SENGEREMA: Afisa TAKUKURU amlamba mwalimu makofi

SENGEREMA: Afisa TAKUKURU amlamba mwalimu makofi

yoga

JF-Expert Member
Joined
Jan 6, 2013
Posts
2,004
Reaction score
10,388
Taarifa zilizonifikia ni kwamba;

Kama kichwa kinavyo jieleza tukio limetokea leo Halmashauri ya Wilaya ya BUCHOSA wilaya ya SENGEREMA MKOA WA MWANZA ambapo Afisa mmoja wa TAKUKURU amemlamba makofi mwalimu wa kike (jina linaifadhiwa) wa shule ya msingi (jina linahifadhiwa) wakati wa uhakiki wa vyeti kwa watumishi wote wa umma wa Halmashauri hiyo kwa kosa la kusimama nyuma yake wakati zoezi likiendelea.

Afisa huyo anashikiliwa na polisi mpaka sasa, kwenye kituo cha polisi cha KATA YA NYEHUNGE ambapo zoezi hilo linafanyika, wakati mwalimu akiwa hospitali kwa matibabu ya michubuko aliyoyapata.

Hii ni mwendelezo wa vichapo na udhalilishaji kwa waalimu ambao wanaonekana kutokuwa nathamani mbele ya kada zingine za kiutumishi.

Mpaka sasa suala hilo lipo mikononi mwa polisi, wizara usika na vyombo vyenye dhamana mtende haki kulinda heshma ya mwalimu.
 
Tutalajie kushuka kwa kiwango cha elimu nchini sababu serikali imeshindwa kuwathamini walimu....
 
Sheria ifate mkondo wake atamzabuaje vibao kwa kosa la kusimama nyuma yake...walimu mna mateso sana
 
Msilikuzeee sana hiyo ni involuntary act inaweza kukutokea, iliwahi kukutokea na baada ya kitendo unajilaumu mwenyewe kwa kile ulichokitenda. Duniani kuna viumbe wengine wasioonekana wanaoweza ku ku control bila wewe kujijua hivyo wakati unalaumu hilo jiangalie wewe mwenyewe hujawahi kukutwa na kitu kama hicho au kinachofanana na hicho?
 
Pole yake teacher.Kofi moja mpaka hospital.
 
jaman walimu. ila huyo mtakukuru amefanya makosa kwa nini achukue sheria mkononi? kama huyo mwalimu alifanya kosa alipaswa ampeleke kwenye vyombo husika na si kumpiga. kwa mfano angefanya mwanajeshi angempiga? imefikia wakati walim tumechoka kuonewe
 
[emoji16][emoji16][emoji16] acha kumzarau mwanamke!!!
Sijamdharau mwanamke ila nimepost hali halisi. Kwani ukisema wanawake wanapenda kujiremba ni dharau?

Nisamehe bure kama nimekosea
 
Back
Top Bottom