Senegal kuingia Gambia Ifikapo saa 6 kamili usiku

Senegal kuingia Gambia Ifikapo saa 6 kamili usiku

Huyu rais wa Gambia ni mbishi sana.Hivi kwanini sisi waafrika ni wabinafsi sana?Hili nafikiri lisiishie kwa Gambia.AU inabidi wawe na chombo cha kusinamia katiba za nchi wanachama.wawa lazimishe nchi wanachama wawe na tume huru za uchaguzi.kiongozi wa nchi asibadilishe katiba bila kupata idhini kwa AU.Hii itasaidia viongozi kutochezea katiba kwa matakwa yao.
AU ynyw inaundwa na hao hao,unawezaje kutoa kibanz kilichopo ktk jcho la mwenzio kabla ya kutoa borit iliyo ndan ya jcho lko?
 
Duh, Barrow kuapishwa katika ubalozi wa Gambia nchini Senegal.
 
Huyu rais wa Gambia ni mbishi sana.Hivi kwanini sisi waafrika ni wabinafsi sana?Hili nafikiri lisiishie kwa Gambia.AU inabidi wawe na chombo cha kusinamia katiba za nchi wanachama.wawa lazimishe nchi wanachama wawe na tume huru za uchaguzi.kiongozi wa nchi asibadilishe katiba bila kupata idhini kwa AU.Hii itasaidia viongozi kutochezea katiba kwa matakwa yao.
Kusimamia katiba ya nchi flan isibadilishwe hadi kwa idhin ya AU halitowezekana coz viongozi karibu wote wana tabia moja ya uroho na ulevi wa madaraka.
 
Sasa si tutakuwa tunawaonea majirani tu, hivi ikitokea rais wa Tz akagoma kama Jammeh unadhani nchi kama kenya,uganda rwanda na burundi zina ujasiri wa kusogelea mpaka wa Tanzania! Jammeh anatishiwa kwa sababu nchi yake haina nguvu ya kijeshi.


Vita ya haki dhidi ya dhulma.
Haki ni lazima ishinde.
Usipime Idi Amin Dada alikua na Jeshi zuri na zana kali sana za kivita lakini wananchi wake waligawanyika kisiasa na wanajeshi wengi walikua wameshaasi.

Kwetu tuombe Mungu yasitukute.
Ikatokea mtu yeyote akawa Rais halafu akaongeza Muda wake na wananchi wakamchoka ujue hata ndani ya majeshi wapo wengi waliomchoka. Na hakuna anayeweza kutoa uhai wake kwa ajili ya mtu aliyeongeza muda kwa tamaa yake na marafiki zake wachach ndani ya vyombo vya dola.
Hali inakua ngumu kutokana na wapiganaji kugawanyika na kutoa siri kwa wavamizi.

Hakuna nchi yenye umoja inayoweza kushambuliwa kirahisi.
Mkishagawanyika kisiasa ujue hali sio nzuri ndani ya vyombo vya usalama.
Na pia ukumbuke wavamizi nao wana mashushu wao ndani ya vyombo vya dola ambao huwalipa zawadi nono kwa kuwasaidia.

Mfano ni ule wa Nchi za Magharibi kutangaza mabilioni ya dola kwa mtu anayefanikisha kuuawa kwa yule wanayemtaka. Ni mbinu za ushindi kwa wavamizi.

Ila tujiulize tu inakuaje kwa mtu anatawala kwa miaka mingi lakini bada anang'ania madarakani tena baada ya kushindwa uchaguzi.
Wafrika tubadilike na tuwakatae hawa watu walioshiba maisha bora na familia zao na marafiki zao na koo zao halafu wanatumia Majeshi kuendelea kujinufaisha kimadaraka na kiuchumi.
Mtu kuwa rais hata kwa miaka mitano ni heshma kubwa sana kama utakua umetimiza wajibu wako kwa haki na kwa amani.
Kiongozi bora ni yule anayeokoa maisha ya watu wake na kuepuka kumwaga damu kwa manufaa yake binafsi kisiasa.

Mungu Ibariki Afrika.
 
Back
Top Bottom