neno "Jimbo" ni jina la sehemu ya nchi kama ilivyo kwa Mkoa, Wilaya na kadhalika. Tofauti kubwa ni jinsi ya kuendesha utawala. Tanzania tunafuata mfumo msonge (centralized) ambapo kila sehemu ya nchi inatawaliwa na msonge, yaani rais. Huyu atateua wakuu wa wilaya, na wakuu wa mikoa, ambao kwa niaba yake nao watateuwa viongozi wengine ngazi za kata na tarafa. Kwa bahati mbaya, chini ya mfumo huo, viongozi wale wako pale kwa niaba ya rais na wala hawajibiki kwa raia waanaowaongoza. Iwapo viongozi hao wasipotekeleza wajibu wa sawasawa, basi itabidi wananchi wale wakalalmike kwa rais kwani hawana mamlaka ya kuwaadhibu. Mipango yote ya maendeleo katika mkoa inategemea ridhaa ya serikali kuu ya Rais. Ingawa kuna serikali za mitaa, zote hizi siyo huru kujifanyia mambo yao kwani zote ziko chini ya ofisi ya waziri mkuu. Utawala wa namna hii ni goigoi sana, na unaleta ukiritimba na vile vile kuimarisha uimra.
Katika utawala uliopewa jina la sera za majimbo, kila sehemu ya nchi inakuwa na utawala wake kukidhi mahitaji ya raia wake bila kuitegemea serikali kuu. Raia watawachagua viongozi wao wa jimbo ambao wanawajibika moja kwa moja kwa wanachi, siyo kwa Rais. Kwa hiyo endapo viongozi hao wakiboronga, basi wananchi wana mamlaka ya kuwafukuza kazi bila kusubiri rais afanye hivyo. Mipango yote ya maendeleo ya wananchi inapangwa huko huko kwa wananchi na vingozi wao, mfumo huo unaweza kujulikana kama decentralized ama amadaraka mikoni lakini siyo kama ule mfumo uliokuwa umejengwa na Nyerere miaka ya sabini. Kwa kawaida mfumo wa aina hii ni efficient sana. Nchi nyingi kubwa zinatumia mfumo wa aina hiyo, Utaona huko Marekani pamoja na kuwapo Obama pale White House, majimbo yote ya Marekani yana magavana wake ambao wamechaguliwa na wananachi, na wanaweza kuondolewa madarakani na wanachi hao bila kumhusisha Obama. Kwa mfano Kalifonia walimwondoa Gavana wao Gray Davis na kumweka huyu aliyeko Arnold Schwarzenegger kwa mtindo huo huo bila kumhusisha George Bush (wakati huo). Ndai ya jimbo pia kuna viongozi wa wilaya (counties) ambao nao huchaguliwa na wananchi wao. Vivyo hivyo ndivyo inavyofanyika Canada, Australia na sehemu nyingi za Ulaya.
Kujenga mfumo huo kunahitaji mabadiliko makubwa sana kwenye Katiba yetu ili kumpunguzia madaraka rais wa nchi, na vile vile kupunguza mabavu ya serikali kwenye maisha ya kila siku ya raia. Chini ya utawala wa majimbo, kunakuwa na polisi wa aina mbili: wale wanaoshughulikia mambo ya kitaifa, na wale wanaoshughulika na mambo local. Polisi local wameajiriwa na serikali ya wananchi wa pale na wanawajibika kwa raia wa hapo, hivyo hawawezi kuwanyanyasa raia wao kama ambavyo imekuwa inafanyika Tanzania.
Kuna faida anyingi sana za utawala wa majimbo ikiwa ni pamoja na kuchochea ushindani wa majimbo; ni vigumu kuzichambua zote kwenye post hii fupi. Pamoja na faida hizo, pia utawala wa namna hiyo unaweza kuchochea kukua kwa ukabila nchini hasa kwenye chaguzi za serikali local. Itategemea sana jinsi katiba itakavyokuwa imeandikwa ili kuepusha hali hiyo.
kuendesha mfumo wa aina hii, inabidi katiba ya nchi i