Taarifa zilizonifikia ni kwamba;
Kama kichwa kinavyo jieleza tukio limetokea leo Halmashauri ya Wilaya ya BUCHOSA wilaya ya SENGEREMA MKOA WA MWANZA ambapo Afisa mmoja wa TAKUKURU amemlamba makofi mwalimu wa kike (jina linaifadhiwa) wa shule ya msingi (jina linahifadhiwa) wakati wa uhakiki wa vyeti kwa watumishi wote wa umma wa Halmashauri hiyo kwa kosa la kusimama nyuma yake wakati zoezi likiendelea.
Afisa huyo anashikiliwa na polisi mpaka sasa, kwenye kituo cha polisi cha KATA YA NYEHUNGE ambapo zoezi hilo linafanyika, wakati mwalimu akiwa hospitali kwa matibabu ya michubuko aliyoyapata.
Hii ni mwendelezo wa vichapo na udhalilishaji kwa waalimu ambao wanaonekana kutokuwa nathamani mbele ya kada zingine za kiutumishi.
Mpaka sasa suala hilo lipo mikononi mwa polisi, wizara usika na vyombo vyenye dhamana mtende haki kulinda heshma ya mwalimu.