VITU IN DEPTH.
 
Mimi sintokwenda huko ila najaribu kuwaelewa hawa jamaa maana wanazungumzia ya zanzibar tu. Hivi kutokana na msemo wa Nguruvi3 hapo juu
Hoja ya Mag3 ni kuwa kwasasa Tanganyika inalipia wabunge 81 kutoka znz.
Rasimu inasema hakuna cha wabunge wa BLW au JMT. Kutakuwa na mbunge mmoja tu kwa jimbo
ya kwamba kutakuwa na mbunge mmoja kwa jimbo, je hiyo bara tuna majimbo mangapi?. Sio kusema kwamba utaondoa hao 60 wa Zanzibar lakini utaongeza wabunge wa majimbo ya Bara ktk seriklai hiyo na pia serikali ya Tanganyika itakuwa na wabunge wote wa majimbo yake yote!. Hivyo, kama ndivyo kweli rasimu inasema huku bara tutakuwa na wabunge wangapi in total wa serikali ya Tanganyika na serikali ya Jamhuri ambao wewe mwananchi utawalipia mishahara, Vx na posho zao juu, acha mbali vikao vya hayo mabunge mawili kuyagharamia.
 
Soma vizuri 105(3) na (4) halafu uniambie kitakachoizuia serikali ya Zanzibar kufanya kila mtaa kuwa wilaya na pia uniambie hiyo 20 umeitoa wapi?? Je, kukiwa na wilaya 40 Zanzibar mtafanya nini?

Kuhusu 2/3, hivi ni wabunge wangapi wa Zanzibar wanaotakiwa kupitisha bajeti au kutoa/kubadili matumizi ya consolidated fund? Kupitisha sheria yeyote zaidi ya Kubadilisha katiba?? two thirds ya Zanzibar ni kwenye mambo ya katiba. Kwa hiyo 2/3rd is not just 2/3rd ..... kwenye bunge la muungano lililopendekezwa 2/3rd ya Wazanzibari ni kwenye kila kitu ... it's like 50/50.

Gharama hazijabadilika Zanzibar au Tanganyika wana uhuru wa kuanzisha majimbo yao kadri wanavyotaka .... who knows we may have 200 Members of The Parliament, nani atawazuia?

Kwa hiyo mkuu mimi nadhani majitaka ni majitaka tu!, Waliozoea siasa za majitaka kama Mag3 HUWA WAKO TOO SUPERFICIAL,HAWAANGALII VITU IN DEPTH.
Well, bunge la S3 kama shirikisho lina idadi ya wajumbe kutoka znz na Tanganyika ambao ni fixed. Kutakuwa na jumla ya 55 kwa mujibu wa rasimu.
Kama sikosei znz watakuwa 20 na Tanganyika 75, sina uhakika lakini ni karibia na hapo.

Kilichotumika na tume ni kutumia wilaya zilizopo kufikia idadi. Hebu someni muelewe.
Haikusema wabunge watategemea kuongezeka kwa wilaya.Someni muelewe kwanza msikurupuke tu

Zanzibar inaweza kuwa na wilaya 600 baada ya hapo, hilo halitaongeza idadi yao katika Bunge la shirikisho kwasababu ipo stated.

Zanzibar wanaweza kuwa na wabunge 700 BLW hakuna atakayewazuia kwasababu ni gharama zao.

Tanganyika nayo itaamua kulingana na mahitaji yake. Kuna uwezekano kukawa na wabunge 150 tukizingatia kuwa Dar es salaam yenye watu milioni 5 inao 7. Hivyo ni Watangayika watakaoamua. Inawezekana wakawa 1000 ni juu yao.

Hadi hapo unaona uzuri wa kutenga mambo, yaani unatoa fiscal autonomy.

Kwasasa znz ina BLW 50, wachache kuliko 81 wanaokuja Dodoma.

Sababu kubwa ni kuwa znz ina fiscal autonomy na inaona haimudu zaidi ya 50.
Lakini wanaleta 81 kwasababu mzigo wa gharama zao anaubeba Mtanganyika. Umeona hapo?

Kuhusu 2/3 hata kama wznz ni 10 bado 2/3 ni ile ile ambayo ni 50% katika maamuzi.
Ukiwa nao 81 ni 2/3 ile ile ambayo ni 50% ya maamuzi.

Hivi hapo huoni unapunguza gharama ukiwa nao 10 kwa uzito ule ule kuliko kuwa na 81 kwa uzito wa maamuzi usioongezeka au kupungua? Mkuu hapa ni hesabu, rudi kabatini kachukue chaki mkuu. Unazo and you live in, kwa mujibu wako.

Mnachopendekeza katika S2 ni kuwa na wabunge 81 ambao wanalipiwa na Tanganyika.

Hivyo mnafanya bunge kama sehemu ya ajira ghali sana za wazanzibar tukijua hawana lolote la kuchangia in terms of cost or idea.

Hawana! si kila siku tunawasikia wakililia nafasi za ubalozi(upuuzi sana), mkuu wa jeshi na IGP(wendawazimu)?
Lini umesikia mznz akizungumzia muungano bila kulalamika wanaonewa.

Halafu wanachoongelea hakiwahusu. Wizara ya afya, Kilimo, ujenzi, mali asili, miundo mbinu n.k haziwahusu.
Ardhi wamekataa yao isiwe ya muungano, leo munawaweka Dodoma wazungumzie ardhi ya Tanganyika kama yao.

Hivi hamuoni hawa watu wamewalisha limbwata.

Halafu jiulize ni wangapi. 1.2 nusu yao wanaishi Tanganyika. Nini cha kudhani ni muhimu kwa hao laki laki 5 kiasi cha kuwavuruga akili hadi mnashindwa kuona hata mkiibiwa

Wana zao na hizi zetu wamekataa kwa mujibu wa katiba yao ya 2010. Sasa tuite watu waje Dodoma kutalii na kupiga soga tukiwalipa mishahara mikubwa for nothing! absolutely nothing. No input of any kind you can imagine. Please

Nikuulize hiyo investment tunayofanya kwa hawa wadai ubalozi na IGP inatusaidia nini down the road.
 
Well, bunge la S3 kama shirikisho lina idadi ya wajumbe kutoka znz na Tanganyika ambao ni fixed. Kutakuwa na jumla ya 55 kwa mujibu wa rasimu.
Kama sikosei znz watakuwa 20 na Tanganyika 75, sina uhakika lakini ni karibia na hapo.

Kilichotumika na tume ni kutumia wilaya zilizopo kufikia idadi. Hebu someni muelewe.
Haikusema wabunge watategemea kuongezeka kwa wilaya.Someni muelewe kwanza msikurupuke tu

Zanzibar inaweza kuwa na wilaya 600 baada ya hapo, hilo halitaongeza idadi yao katika Bunge la shirikisho kwasababu ipo stated.
.
Ipo stated wapi?? Soma vifungu nilivyokupa, halafu ndio ujadili.

Wajumbe watatoka kila mkoa Tanzania Bara na kila wilaya Zanzibar.
Hakuna neno fixed, na hakuna tarakimu yeyote iliyoandikwa kwenye vifungu hivyo vya katiba. hakuna idadi fixed iliyowekwa kwenye katiba kama unavyotaka kutuelewesha.

hakuna neno 20 wala hakuna neno 50 .... hizo ni tarakimu unazojaribu kuja nazo kwa kusikiliza midahalo, siyo zilipzopo kikatba. na hakuna nguvu ya kupanga majimbo na wilaya na mikoa kwa Serikali ya Muungano.
 
OK baadaye kidogo nitadurusu tena na tena halafu tutajadiliana.
 
Nguruvi3,
Mkuu swadakta leo umerudi mwenyewe katika mstari ambao mimi nataka kuwafahamisha wananchi. Rasimu imezungumzia kutakuwa na wabunge wasiozidi 70 kwa maana ya kwamba tunachokiunda hapa ni SHIRIKISHO baada ya kuua Muungano kama tulivyo katika EAC yaani Tanganyika na Zanzibar zitakuwa nchi zenye uhuru kamili ktk mambo tusiyoungana. Na ndio maana hiyo serikali ya muungano itakuwa ya kipekee ktk miungano yote ilowahi kutokea maana tunaungana upya pasipo Tanganyika kuwepo kwanza ila tunaunda kwanza Shirikisho pasipo Tanganyika halafu ndio tuje kuunda Tanganyika baada ya Shirikisho...

Na ndio maana rasimu imependekeza hata wabunge hawa wawe wa uuwiano baina ya wanawake na wanaume, na tutawachagua kama tulivyowachagua kina Shyrose, hivyo kinachofanyika hapa ni kuuvunja Muungano na kuunda Shirikisho kama ilivyo mahusiano ya Tanzania na Kenya ambako tuna mahusiano ktk mambo yalokubaliwa tushirikiane, lakini tofauti yake ni kwamba Tanzania tumepeleka wawakilishi wetu kufanya maridhiano kabla ya kuunda EAC kwa kuzingatia maslahi yetu na sheria zetu.

Sasa tunapokuja hapo kwenye hii rasimu ndipo mimi nasema sisi wengine hatuitazami Zanzibar kama Kenya ili tuanzishe ushirikiano bali Zanzibar ni sehemu ya taifa letu ni nchi moja na tungependa Kenya Uganda na Rwanda wajiunge na Umoja huu huko mbeleni.
Matatizo yaliyopo ktk umoja wetu sii ya kuvunja Muungano bali kuyatafutia ufumbuzi na kuyamaliza kwa sababu sii magumu hivyo. Nimeisoma rasimu wanapendekeza hiyo serikali itakuwa na wabunge wasiozidi 70 ambao watakuwa hawawakilishi wananchi bali wanawakilisha mambo ya Muungano kama ilivyo EAC. Huu ni mfumo mbovu zaidi unajenga umimi kwa kila upande kutazama kwanza interest zake. Na hizi interest ndizo zimetukwamisha ktk Jumuiya ya EAC kutokana na kwamba hatuaminiani. Na kutoaminiana kunaaza kujitokeza kwa nguvu kubwa baina yetu na Zanzibar.

Hivi niwaulizeni nyie hao wabunge wa EAC wamewawezesha nini zaidi ambacho kweli leo kodi zenu mna uhakika zinatumika vizuri? Je ushirika huu unaopendekezwa na rasimu hatungeweza kuupata kama tukiachana kabisa, sote tujiunge na EAC na hivyo ziwe nchi mbili tofauti? lakini kwa nini tufikie kufanya hivyo!
 
Nikuulize hiyo investment tunayofanya kwa hawa wadai ubalozi na IGP inatusaidia nini down the road.
Mkandara atakueleza Kwamba ni udugu, umoja na mshikamano in a panafricanist fashion. Hakuna ubishi Kwamba muungano baina ya Tanganyika na Zanzibar was a political union, nothing economical. Ndio maana hadi Leo, watetezi wake wanasimamia hoja za kisiasa kuliko kiuchumi. Swali linalofuata ni je: this political union - does it demonstrate a success story of panafricanist unity or it's failure? Jibu ni the later - it's failure. Why? Kwa sababu umetawaliwa zaidi na political mobilization kuliko economic calculations. And any successful union baina ya nchi is built on an economic foundation, political? Never, and there's hasn't been any case study of that nature.

Sent from my iPhone using JamiiForums
 
Last edited by a moderator:
Yani tusidanganyane kisiasa, s3 ni kujitwika mizigo isiyo ya lazima, kwani znz ipewe upendeleo wa wazi kihiivyo kwenye karne ya fair competition ambayo ndo hii kwa misingi gani na sababu zipi za msingi.

Gharama za maisaha zinapanda kila siku, badala ya kuwa na mfumo nbora wa kiutawala na fair distribution ya National cake ndo kwanza tunaongeza wingi wa watawala ambao hadi leo bado wao ndo sababu Tz haijakaa sawa kimsendeleo. Nilidhani waTz watakumbuka vyema tumetoka wapi na wapi tunapelekwa badala ya wapi tunataka kwenda. Ni wakati wa kuchukuwa maamuzi ya kikubwa sasa, takwimu zimeanza kuandikwa hata kabla hatujazaliwa kwa hiyo ni kitu cha muhimu sana kukizingatia kama kinaleta faida kwa Uma.

Tujenge serikali itakayo tukomboa waTz sio kwa kuwa s3 ama s2 (yaani kwa kuangalia ukubwa wake) bali ni kwa kangalia ufanisi na nguvu ya serikali hiyo katika kumkomboa Mtz.

Serikali ikiwa nI moja na watu wake ni Wtz hapo hakutakuwa na mimi Mzanzibari na wale ni Watanganyika ila itakuwa mimi Mtanzania na yule ni Mtanzania mwenzangu.

Tujenge taifa kwa upendo na sio vinginevyo
 
Mkandara atakueleza Kwamba ni udugu, umoja na mshikamano in a panafricanist fashion. Hakuna ubishi Kwamba muungano baina ya Tanganyika na Zanzibar was a political union, nothing economical. Ndio maana hadi Leo, watetezi wake wanasimamia hoja za kisiasa kuliko kiuchumi. Swali linalofuata ni je: this political union - does it demonstrate a success story of panafricanist unity or it's failure? Jibu ni the later - it's failure. Why? Kwa sababu umetawaliwa zaidi na political mobilization kuliko economic calculations. And any successful union baina ya nchi is built on an economic foundation, political? Never, and there's hasn't been any case study of that nature.

Sent from my iPhone using JamiiForums
Mkuu wangu Muungano wa nchi gani usiokuwa wa Political ama unazungumzia Jumuiya kama ya EAC na nchi za Ulaya maana hueleweki unaposimama. Nchi gani zimeungana kuunda Taifa moja na haikuwa Political na Kiuchumi?
 
Nyerere alijaribu, si unasikia ya znz kumlaani kila siku tena viongozi wake wakiwa kimya? Nani mwingine unaeoona ataweza?

Mbona hujaalani znz kujitoa katika muungano?
 
Ebu Nijibu hili swali:
Political federation or unity huwa Inakuja Katika hatua gani ya integration?

Sent from my iPhone using JamiiForums
 
Mkandara atakueleza Kwamba ni udugu, umoja na mshikamano in a panafricanist fashion. Hakuna ubishi Kwamba muungano baina ya Tanganyika na Zanzibar was a political union, nothing economical. Ndio maana hadi Leo, watetezi wake wanasimamia hoja za kisiasa kuliko kiuchumi. Swali linalofuata ni je: this political union - does it demonstrate a success story of panafricanist unity or it's failure? Jibu ni the later - it's failure. Why? Kwa sababu umetawaliwa zaidi na political mobilization kuliko economic calculations. And any successful union baina ya nchi is built on an economic foundation, political? Never, and there's hasn't been any case study of that nature.
Mwambie hivi, Russia ilikuwa nchi moja. Choko choko za kuisambaratisha zilichagizwa sana na uchumi. Perostroika.

Leo wanaanza kufikiria kurudi kwasababu za kiuchumi.
EU ipo kwasababu za kiuchumi, vinginevyo walikuwa na NATO siku nyingi.

BRICK imeundwa kwa nguvu za kicuhumi, si uzuri wa Zuma, Putin au mwingine.
EAC ya sasa inaundwa kiuchumi. Kilichoua ya 1967 ni siasa zaidi ya uchumi.

Wanaogopa kuzungumzia uchumi kwasababu utaua hoja zake. Imbalance and injustice is unjustifiable.
 
Nyerere alijaribu, si unasikia ya znz kumlaani kila siku tena viongozi wake wakiwa kimya? Nani mwingine unaeoona ataweza?

Mbona hujaalani znz kujitoa katika muungano?
Mkuu unalazimisha vitu visivyokuwepo hata kama tumeelezwa vizuri tu. hapakuwepo na Muungano isipokuwa muungano wa watu wake hata kabla ya Uhuru. Ni jinsi jamii hii ilivyo ndivyo tulivyounda Utaifa wetu kama kiswahili kilikuwepo hata kabla ya kukifanya lugha ya taifa, Muungano, katiba na sharia ni kuhakikisha jambo hilo linatambulika kimataifa na amrisho kwetu sote kutambua mipaka yake.

Sheria mama ilokuwa ikitungwa ilikuwa ya Tanganyika na hivyo moja kwa moja kuwa ya Tanzania, hivyo Zanzibar hawakutakiwa kuikiuka kutokana na kuwa katiba mama. Wao wamekuja gundua sheria hizi zilitungwa kwa minajiri ya Tanganyika zaidi ya Muungano wetu na ndio maana walihitaji ridhaa yetu wakati sisi hatuhitaji ridhaa yao. Yaani what we like inaingia katika katiba kumbe ni katiba mama na kuwalazimu wao wafuate maana hii ni sheria mama. Wakaona Uhuru wao unapotea na ndio mwanzo wa kudai mamlaka kamili.

Hivyo nakubaliana na S3 ikiwa tu serikali hiyo kuu itakuwa ya Muungano na sio ya Shirikisho na serikali zote za bara na visiwani zitapewa mamlaka madogo ambayo hayatapingana na sheria mama na bila kuepuka mahitaji ya wananchi. Sheria mama itayagusa mambo yote yanayoijenga jamii yetu na kuacha mengine tunayo tofautiana kuwa mikononi mwa serikali hizo upande wa sheria na utekelezaji. Bara tukiamua ushoga halali sii lazima sheria hiyo itumike Zanzibar ila sheria ya Muungano ikisema ndoa za kishoga haramu basi ni haramu kote sio kwa sababu bara wanataka kuharamisha bali bunge la Muungano limekubaliana kuharamisha kutokana na matakwa ya wananchi.

Kifupi tumeshindwa kutenganisha katiba (sheria mama) inayohusu JMT na katiba ya Tanganyika na ndio maana Warioba na tume yake wamependekeza kuundwa kwa serikali 3 ili tujenge sheria za Kitaifa, na kila nchi iwe na mamlaka ya sheria zake ndogo za kinchi.
 
Mkandara atakueleza Kwamba ni udugu, umoja na mshikamano in a panafricanist fashion. Hakuna ubishi Kwamba muungano baina ya Tanganyika na Zanzibar was a political union, nothing economical. Ndio maana hadi Leo, watetezi wake wanasimamia hoja za kisiasa kuliko kiuchumi. Swali linalofuata ni je: this political union - does it demonstrate a success story of panafricanist unity or it's failure? Jibu ni the later - it's failure. Why? Kwa sababu umetawaliwa zaidi na political mobilization kuliko economic calculations. And any successful union baina ya nchi is built on an economic foundation, political? Never, and there's hasn't been any case study.

Sent from my iPhone using JamiiForums
Nje ya chaki, ila hapo kwenye nyekundu....

Muungano kati ya England na Scotland, Ireland na Wales ulikuwa based on economic foundation? Tuelezee how.
Je muungano huu ni failure? (Set aside the refferrendum).

EAC ni success story in your views? Tuelezee how is it successful compared to SADC (as a Tanzanian).
Je, EAC na SADC ni muungano upi upo more political in your view? As to, how politically mobilize/harmonized is EAC compared to SADC?

Is African Union a more Political Union than Economic? Is it a failure? Je, OAU na AU ni ipi ilkuwa more politically mobilized na ipi ipo relatively more coherent?

Political mobilization is a precedent to a better economic union, if you ask me. And not otherwise..... Ila tusiharibu mada kwa kuanzisha mambo mengine.
 
Mwambie hivi, Russia ilikuwa nchi moja. Choko choko za kuisambaratisha zilichagizwa sana na uchumi. Perostroika.

Leo wanaanza kufikiria kurudi kwasababu za kiuchumi.
EU ipo kwasababu za kiuchumi, vinginevyo walikuwa na NATO siku nyingi.

BRICK imeundwa kwa nguvu za kicuhumi, si uzuri wa Zuma, Putin au mwingine.
EAC ya sasa inaundwa kiuchumi. Kilichoua ya 1967 ni siasa zaidi ya uchumi.

Wanaogopa kuzungumzia uchumi kwasababu utaua hoja zake. Imbalance and injustice is unjustifiable.
Mkuu unazungumza vitu gani hapa. Kwani Germany haina Muungano wa nchi yake, Uingereza, Uswiss japo haimo, na kadhalika iweje leo wewe ufananishe Urusi na EU ama kusema ati NATO ni muungano wa nchi? Hiyo Marekani mshirika wa NATO anapakana vipi na nchi za Ulaya? Marekani wana nchi 50 zilizoungana ni kwa sababu ya Kiuchumi? aaah mnachosha nyie...Kifupi mnaonyesha jinsi msivyokuwa na uelewa wa Muungano ama tunabishana juu ya nini..ndio maana hamtulii na hoja mkibanwa huku mnarukia kwingine.

NB: wanaokutana huo kwenye mikutano ya siri ya EAC inayomtenga JK sii siasa? Dunia ya leo utaweza vipi kutenganisha Siasa na Uchumi katina uongozi wa nchi.
 
Back
Top Bottom