Senegal kuingia Gambia Ifikapo saa 6 kamili usiku

Kibo10

JF-Expert Member
Aug 20, 2013
11,277
8,859
Wanajeshi wa Senegal wako kwenye mpaka wa nchi hiyo na Gambia na wataingia Gambia iwapo Rais Yahya Jammeh hataondoka madarakani ifikapo saa sita usiku, hayo ni kwa mujibu wa msemaji wa Jeshi la Senegal kanali Abdou Ndiaye.
Ndiaye amesema iwapo hakutakuwa na suluhu lolote wakati huo basi wataingia Gambia.
Kiongozi wa upinzani Adama Barrow ambaye alishinda uchaguzi wa Desemba 2016 alipangiwa kuapishwa leo
 
Huyu rais wa Gambia ni mbishi sana.Hivi kwanini sisi waafrika ni wabinafsi sana?Hili nafikiri lisiishie kwa Gambia.AU inabidi wawe na chombo cha kusinamia katiba za nchi wanachama.wawa lazimishe nchi wanachama wawe na tume huru za uchaguzi.kiongozi wa nchi asibadilishe katiba bila kupata idhini kwa AU.Hii itasaidia viongozi kutochezea katiba kwa matakwa yao.
 
Sio senegal peke yake...majeshi ya senegal,nigeria,mali na togo yapo mpakani kwa gambia tayari
 
Akamatwe tu na kuondolewa kwa nguvu ili kulinda haki ya wenyenchi walioamua kuwa apumzike
 
Na afrika mashatiki tungekuwa ivi safisana lakin hata ashinde akishinda mpinzan tume lazima itie dosari kijan kiendelee kutawala
 
Afrika Mashariki tuwe na Jeshi letu tuwadhibiti viongozi wang'ang'anizi wa madaraka,
Sasa si tutakuwa tunawaonea majirani tu, hivi ikitokea rais wa Tz akagoma kama Jammeh unadhani nchi kama kenya,uganda rwanda na burundi zina ujasiri wa kusogelea mpaka wa Tanzania! Jammeh anatishiwa kwa sababu nchi yake haina nguvu ya kijeshi.
 
Back
Top Bottom