Sema chochote kwa Baba yako, leo Father's Day

Sema chochote kwa Baba yako, leo Father's Day

Sikuwahi jua umuhimu wake kwa ufasaha mpaka alipofariki. Zipo nyakati natamani uamke dakika japo 5 utoe muongozo kwa yanayonikabili then ulale lakini haiwezekani. Wenye baba na mmeshakuwa watu wazima, jaribuni kuwa sababu ya furaha kwao japo kwa mambo madogo tu. Kwenye utu uzima huwa hawahitaji mambo ya gharama sana.
 
Umekuwa baba mwema sana, kwa malezi yote, kuanzia nyumbani, kielimu hata kijamii pia, wewe ni zaidi ya vyote ktk maisha yangu, umesisitiza sana kuhusu elimu, ushirikiano, upendo, U a the great!! Saloote mshua!!
 
Pole sana rafiki yangu, ni kuendelea kumuombea apumzike kwa amani baba[emoji120]
Asante sana bestie. Take care of your dad please. Kuna tabia katika jamii zetu watoto kuelekeza upendo wote kwa mama zao na kuwaacha akina baba katika upweke na masononeko. Matokeo yake wanakufa mapema sana. Tupendeni na sie akina baba jamami. Tumepambana sana kulea familia zetu. Mungu Ampe dad wako maisha marefu na yenye furaha na amani [emoji120][emoji2536]
 
Nakushukuru mzee wangu kyaka kwa kunifundisha maisha ..nakumbuka ulipokea kipensheni chako 2012 Ila nilichoambulia ni pagara la vyumba vitatu ukasepa zako..mungu akuongoze na akuponye na mkeo huko ulipo..
 
Katika ukuaji wangu sikubahatika kuzoeana na mzee, alikua ile type ya washua makauzu. Alikua ananibutua ile mbaya, hadi ikafikia kipindi nnapoanza sekondari nikakimbilia kukaa kwa bibi. Baba alikua analipa ada kama kawa na ukauzu wake ukafanya safari yangu ya kielimu iwezekane.

Nilipoanza tu kidato cha tano nikaanza kukaa ghetto, kwa hiyo sikupata wasaa wa kuzoeana na mzee.

Nilipokuwa chuo mwaka wa tatu nilifanya ujinga mmoja ambao ungefanya masomo yangu yakomee hapo. Sikuwataarifu nyumbani mana ilikua soo ya aibu mno, sijui ilikuaje mzee akajua. Akaenda chuoni akaelekezwa kila kitu na dean, mzee alibembeleza sana pale (niliambiwa na mother), siku moja nikapigiwa simu chuoni kuwa niende ku clear baadhi ya vitu. Zile harakati zilikua na nenda rudi nyingi sana, na mara zote hizo mzee alikua analazimisha awepo. Kile kipindi ndio nilipata fursa ya kuwa karibu na mshua.

Japo hakutaka nione kwamba anaumizwa na ule ujinga nliofanya ila nililiona hilo machoni mwake (niliumia asee, sikutegemea kuja kuona upande huo wa yule jamaa).

Mungu sio sholo mwamba lile likapita, ni experience mbaya kuikumbuka lakini ilileta ukaribu sana na mzee, na zaidi nilipata nafasi ya kumjua vizuri. Hakuwa vile ambavyo nilikua namfikiria hapo awali,

Siku hizi kawa mshkaji wangu sana, asilimia kadhaa za mshahara wangu naziingiza kwenye account yake kila mwezi. Anapata kiasi kadhaa cha mapato yangu ya side hustle baada ya wiki mbili. Najua hiyo haitoshi kumlipa, na katu sijaribu kufanya hivyo..ila najivunia kuwa at least namuonesha kwamba najali.
 
Asante sana bestie. Take care of your dada please. Kuna tabia katika jamii zetu watoto kuelekeza upendo wote kwa mama zao na kuwaacha akina baba katika upweke na masononeko. Matokeo yake wanakufa mapema sana. Tupendeni na sie akina baba jamami. Tumepambana sana kulea familia zetu. Mungu Ampe dad wako maisha marefu na yenye furaha na amani [emoji120][emoji2536]
Amen to that na asante sana dear. Mchango wa akina baba ni mkubwa sana katika familia japo ndo hivyo wengine wamekengeuka ila ndo baba zetu hatuna budi kuwachkulia jinsi walivyo...
Mungu awabariki akina baba wote wanaopambana kwa ajili ya watoto + familia zao.
 
TAFADHALI

Kuna kitu nimejifunza. Siku ya mwanamke, ni ngumu sana mwanaume kuitamka kwa dhihaka. Inabebwa kiheshima na kwa thamani kubwa. Lakini siku ya Baba dhihaka ni kubwa sana.

Dhihaka hasa toka kwa wanawake ambao kwa kiherehere chao hawakuchagua mtu sahihi wakajiangusha kwa kijitu tu na kubeba mimba. Mwisho wanajipachika jina la kidwanzi la single mothers... utadhani kuna album mothers au double mothers.

Wewe single mother ushawahi kutafakari uzinzi wako uliofanya kabla ya kupachikwa usingle mother wako huo na kibwana chako huko mitaani? Je kosa lilikuwa la mwanaume au kiherehere chako cha kutaka kuona mama zako wanapata nini kwa wanaume?

Sasa UPUMBAVU wa kibwana chako ndo unataka kuipindua siku ya Wababa wenye majukumu yao iwe yenu kisa haraka zako za uasherati? Mmekuwa kama Wakenya kutaka kila kitu cha Tanzania kiwe chao. Nanyi siku ya Baba Duniani mnaitaka kwa kuita "Happy Father's Day kwa Single Mothers?"

Pambaneni na hali zenu.

"Happy Father's Day"
 
Back
Top Bottom