Kuna karani mmoja rafiki yangu yeye kapangiwa Mwananyamala Kisiwani ananiambia mpaka saa 9 kaishahesabu nyumba 12 tu kila nyumba akiingia anakutana na upinzani mkali watu hawataki kuhesabiwa.
Mtaani kwetu yamejaa mabango ya(mimi muislam sihesabiwi) hivyo makarani wanapita tuu...cjui itakuwaje?
Ukistaajabu ya Mussa utaona ya Firauni. Kuna mtu katembelewa na karani wa sensa na akawajuza wadau wake kwamba yule karani aidha ana uwezo mdogo sana wa kusoma na imechukua saa nne kukamilisha mahaojiano!!! Kwa spidi hii ya saa tatu kaya moja si katika siku moja (12 day light hours) karani huyu atapitia kaya tatu tu, na kwa mtaa aliopangiwa karani kama huyu atachukua miezi miwili kumaliza. Sijui ndiyo laana ya kuwaacha waalimu, au huyu karani alikuwa anategea lunch ya dezo maana labda hajalipwa posho ya kazi.
Ni takriban dakika 10 zilizopita nimekuwa na ugeni nyumbani kwangu wa karani wa sensa na imenichukua kama dakika 7 au 8 hivi kukamilisha zoezi zima la kuhesbiwa. Maswali aliyouliza ni watu wangapi wamelala kwenye nyumba usiku wa kuamkia leo, umri wa kila mmoja, elimu yao, je mko katika mfuko wa hifadhi ya jamii au bima ya afya, kuna mlemavu yeyote katika familia, kuna kifo chochote kimetokea kati ya mwaka jana na sasa, kuna ndugu yeyote yuko nje ya nchi? Ni hayo tu, nawasihi wale wanaoogopa na kuhofia mambo kibao wasifanye hivyo maana ni very interesting. I suggest tuwape ushirikiano makarani wa sensa maana takwimu hizi zitatumika kwa miaka 10 mbele hivyo ni muhimu sana. I wish you all the best, week end njema!
Nijuavyo mimi sensa itaendelea through 7days. Sasa kisa cha kuwasimamisha abiria ninini? Na wewe umekubaliana na jambo hilo?
Ungekuwa uchaguzi ningeelewa.
Mtaani kwetu yamejaa mabango ya(mimi muislam sihesabiwi) hivyo makarani wanapita tuu...cjui itakuwaje?
Wakuu,
Naisikitikia sana nchi yangu Tanzania. Raia tumeanza kuongea lugha tofauti kama wajenzi wa mnara wa babeli.
Yatupasa kuchukua hatua kurekebisha hali hii, wananchi waipende nchi yao, wajivunie utanzania wao, wakisikia kuna sensa wajitokeze kwa wingi kuhesabiwa. Tumekosea wapi? Tuliowapa madaraka ya kutuongoza hawaoni tatizo?
Ingewezekana kabisa kufanya sensa, vitambulisho vya taifa na daftari la kudumu la wapiga kura kama zoezi moja, na tungeokoa pesa nyingi za watanzania ambazo zingetumika katika shughuli nyingine za maendeleo, tuliowapa madaraka ya kutuamulia hawawezi kuliona hili.
Hata hivyo nitarudi nyumbani kesho jioni, (unless nipate tatizo la flight connection), na ikiwezekana nitahesabiwa. Siyo safari maalum kwa ajili ya sensa ( is just a coincidence)!
Ni muhimu sana tukajua idadi yetu na uwezo wetu katika nyanja muhimu ili tuweze kupambana na changamoto za maisha ya hapa duniani.
Mpaka sasa, idadi kubwa ya waislamu wamegoma laivu bila kujificha. Msikubali kudanganywa. Watu wengi nilio ongea nao wameniambia wamekataa kuandikishwa. Nimeaongea na mwandishi mmoja wa sensa akaniambia hali ni tete serekali imekula hasara kwa kiburi chao. Tunasubiri mswada bungeni wa kutokua na imani na rahisi. Tuchague raisi mwengine.