Sera ya 'Maridhiano' ya Samia Suluhu inarudisha wizi Serikalini

Poppy Hatonn

JF-Expert Member
Apr 9, 2021
2,101
2,712
Watanzania wanajua rais wanayemtaka. Wanataka rais ambaye ata- sacrifice maisha yake kulinda rasilmali za nchi lakini hapa tunaye rais anayeongea kuhusu maridhiano na anawawezesha watu kuiba tena.

Si ndio maana watu walikuwa wanauliza kama mwanamke anaiweza hii kazi ya urais. Rais hachaguliwi ili aonyeshe jinsi alivyokuwa na huruma. Rais anapaswa kutenda haki.

Tunataka maridhiano au tunataka rasilmali za nchi ziwe salama? Again tunasema,rais anafanya mambo mengi mechanical. Anapanga safu yake lakini kazi inakuwa too intimidating. Kama wamemdukua Mwendazake,watanishindwa mimi?

Ndio hapa watu wanakwama. Wanasema kazi iendelee lakini kazi haiendelei. Watu wanakamatwa red-handed tunaambiwa wakae kando wapishe uchunguzi,watu ambao Magufuli angewashughulikia papo kwa papo,mbele ya watu wengi wanamshangilia.
 
Yule aliyewajengea wakwe zake daraja la busisi kwa bilioni 700 hakuwa mwizi?

Akajijengea uwanja wa ndege kijijini kwake hakuwa mwizi?

Anawatuma sabaya na makonda wanyang'anye pesa wafanyabiashara hakuwa mwizi?

Kaa kwa kutulia wewe uliyekata tamaa ya kuishi baada ya mwizi mkuu kutoka chato kudanja!
 
Basi ingelikuwa ndivyo hivyo "kusingelikuwa na haja ya kuwa na "mahakama... mapolisi... Takukuru... uhamiaji... na... na... na..." zaidi ya yote tusingelihitaji katiba wala utawala wa sheria!!!

Kimsingi nchi huendeshwa na taasisi imara na si mpiga firimbi mmoja mwenye wapambe wasiojielewa wanataka nini... fitna aliyoiacha itapotea kama unyevu jua liwakapo "wanyonge bhana!"
 
ndo maana nasemaga hakuna mzenji mwenye akili!!
anyway maza hali halisi itamshep tuu
Ukitaka kutofautisha wenye akili na wasio sikiliza kauli ama soma maandiko kisha tazama msemaji na washangiliaji wake... "....huyu ni kichaa kama mimi!!!"
 
Mwendazake alikuwa anaiba mwenyewe na hakutaka Mtanzania mwingine aibe. Imagine Tsh 2.4 Trillion kwa miaka 3 ambazo CAG alizihoji.

Wale ambao Mwendazake alikurupuka kuwa wameiba na akawaweka rumande kwa kufungua mashtaka ya kuhujumu uchumi, kesi zao bado hazina ushahidi kuanzia 2016 hadi 2021 ambapo amekufa na kuzikwa.

Ibara 13 ya Katiba ya JMT inatamka kuwa kila mtu ni innocent unless proven guilty by the court of law.

Acheni Utawala wa sheria uchukue nafasi, UDIKTETA tuliuzika rasmi na Magufuli mnamo Machi 27/03/2021
 
Hivi ni toka lini makada wa chama tawala waliojazana na kupewa vyeo ndani ya serikali wamewahi kuuacha kuiba na kufanya ufisadi wa fedha za umma? Ukiona pesa zimepigwa ujue tu hiyo ni "syndicate" ambapo ndani yake "beneficiaries' ni wengi.

Hata wakati wa mwendazake hali ilikuwa ni hiyo hiyo tu, isipokuwa jamaa alikandamiza mno uhuru wa kupatikana kwa habari. Mama Samia, Rais wetu ndiyo kwanza ana siku zisizozidi 100 tangu aishike nafasi hiyo nyeti. Kwa hiyo bado ana muda wa kujipanga zaidi ili kuiweka nchi ktk mstari sahihi.
 
Mwendazake alikuwa anaiba mwenyewe na hakutaka Mtanzania mwingine aibe. Imagine Tsh 2.4 Trillion kwa miaka 3 ambazo CAG alizihoji.

Wale ambao Mwendazake alikurupuka kuwa wameiba na akawaweka rumande kwa kufungua mashtaka ya kuhujumu uchumi, kesi zao bado hazina ushahidi kuanzia 2016 hadi 2021 ambapo amekufa na kuzikwa...
Tuonyeshe zilipo fichwa Basi na ID take ya Tumbili sa sijui ndo akili imekaa kitumbilitumbili
 
Subiri matokeo usiwe na haraka kila uongozi na staili yake, ukiona imepita kimyakimya aanza kulaumu.
Tunasubili tuone,

Kuna mtu ameacha mabasibya udongo ndaki wakati angelipa hata vijana waoshaji laki moja kila gari na mabasi hayo yangekua salama lakin unaacha yanaoza kisha unayakarabati kwa milioni 50 kila moja.

Bado mtu huyo yupo ofisini anadunda tu.
 
Umeanza vizuri ila umemaliza vibaya. Siyo kuwadhalilisha watu,ila ni kuacha sheria ifanye kazi bila shinikizo.Kama kuna mharifu vyombo husika vishughulikie na inyeshe vinashugulikia.

Siyo Rais kusimama majukwani na kuuliza mnataka nimfanye nini huyu nimtumbue! waty tumbuaaaa! Hiyo haija kaa kitaasisi.maana kuna majungu pia tusisahau,bila macho ya ziada unaweza ukawa unashughulikia kutekeleza majungu ya watu.
 
Si mnataka hela zirudi mtaani ili bavicha wawe wanaziokota?
 
Ha
Wizi ni tabia,mawazo ya Raisi hayasababishi wizi.
Hata mkeo ukimruhusu kwenda disco peke yake kila siku ipo siku atataka alale huko pia.

Kwa hiyo raisi ni nembo ya kuzuia hayo.

Akilegea tu kila kitu kinalegea.

Ukitaka kujua hilo anza kuiba vi kuku vya watu unakuja navyo nyumbani, na ipo siku utakuta mwanao nae kaja na kifaranga cha kuku
 
Tuonyeshe zilipo fichwa Basi na ID take ya Tumbili sa sijui ndo akili imekaa kitumbilitumbili
Magufuli alitumia fedha ya Serikali HOVYO ikiwa ni pamoja na;
1. Kujengea miundombinu Kama ya Uwanja wa Ndege, Hospitali ya Rufaa kijijini kwake Chato

2. Kununua wabunge wa CHADEMA/CUF akina Gekul, Mollel, Silinde, Waitara, Mtulia

3. Kugawa fedha barabarani na kwa mahawara kama akina Jokate, Tulia na Kairuki
 
Back
Top Bottom